Msuya atueleze aliko Sokoine

Msuya atueleze aliko Sokoine

Tunapokaribia kuadhimisha miaka 31 tangu kilipotokea kifo kilichojaa utata cha aliyekuwa Waziri Mkuu Ndg.Edward Moringe Sokoine,ni wakati mwafaka sasa kumhoji Mh.Cleopa Msuya juu ya tuhuma za kuhusishwa na kifo cha Mh. Sokoine;kwa sababu Mh. Msuya kwa siku za karibuni amejitokeza kukemea maovu mbalimbali yanayofanywa na viongozi wa CCM bila shaka pia atakuwa na ujasiri wa kujitokeza na kutolea ufafanuzi wa tuhuma hizi.
R.I.P chacha Wangwe
 
Mkuu Msuya si tu alihusika na kifo cha Sokoine bali alihusika na Kuchoma BOT kwa maslahi yake binafsi ... Mwanga Development Bank inamhusu pia...

Msuya kayataka haya....yeye na Kawawa ndio prime Suspects though ni wazi Kawawa hakuhusika...Msuya ndie aliyeliliwa na wengi na hata hayo mauzauza kipindi kile yalimhusu yeye...Mzee Rashid aliingizwa na wahuni ili Cleopa apone.

Mwalimu ali handle hii issue vyema otherwise Msuya asingelipona toka usoni machoni pa watu
 
Yapo hv : Deus Mallya Rafiki mkubwa wa Mnyika alipandikizwa kwa Chacha kwa Gia kuwa atakuwa akimpa Siri juu ya nini kilikuwa kinaendelea Upande wa pili, kipindi Hicho chacha alikuwa kasimamishwa Kazi, Deus malya akatengeneza mazoea ya kasi kwa chacha akawa anampelekea Habari za kizushi akizuga kuwa kawasikia cc wakimteta chacha nk ndipo chacha akaanza kumwamini Deus: SIKU YA TUKIO chacha akiwa Bungeni aliomba maji ya kunywa ameze dawa, lakini Mrema wa CDM alimpatia maji yenye dawa ya Usingizi akaanza kujisikia vibaya akaamua kuludi nyumbani haraka, akiwa nyumbani Deus akaenda kumgongea wasafiri kwenda Dsm kwenye msiba wa Bhoke Mnanka, chacha akamwambia Deus waahirishe Safari mama anajisikia vibaya,Deus akawa King'ang'anizi alienda kumgongea mara 3 hadi akaamka ili wasafiri, wakati huo Deus alikuwa kaikorokochoa Gari kiaina huku akiwasilana na Wauaji wawili ambao mmoja ni mbunge wa huko kasikazini na mwingine yupo makao makuu Kinondoni. Safari ikaanza huku Chacha akiwa anasinzia sinzia walipofika eneo la Tukio chacha akawa bado yupo macho ikabidi Deus Mallya azuge kuwa Gari ni Mbovu ili wapate sababu ya kuludi Dodoma angalau wakiludi eneo la Tukio kuwe kuna Giza ,wakaludi Dodoma walipofika Deus akazikaza zile Nati ambazo alizilegeza awali na Safari ikaanza tena hatamae wakafika eneo la Tukio Giza likiwa limeingia ,Wakati Huo chacha alikuwa kasinzia Deus akasimamisha Gari wakapanda watu wawili wote wanatoka kasikazini mmoja ni mbunge na mwingine yupo makao makuu, baada ya kupanda Gari wakaenda kuegesha Gari walipopaandaa wakampiga Risasi Mdomoni kisha Kijiko (Greda) kikaibonda Gari kwa juu na kuibinua na kutokomea huku wale watu wawili nao wakipanda Gari na kuishia wakimwacha Deus Mallya akizuga na kuwahadaa Watanzania kuwa ni Ajali, wanakijiji wa pale na Polisi walijua Mchezo wote lakini Rushwa ni Adui wa haki kwa leo tuishie hapa siku ingine nitakujuza zaidi.

Watu mnajua kutunga .......... kama kuna watu wanaamini hii story basi Tanzania hatuna vyombo vya usalama na CCM inabidi wakubali wameshindwa kuongoza nchi.
 
Msuya kipindi hicho alikua nani katika nchi hii? Je alikua na majeshi yote(JWTZ,Police,Usalama wa Taifa) ya nchi hii yalikua yanaripoti kwa Msuya? Kama mtu anaweza kupanga njama za kumua waziri mkuu na akafanikiwa bila kuchukuliwa hatua yeyote basi hicho kitendo kina baraka za amiri jeshi mkuu.

You said it all ........ kama Hayo ya Sokoine na Wangwe ni kweli, basi serikali imeshindwa kazi au serikali ndiyo imehusika. Period!!
 
Watu mnajua kutunga .......... kama kuna watu wanaamini hii story basi Tanzania hatuna vyombo vya usalama na CCM inabidi wakubali wameshindwa kuongoza nchi.

