Kumbukeni kuwa zawadi pekee unayoweza kumpa mtoto wako ni kumpenda baba/mama yake. Kwa hiyo kama umezaa na mtu mvumilie tu kwa yote kwa kuwa mtoto wenu akikugundua kuwa unamchukia baba/mama yake jua fika hata umgharimie kiasi gani na yeye atakuchukia tu. Mimi baba na mama waliachana nikiwa form one. Baba ni chanzo cha ndoa kuvunjika lakini nashukuru Mungu mama always anatusisitiza tuwe tunamsalimia baba yetu and there is no msukule between them kwani wote sasa ni above 60 and my mum hakuolewa tena wala hakufuatilia maisha ya baba baada ya kuachana. Baba pia siku zote anaongea positive things about our mum. Nina hakika wangewekeana ligi za kuchafuana kwetu mmoja wao au wote wangekosa upendo wetu.
Nadhani hii ndiyo inafanya watu waseme watu waliokwisha zaa pamoja hawahachani. Tumeshaona wengi wanarudiana even after 10 years.
Hongera mbu kwa mada tatanishi sana...maty jaribu kuyaangalia maisha ya simba mnyama...wewe kama mwanamke ni lazima utampigania mwanao...na huyo mumeo yeye anaangalia kukumiliki 100% ikiwemo kuwa na kizazi naye na kwa taarifa huyo mwanao sio ishu kwake kabisaaa...na kuendelea kumuendekeza huyo ex kisa mtoto ni kujitafutia jambo jingine..hapa kuna utata wa kimaumbile. Hata maandiko yanasema Yusuph baada ya kujua Marimu yu mjamzito akapanga kwa siri 'kumuacha'mpaka alipopigwa mkwara mzito (alitengenezwa kiroho)Asante nyumba kubwa kwa mfano mzuri na amini utatusaidia si wengine katika malezi ya watoto wetu. Mimi nilikua nafikiri tu kuwa tukianzisha ligi mi na huyu mwenzangu inaweza kumuathiri mtoto na baadae akatuona hatufai ikumbukwe nilikua nafikiri tu kwani mimi nimelelewa na baba yangu na mama yangu na mpaka sasa wanazeeka pamoja. Kumbe mawazo yangu ni sahihi thanks a lot nyumba kubwa na kwa kweli niko tayari kufanya lolote liwezekanalo kumfanya binti yangu awe na amani na sio kuanza kuwaza kujifurahisha mimi na utu uzima huu lol.
Ukiona ex wako anakuendesha na bado unaingia line ujue bado kuna ka feeling fulani unacho juu yake,kuhusu kuzaa nafikiri ukiwa umefanya yanayohusu mtoto ipasavyo na kuhakikisha unamwona mara kwa mara mwanao haezi kukuita ovyo usiku wa manane coz utakuwa labda umemuona mtoto mchana na kujua afya yake,so akikuita usiku utamjibu mkato tu,tutaonana kesho,kuna wanaume wengine huwa hawna msimamo kabisa ukiwa na msimamo from begining sidhani kkama atathubutu kukuyumbisha
Doh! Mbu maumivu yake tusome kwenye maandishi..........hapo sasa kupenda tusipopendwa kabla ya kugundua tulishapenda .........huwa tunahitaji kufanya nini kabla ya kupenda?maana wengine mioyo yetu ina viherehere sana.
Inawezekana kujali hisia za mtu usiyempenda?Najaribu kufikiria mengi Mbu usichoke maswali yangu.
Have her out with another brother in the bar. My son with another man in the car. Girl you ain't gonna play me like that.
I'm just not gonna be tolerating this and paying that. See I pay the bills, I pay the phone.
If I catch you here again, hommie we gonna have a problem. Let it be known, I might not stay here but this is my home.
Leave it alone, cause this child is my baby. No ifs, ands, buts or maybes.
I don't wanna be with her, but I just can't stand to see her with nobody else. I know it's bad but I can't help myself.
See, I'll be damned if I let my son call another man daddy. And if u feel like I feel, that's baby mama love.
NB: My rendition by courtesy of N2U.
AshaDii.. I have no idea kwanini niko sceptical na hii issue nzima ya mapenzi ambayo inasumbua vichwa wa watu. Na sielewi kwanini despite the fact that sifanyi vile wengi wanafanya ku-prove wanajua kupendana mimi, mwenza na familia yangu tunaaminiana kiasi cha kutosha kusolve bump ndogo ndogo na ku-excel smoothly na life..labda hii ndiyo inanipa kichwa kuwa hakuna mapenzi ila kuna maisha.. Ni vile wewe unaamua kuishi na ku-balance equation yako na mwenza + family. Na ukiweza hili uta-feel uchungu wa wenzako kama wa kwako..
