Smile Digital Stationery
JF-Expert Member
- May 5, 2024
- 202
- 317
Mimi sio mtu wa siasa, sina chama chochote ispokuwa mimi ni mfuatiliaji wa hoja zote, pale napoona anayeongea na kufanya mazuri namfurahia na kumwombea afanye zaidi, na anayefanya mabaya namchukia na kumwombea abadilike awe mwema.
Kwa muda mrefu nimeona na kusoma malumbano ya hoja mbali mbali za wanasiasa, kiukweli mimi yeyote anayeitwa Mwanasiasa simchukulii kama Suluhisho, bali namchukulia kama mtafutaji na kachagua hiyo ndio njia yake ya riziki na haijalishi ni wa chama gani.
Kwa siku za hivi karibuni nimewaona wanasiasa wa Chama cha Chadema wakifarakana na yote hyo ilianzia pale kwenye kubadilisha Kiongozi wao Mkuu (Mwenyekiti) wa chama, kiukweli mimi haya yanayotokea nilishajua kuwa yatatokea, maana ulikuwa ni uchaguzi ambao wagombea walitumia silaha kali za kutoleana na kukosoana bila kuangaliana usoni, kiuhalisia wakati mshindi anapatikana kwa mwenye jicho la saikolojia ya kumsoma mtu, yule kiongozi wa mwanzo baada ya matokeo walikumbatiana ila yule aliyeshindwa hakuwa ni mwenye kukubali 100% na matokeo yake ndio kama haya yanayoonekana, kwamba wale walikuwa wanamsaport kuondoka kwenye chama baada ya Uongozi wa sasa kuja na agenda yao ya "No reform No Election".
Mnadhani kuwa KUBWA LA MAADUI NI NANI?, Unaweza kujiuliza, ni kwanini hawakuondoka awali na badala yake wamesubiri hadi Baadhi ya Viongozi kuwa kwenye matatizo?
Jibu linabaki palepale kwenye mawazo yangu kuwa, "Wanasiasa sio watetezi wetu wenye kutatua changamoto zetu bali ni watafutaji wa riziki". Wale walioondoka wameondoka maana wameona huku hakuna ulaji tena, hawawez kukaa sehemu ambayo haina ulaji, hvyo wameenda wanapokwenda kwa lengo la kuja kugombea na kuja kuwadanganyeni kwenye kampeni muwape ulaji.
Na kubwa zaidi turudi kwa nyie wananchi na wanachama wa chadema, wale watu wanaoondoka kwenye chama miongoni mwao wana majeraha, na historia ya kuteseka wakidai waliteseka kwaajili yenu, (ijapokuwa ni kwaajili yao pia), Ila je, Mliwasaport kwa kiasi gani kipindi walipokuwa wanaumia kwaajili yenu?,
Walipokuwa wanaitisha maandamano ili kuishurutisha Serikali kuwasikiliza na kufanyia kazi malalamiko yao, mlikuwa mnawaonyesha kwenye social medias kuwa mpo nao pamoja, ila siku husika za maandamano MBONA MLIWAACHA WAO WENYEWE WAPIGWE NA KUUMIZWA?.
Namalizia kwa kusema, MSIWADHIHAKI WANAOONDOKA MAANA HAMKUWASAPORT PINDI WALIPOKUWEPO.