Msukuma: Serikali ihalalishe Bangi na Mirungi

Msukuma: Serikali ihalalishe Bangi na Mirungi

Ila bange baba ni hatari.Niliwahi fuata reli kwa miguu kutoka shaurimoyo kwataz za reli miaka hiyo kama mnakumbuka hadi pugu.Bahati sikukutana na treni ya kati ningekoma.Sijui tungepishanaje maana mimi mwenyewe nilikuwa kama gusi.Ila nilipata fahamu baada ya mlipuko kuisha.Yani toka siku hiyo nilisalimu amri maana ujana ulitaka kuniviruga.Ninamsihi ndugu yangu msukuma atafakari kwa kina.
Umeanza kuharibu, KAA KIMYA

Legalize it
 
Nani anamfaham snoopy Dogg doggy huyu ni mwanamziki mkongwe mwenye umri wa baba yangu Na ni bilionea ila Na mvutaji wa bhangi zaidi ya miaka thelathin anavuta JE amewah kuwa chizi Na alivunja record ya dunia baada ya kuwa binadam wa kwanza kuandika kitabu kilichokuwa rizla kwa maana ya karatasi special za kuvutia bhang ye aliandikia kitabu opium haina madhara ni God made
 
Mmmmh!ikihalalishwa nakunya kuanzia ubungo hadi mwanza nyegezi stend.
 
Nyie watu Elimu Elimu Elimu
Mnashinda hapa JF wale wenye Elimu ya hapa na pale wanatutungia sheria za Inchi.
Mtasema sanaaaaa mwisho mtalala tu
 
hahaha bila hata kuuliza majibu yapo wazi kabisa.... kwa kuokoa maisha ya wengi na taifa kwa ujumla isingefaa hii kitu halalishwe kwa sababu ni haramu.
Uharamu wake ni upi mkuu? Pombe na sigara lini viliwahi kuwa halali?
marijuana inaweza kutumika kwa manufaa mbalimbali ikiwemo kutibu magonjwa mbalimbali. Ifanywe uchunguzi kwanza na itumike kwa manufaa zaidi si lazima wahalalishe uvutaji
 
Duh!yaani mmea uruhusiwe!sipati picha yaani itakuwa harufu yake kama harufu ya pilau siku ya eid mubarak au Christmas mitaani itakuwa kunyonga na kuwasha.
 
Katika kile kinachoonekana kukurupuka na kutojielewa leo mbunge musukuma kasheku ameomba serikali ihalalishe matumizi ya bangi ili iweze kuongeza pato la serikali. Hii inaonesha ni aina gani ya wabunge tulionao katika awamu hii. Naomba serikali ipige marufuku wabunge wa namna hii.
Nadhani Serikali iangalie ubaya Na faida wa hiyo Bangi, ili ifanye maamuzi...
 
marijuana inaweza kutumika kwa manufaa mbalimbali ikiwemo kutibu magonjwa mbalimbali.

mkuu nadhani muheshimiwa mbunge ali hitaji ihalalishwe kwa ajili ya ku smock tu.maana nahisi atakuwa anajificha ficha,,..lakin kama kwa ajili ya manufaa hayo ya kiutabibu naunga mkono hoja.
 
Therapeutic value ya mirungi na bangi ipoje dhid ya pombe. Infact ni kwamba pombe ni dawa 'drug' kuliko bangi na mirungi
Mirungi ni kosa kuingiza kwenye kundi la drugs, ninawajua watu ambao wamekuwa wanakuja mirungi kila siku kwa zaidi ya miaka Arubaini na hawana matatizo yoyote na ni wenye heshima zao. Sijasikia mla mirungi kafanya fujo, na panapoliwa mirungi hapana fujo wala kelele, utakuta watu wameka kistaarabu na mazungumzo yasimfikie maana kabisa.

Wakati wa mtihani wangu wa form 4, tulikuwa tuna kula mirungi zarba kama mbili hivi na tulikuwa tunakesha kusoma, we did very well we were a group of 4 na tulipasi vizuri sana.

Kule same kuna vijiji vilikuwa hoi kiuchumi na hali ilipanda sana kimaisha, walipogundua mimea ya mirungi porini, watu wameweza kujenga nyumba za hadhi na visima vya maji , hata wameweza kupeleka watoto wao mashuleni.
 
Inaonekana tukipewa nafasi ya kupiga kura kama Bangi na Mirungi ihalalishwe au la, basi kura za NDIYO TUHALALISHE zitakuwa mingi sana... Tutasmoke pale academic bridge (udsm) afu tunaenda discussion m-degree..
 
Naunga mkono hoja, pato la taifa litaongezeka kwa kupitia zao hili la muhimu na lenye faida katika mwili wa binadamu

Na idadi ya watalii itaongezeka maradufu,hawa watatoka si tu Ulaya na Marekani bali nchi zinazotuzunguka pia.

Mtu anavuka boda anavuta mmea bila bugdha akitosheka anavuka boda tena kurudi kwao.
 
Huyo mbunge anatsfasili mambo kinyume anadhani mjengoni wsnaingia wenye elim ya upe kama yy, fikilia dunia inahangaika kutolomeza madawa yakulevya kwasababu yanaangaminza nguvu kz,yeye mwenye elimu ya upe asiejua tofauti ya mgongona tumbo anasema vihalalishwe ilitaifa lipate mapato kutokana na mauzo ya bangi na milungi, nadhani alisema hayo kwa sababu yy nimkulima mkubwa wamazao hayo
We una elimu gani mkuu hadi uibeze ya Msukuma?
Kuandika tu kiswahili kwako tatizo!
 
Na idadi ya watalii itaongezeka maradufu,hawa watatoka si tu Ulaya na Marekani bali nchi zinazotuzunguka pia.

Mtu anavuka boda anavuta mmea bila bugdha akitosheka anavuka boda tena kurudi kwao.
Jamaica imepata popularity kubwa sana among American superstars kwa ajili ya mmea tu ...
Jigga anasema "am I fly to Kingston, just to roll some reefer"
 
kumekua na mijadala mirefu saana mitaaan inayohusu swala zima la matumizi ya bangi baada tu ya mbunge wa geita kuiweka hoja mezan ndan ya bunge.

imeleta taswila tofauti kulingana na mapokeo yake haswa ikionekana kupewa nguvu haswa na watumiaji na kupingwa nawasio watumiaji kutokana na hoja isemayo hakuna kitu kisichokua na faida na hasara

wengi wetu tumekua tunaipinga bangi lakin nimepata baati yakukaa na watumiaj kujua kwann wanaunga mkonyo hoja na kupata sababu moja tu ilio kuu kwa upande wangu wakidai kua kumekua namatumiz mengine ya vileo nchin inavyoruhusiwa licha ya kua pia na hathar kubwa pengine zaid kuzidi bangi kwa mfano sigara na pombe sasa iweje bangi tu ndo izuiliwe!!?

swali lao nilijitaid kwa uelewa mdogo nilio kuanao juu ya athar za bangi kulijibu lakin kiukwel nilielemewa na uzito mzito wa hoja zao ikabid niseme tu BANGI NOMA!!!

sikukata tamaaa ndo sababu kubwa leo nauliza kwann tuzuie bangi na kwann tupitishe bangi!!? unalichukuliaje swala hili!!?
 
Hata nchi za magharibi walianza na mijadala kama hii;mara bangi ihalalishwe,mara utoaji mimba uhalalishwe,hivo watanzania tusishangae iko siku kuna watu watataka na USHOGA uhalalishwe.BEWARE.
 
Back
Top Bottom