Anyway..back to the sired.. Naamini issue na impact za msukule wa mapenzi zote ziko ndani ya uwezo wetu hadi pale tunapoziachia na kuwa juu ya uwezo wetu..ikifika wakati huu..yaani ni vigumu kuzi-control..hasa zikihusu wale malaika yaani watoto..au wazazi..
Tulizo ndugu yangu, hongera sana yaani natamani kweli ningeweza nami kuishi 'kikavu' kama uishivyo wewe!!
unajua suala zima la maumivu linatokana na hisia ambazo zamani kidogo hazikuwa na umuhimu mkubwa kihiiivyo katika mapenzi (nadhani ndo maana ilikuwa pia rahic kuoa/lewa na mtu uliyechaguliwa na wazazi)
Unfortunately kizazi chetu hiki tumejichakachusha kwa mapenzi ya kizungu ambayo yanaweka hisia mbele zaidi kuliko hali halic............ukitendewa jambo kidogo tu la kimaisha.... unalitafcri kihisia, kwa nini, why me, kwa nini anifanyie hivi, atakuwa hanipendi, eh atakuwa keshapata mwingine ili muradi tabu tupu...........Naomba shule wajameni
... unajua suala zima la maumivu linatokana na hisia ..... Unfortunately kizazi chetu hiki tumejichakachusha kwa mapenzi ya kizungu ambayo yanaweka hisia mbele zaidi kuliko hali halic............ukitendewa jambo kidogo tu la kimaisha.... unalitafcri kihisia, kwa nini, why me, kwa nini anifanyie hivi, atakuwa hanipendi, eh atakuwa keshapata mwingine ili muradi tabu tupu...........
...mmnnh? kwanini umetamani hilo?
...mnnhh? hisia za zamani zinatofauti gani na za sasa?
Mwj1, hali halisi ndio ikoje hiyo yarabi compared na mapenzi ya hisia?...
MJ1, Nakubaliana nawe kuwa moja ya chanzo cha misuguano ndani ya mahusiano ni jinsi gani tunavyoshindwa kudhibiti hisia zetu.
Kwa mtazamo wangu hapa kunaingia vitu vingi..Trust, kiasi gani nimemwamini mweza; sacrifice - kiasi gani nimejitoa muhanga yaani si kila siku mtu mmoja tu apate ushindi wa hoja ndani ya nyumba..lazima ushindi uwe wa kupokezana .leo mimi..na kesho yeye.labda tu kama hoja ni ya nguvu..hivyo basi hapo utaona kuna aina fulani ya kubali yashinde au kwa upande mwingine unakuwa msukule wa kujitakia ..ili kuleta usawa, kuaminiana na kupunguza hisia kali kwenye mahusiano.
Lakini ..Je? utandawazi unachangia kushuka thamani..kwa Sacrifice, Uaminifu, Heshima, Busara, Nidhamu etc.. Inawezekana ni kweli..Wazazi wetu wamezaliwa na kukua katika mila na tamaduni nyingine..wakatufundisha wanavyojua wao.. lakini sisi watoto wa dot com tukaacha tamaduni zetu na tunajaribu ku-experiment mseto wa tamaduni za utandawazi na za kiafrika yaani kinachotoka hapo ni chotara...na kusaga meno..
Jamani mimi sijaelewa,
Hivi ex-BFs/GFs ni mashirika ya kutoa misaada kwamba ndo yawe kimbilio mtu anapokuwa na matatizo yake? Sihitaji kuwa karibu naye wala kujua matatizo yake ya kila siku. Kuendekeza huruma ndo mwisho wake unapoteza vyote..Anakuharibia ndoa na kuanza kukucheka!
Watu wa namna hiyo wana nia mbaya sana..ni devils!!
Samahani wadau wa huu mjadala,
Naona nimekwama kabisa. Kila ninachosoma hakieleweki...Naogopa kunyonyoa hizi mvi zangu na kubaki na kipara (ukizingatia huku karibu na DRC kipara ni deal la nguvu)!
Kuna jamaa alinambia kuwa hii dhambi inayohusisha kugandishana kwa miili ni mbaya sana, kwani haifutiki milele! Ni zaidi ya kupigwa ndonya usoni!!