Hii story si ya kutunga ni wewe pekee aambaye ulikuwa Haujui, Vyombo vyote wanajua lakini Tambua Rushwa ni Adui wa haki, Rafu zilianza kuchezwa kule kule kwenye Ajali kisha zikaendelea hadi kwenye ile Tume ya Uchunguzi, wauaji walijipanga mapema wakajua namna ya kuzima kila fununu hasa ukizingatia kipindi kile IGP alikuwa ni Mtu wa kasikazini na watuhumiwa ni Watu wa huko huko.
 
Nilishiriki katika "Mazishi" ya Ndugu Sokoine Jumapili tarehe 15.4.1984, pale nilipokuwa miongoni mwa mamia ya wananchi tuliojipanga barabarani kuuaga mwili wake ulipopitishwa hapa Kikatiti (Arusha), ukitokea KIA kuelekea Monduli Juu. Nilikuwa mwanafunzi wa madarasa ya juu ya shule ya Msingi.
 
You said it all ........ kama Hayo ya Sokoine na Wangwe ni kweli, basi serikali imeshindwa kazi au serikali ndiyo imehusika. Period!!

Kwa Upande wa Sokoine Msuya na watu wake walicheza muvi lakini wao pia ni wa kasikazini kwa maana Kombe na yeye Msuya japo kidogo walimix makabila wengine, Na kwa Upande wa Chacha wangwe Muvi lilichezwa na Kabla moja tena Ukoo mmoja tu, yaani Mbowe,Mnyika, Lema, Kileo, Mrema na Deus Mallya, wengine hawakushirikishwa.
 
Nilishiriki katika "Mazishi" ya Ndugu Sokoine Jumapili tarehe 15.4.1984, pale nilipokuwa miongoni mwa mamia ya wananchi tuliojipanga barabarani kuuaga mwili wake ulipopitishwa hapa Kikatiti (Arusha), ukitokea KIA kuelekea Monduli Juu. Nilikuwa mwanafunzi wa madarasa ya juu ya shule ya Msingi.

Sasa ndipo uzinduke ujue kuwa Msuya kumbe aliyaingilia Mapenzi ya Mungu kwa kumrejesha Sokoine kwenye shimo la futi sita kisa Uhujumu Uchumi wake uliingiliwa na Sokoine . R. I .P Chacha Wangwe na Sokoine.
 
Habari za kifo cha Ndugu Edward Moringe Sokoine zilikwisha andikwa (documented). Sababu za kifo hicho zielezwa. Kama kuna jina la mtu lililotajwa kuhusishwa na kifo hicho basi ni dereva wa gari landcruiser Dumisan Dube Mwanachama wa chama ANC cha AFRIKA KUSINI. David Cleopa Msuya hajatajwa popote. Tangazo la kifo cha Sokoine lilitolewa na serikali,chombo chenye mamlaka ya kutoa tamko. Serikali yoyote makini inatoa tamko baada kujiridhisha na kile inachokisema. Anayesema Cleopa Msuya alihusika kumuua Sokoine kwanza hana mamlaka ya kuyasema anayoyasema. Pili Msuya siyo msemaji wa serikali iliyokuwa madarakani wakati ule. Hata kama anajua chochote kuhusu kifo hicho atasema kama nani?
Lowasa tunamfahamu,ni kijana wetu, hana jipya kwa sasa. Mbinu zake za kuwabambikizia tuhuma wapinzani wake kisiasa haanzi sasa. Mwaka 2005 wakati wa kinyang'anyiro cha kumpata mgombea wa uraisi kwa tiketi ya CCM alikuwa kwenye mtandao wa JK. Alimzushia Salim Ahamed Salimu tuhuma nyingi ikiwemo kumuua Rais Shek Abed Karume na kuwa na ndugu zake Omani ambao wana vyeo vya juu katika jeshi la Oman. Alizusha tuhuma kuwa Waziri Mkuu Frederick Sumaye amefisadi pesa, Prof. Mark Mwandosya amekula rushwa toka kampuni moja ya simu ya Afrika kusini kwa njia ya kumfadhiri binti yake Sekela, aliendelea kuzusha tuhuma kwa Samweli Malecela kuwa amefadhiliwa na waarabu katika harakati zake za kutaka urais. Akaongeza kusema mzee Malecela amebadili dini yake na kuwa mwisilam. Alikuwa hasemi hadharani, mtandao wao kupitia magzeti mbalimbali ulitumika kusambaza uwogo huu. Sasa hivi watanzania wanamjua Lowasa na siasa zake za maji taka.Nadhani kijana huyu ashauriwe kama anautaka uraisi sawa, lakini atafute mbinu nyingine hii imechacha
Mtengeti, usimkaripie. Historia hairekebishwi lakini hufundisha. Lakini pia usiwe na uhakika sana kwamba serikali mpya ijayo haitafuatilia yaliyopita hasa yenye maslahi ya taifa kama mikataba fake, ufisadi na wizi wa raslimali za taifa. Hawa tunawafahamu na tutadeal nao. Wote waliokwapua mali zetu kwa njia yoyote, zikaachwa nchini ama kupelekwa nje, tutazifuatilia. Wengine watakuwa marehemu, tutashughulika na warithi wao lengo raslimali za taifa zirudi, zifanye maendeleo ya nchi, lakini pia liwe somo kwa wanaodondosha mate wakitamani fursa za kufanya uhuni kama ule.