Halafu inakuwa mbaya endapo dhambi hiyo inaenda hatua moja mbele kuleta matunda ya uumbaji!
Kama Ex-BFs/Gfs hawachani milele, iweje wakiwa na mtoto....Hili naomba nijitoe katika mjadala wake!
Sorry i can never seem to narrow things down.... hasa kama imenigusa/inanihusu.... thus the long post....
Mbu Mapenzi kitu cha ajabu saana na kweli kabisa hayana adabu . For ukiwa in love, yenyewe pamoja na huyo abuser (who in most cases anakua hana mapenzi ya kweli) ndio yanakuendesha Kwa kuzingatia hio term ya Emotional Rollercoaster Ubaya ni kwamba kama mhusika bado una feelings za Ex wako hata apewe ushauri gani atakubali NDIO but yet still itapofika Yule ex akajitokeza na kumsumbua ana rudi hali ile ile ya unyonge na kubulutwaa hio tokana na ukweli kwamba hawezi control hizo feelings . Uzuri tu ni kwamba hata abuluzwe namna gani iko siku yeye mwenyewe mhusika atatia akili (time hu vary ) kua sasa basin a hatavumilia upuuzi wowote toka kwa huyo ex.
From experience Kwa wanao nifahamu kwa ukaribu hapo nyuma I was a Great example wa Msukule wa Mapenzi . Usiombe Nilikua naambiwa but yakawa yanaingilia sikio moja na kutokea linguine But nilikuja vumbua mwenyewe!!! Huyo ex nimezaa nae but imepita hata three years toka tuliwasiliana/onana mpaka tu juzi kati kwenye matatizo ya misiba....
Mzee wangu DC, with all due respect I beg to meander hapo kwenye red.........not to differ with you because to some it is and will remain true but I would like to meander kwa upande wangu. It only depend with sababu zilizowaachanisha na status mliyopo kwa sasa. Kama mliachana bila mapenzi yenu i.e. wazazi hawakupenda, au mitazamo tu ya maisha ikawafanya muachane ilihali bado mwapendana inawezekana kweli msiachane! But also inategemea na status yenu kwa sasa....kama mliachana mkingali mnapendana halafu kila mtu akamove na mahusiano mengine to some extent inakuwa ngumu kidogo (sisemi haiwezekani) kurudia kuwa na mahusiano.
But Babu mmeachana baada ya kuumizana kwa maana halisi ya kuumizana hisia kiasi kwamba mioyo imejaa kutu halafu kila mmoja akawa na mahusiano mengine nadhani itakuwa ngumu kurudisha hisia! Ni mtazamo wangu tu inawezekana kabisa isiwe sawa.
Darling, ndio najaribu kuomba msaada wa somo hapo! Maana kwangu mie (tofauti na Tulizo) siwezitenganisha mapenzi na hisia.......kwa sababu alivyoeleza kuwa tofauti na wale ambao wanajifanya wanajua kupenda (nimetafsiri kuwa ku'hangaika' kuonyesha unampenda mtu lazima kuendane na hisia........nitakukiss Mbu kwa kuwa ninahisia za kukupenda, nitaku-hug kwa kuwa ninahisia za kukupenda vivyo hivyo nitakuprotect na 'maumivu' ya moyo na nafsi kwa kuwa nahisi ninakupenda- Hii ni tafsiri yangu ya kuexpress love. Kwangu mie LOVE=Feelings ambazo zinadirect matendo yangu kwako.
Hazina tofauti Mbu nilichomaanisha ni kuwa watu wa zamani hawakuwa wana'zisikiliza sana' hisia zao au hawakuwa wana'zitii' sana hisia zao za kimapenzi. Yaani ku'itikia' hisia kipindi hicho kulikuwa si kwa sana kama leo hii na ndio maana kulikuwa na 'tolerance' ya namna flani hivi kwamba baadhi ya makosa ya ndani ya ndoa (kimapenzi) yalichukuliwa ni madogo na yalitatuliwa kirahisi zaidi si kama siku hizi ambapo mtu akinyimwa unyumba siku moja tu kwa kuwa mwenzi anaumwa basi anatafsiri ana mwingine/ amegawa kwa houseboy/girl/bosi au secretary n.k. ni hisia ambazo zinajijenga kwenye imani na mwisho matendo ya revenge n.k.