Kwa habari ya kifo cha Sokoine, Bwana Msuya na Kawawa ambaye ni marehemu kwa sasa, wlaikuwa kwenye system. Sidhani kama mtu akiwauliza uelewa wao juu ya jambo hilo la kifo cha Sokoine, kunakuwa na jinai yoyote.
Yeye ajibu tu anachokielewa, historia iandikwe vizuri au iwe updated. Pale atakwama, atasaidiwa.

Kwani yule mganga aliyekuwa anawaosha madawa usiku kwenye mavyungu pale kwa Msuya, ambayo yanasemekana yalimaanisha kuondoa maruwe ruwe aliyokuwa yakiwatokea baada ya kifo hicho alikufa? Kama hayupo bila shaka watoto wake bado wapo, wanaweza kusaidia pia katika uandishi wa historia hii katika kipindi hiki cha maendeleo ya sayansi.

Hallucinations zinaweza kuwa zilikuwa zikiwapata kwa labda walimpenda sana Marehemu na kuguswa sana na kifo chake kuliko wenzao. Na ukaribu huo ndio unaotamanisha watu wasikie lolote juu ya kifo hicho kutoka kwao.
 
Stata Mzuka acha hadithi za paukwa pakawa. Dumisani Dube alipomaliza kifungo aliihojiwa na Daily News ilimnukuu akijitetea kuwa Dereva wa Sokoine alimpelekea ile Benzi ili aigonge. In short Dereva wa Sokoine alilazimisha ile ajali. Wiki hiyo hiyo Dumisani Dube alipewa Persona Non Grata (PI) na kurudshwa SA. Ukweli anao Prof Shaba kuwa Sokoine aliuliwa na Bodygaurd wake kwa risasi kisha wakaframe ile ajali. Imrani Kombe (RIP) alimbadilishia Sokoine mlinzi baada ya kikao kuisha Dodoma. Msuya; Kawawa; Alifred Tandau (RIP)pamoja na Kombe ndiyo wahusika wa kifo cha Sokoine. Kombe naye alipigwa risasi mbele ya mkewe eti polisi wakidai walimfananisha na mwizi wa magari "Mr. White". Mwosha huoshwa. Cleopa David Msuya wenzako wameshatangulia kwenye kiti cha HUKUMU hebu jitetee hapa jamvini.

Prof Shaba ndie alifanya postmortem.....atueleze
 
Kwa Upande wa Sokoine Msuya na watu wake walicheza muvi lakini wao pia ni wa kasikazini kwa maana Kombe na yeye Msuya japo kidogo walimix makabila wengine, Na kwa Upande wa Chacha wangwe Muvi lilichezwa na Kabla moja tena Ukoo mmoja tu, yaani Mbowe,Mnyika, Lema, Kileo, Mrema na Deus Mallya, wengine hawakushirikishwa.

ukabila shida sana unaondoa akili unawaza ukabila tu utakusaidia nin angalien sana ccm mana ndio mtaji mliobaki nao
 
ukabila shida sana unaondoa akili unawaza ukabila tu utakusaidia nin angalien sana ccm mana ndio mtaji mliobaki nao

Hapa sijawaza Ukabila nimeongea hali Harisi ww mwenyewe pima kifo cha Sokoine Msuya na kifo cha chacha ni mbowe wanatoka wapi? Wote si wa kasikazini?
 
Stata Mzuka acha hadithi za paukwa pakawa. Dumisani Dube alipomaliza kifungo aliihojiwa na Daily News ilimnukuu akijitetea kuwa Dereva wa Sokoine alimpelekea ile Benzi ili aigonge. In short Dereva wa Sokoine alilazimisha ile ajali. Wiki hiyo hiyo Dumisani Dube alipewa Persona Non Grata (PI) na kurudshwa SA. Ukweli anao Prof Shaba kuwa Sokoine aliuliwa na Bodygaurd wake kwa risasi kisha wakaframe ile ajali. Imrani Kombe (RIP) alimbadilishia Sokoine mlinzi baada ya kikao kuisha Dodoma. Msuya; Kawawa; Alifred Tandau (RIP)pamoja na Kombe ndiyo wahusika wa kifo cha Sokoine. Kombe naye alipigwa risasi mbele ya mkewe eti polisi wakidai walimfananisha na mwizi wa magari "Mr. White". Mwosha huoshwa. Cleopa David Msuya wenzako wameshatangulia kwenye kiti cha HUKUMU hebu jitetee hapa jamvini.

umeweka record sahihi kabisa huu ndio ukweli ninaoufahamu
 
Back
Top Bottom