Mbu mbona umeichambua sana hii post jamani?.........hali halisi mie ninadhani ni kujaribu kulink hisia na maisha halisi. Hii ninafikiri mie haiko sana kwa wenzetu wazungu ambao wao wana tendency ya Ku-dilink/kutenganisha hisia na maisha (kama kuna tafsiri yake!) ambapo kwao hisia zina nafasi kubwa zaidi na wanazitii sana sometimes unnecessarily... (mfano umekaa na mtu kwa miaka miwili---ndoa halali-- ghafla unaamka hujisikii kumpenda tena--- unafile divorce!!!) . So ninachomaanisha hapo Mbu ni kuwa hata ikitokea siku nimekujibu vibaya basi usikimbilie kuumia hisia zako kuwa mapenzi yamekwisha siku hizi! Au siku nikikwambia I need time alone (nendalala chumba cha wageni LOL) unielewe na sababu nitakayokupa uielewe usikimbilie kuconclude kuwa mapenzi yamepungua au siku hiyo nitakuwa nimepata 'dozi' kubwa kutoka kwa 'mwizi' wako!
Leo nimelichokoza .................Jamani mada ni Msukule wa Mapenzi na si nyingineyo.
Mbu na wale ambao walionja wakanogewa, wakaamua kubinafsisha then wakakinai wakakitelekeza lakini bado wanakushkilia kiaina (hizo emotional chains) huku wakikupa zile za ..............au .......Mie najua kuoa tu, sijui kuacha au Niliapa for Better, for worse on my wedding day so I wont give you a divorce??
.....Nafikiri tuko katika jahazi moja Tulizo ni sawa kabisa na niaminivyo mie. Mambo ya utandawazi na package yake yote ndio chanzo cha misuguano katika ndoa nyingi..... ingawa si kwa mabaya tu but hata kule kumfunua mtu juu ya haki zake kimapenzi/ndoa ambavyo kwa namna moja au nyingine kumesababishwa na Utandawazi umechangia sana katika kuvunjika kwa mahusiano mengi hasa ya kindoa. Uvumilivu na ile hali ya 'kuchukuliana' imepungua kwa kiasi kikubwa sana..........Mama yangu mara nyingi husema mahusiano yetu siku hizi ni ya 'ki-Egoli" yaani kama mchezo wa kuigiza hayana uhalisia hata kidogo.,, hayampi mtu mwanya wa kuishi kama yeye, kwa staili aionayo yeye inamfaa kuhakikisha ndoa/mahusiano yake yanadumu! Akikosewa kidogo ataanza kulinganisha na mwenzake na kuangalia mwenzakek alichukua hatua gani, vitabu, theories zinasemaje juu ya kitendo alichotendewa n.k
...nadhani hii pia inatokana na kasi ya maisha,...kwa sasa hatuna muda wa kukaa chini ya mwembe kusubiria dodo lianguke, au alfajr unaamkia chini ya miembe kutafuta yaliyoanguka usiku...Kizazi hiki ni cha kukimbilia Shoprite au Imalaseko kununua Mango juice ya Azam, tamu kuliko tunda lenyewe... yaani tunaishi maisha ya short cuts kibao,...na siku hazigandi vile vile...Tukubali mabadiliko. Zama za kuandikiana barua, niifukizie poda na marashi, kisha niitume kwa posta mpaka ikufikie wakati kuna emails/sms leo hii nitaonekana sijali muda.
Hizi theories, kusoma vitabu, au kubandika post JF upate msaada wa mawazo ni kiashiria kwamba hatuna muda wa kukaa na wazee wetu, mashangazi na wajomba kupata busara zao juu ya maisha kwa ujumla. Kama mnakumbuka ile Topik ya Wheel of Life?, kuna wengi waliipinga kwamba muda hautoshi kabisa. Twendeni na wakati kabla wakati haujatuacha tukabakia tunashangaa...
...Mzee DC bado anashangaa shangaa haya mambo tunayoongelea,....kwani kuzaa na mtu lazima muwe mlipendana nae kiviiile? Vile vile kuna zile One night stands ambazo mw'mke ana conceive kisha anachukulia mtoto kama bakora ya kukuchapia. Mwanaume unaishia kulambishwa kimtego mtego, ....mtoto hupewi, kwa mkeo hajulikani,....uhakika wa mtoto mwenyewe kama ni wako au sio wako hujui...ukijifanya kusahau unakumbushiwa...almuradi unachezeshwa makida-makida tu... mnh, maisha haya, misukule ipo ya aina nyingi!