Msiwahukumu wa mapenzi ya jinsia moja: Papa Francis

Mimi Nina swali (lengo langu ni kujifunza na kuongeza maarifa tu) Kwanini mahusiano ya kingono ya jinsia moja iwe suala la uhuru na uamuzi wa mtu kujichagulia aina ya maisha yake. Na si hivyo kwa maharimu kushiriki ngono?

Maana hata huo nao ni uhuru wao wa kujichagulia aina yao ya maisha.

Kaka.
 
kusema kuwa binadamu hana uwezo wa kumhukumu mtu sio kweli kwa wale wakatoliki wanafahamu mtu kama ukiwa hutoi zaka,huendi kanisani wala kushiriki katika vigango licha ya kutofanyiwa ibada yeyote ya maziko hutoruhusiwa kuzikwa ktk eneo husika la katoliki hata kama wewe ni mkatoliki je hio sio hukumu
 
160408151500_pope_francis_catholic_304x171_epa_nocredit.jpg

Papa Francis amewataka Wakatoliki Duniani kuwaomba radhi watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kwa madai kuwa si haki kuwahukumu na kuwachukulia kinyume kwani kanisa halina mamlaka ya kuwahukumu.

Akizungumza na waandishi wa habari ndani ya ndege wakati akirejea kutoka Armenia,Papa Francis kanisa pia linapswa kuwaomba makundi mengine ambayo yametengwa kama vile wanawake,masikini na watoto ambao wapo katika ajira hatarishi. Hata hivyo baadhi ya wakatoliki wenye msimamo mkali wamepinga hatua yake ya kuwazungumzia watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
 
wazungu katika harakati za kutaka dunia kukubali ushoga,inasikitisha sana hasa kiongoz kama huyu akiongea maneno kama haya
Hajakwambia ukubali kakwambia usihukumu,

Kuhukumu si kazi yako....hata kiongozi wako wa kiroho humuelewi seuse huyo mungu wenu?
 
Wakati mwingine huwa nawaza hivi papa ile page ya sodoma na gomola iling'olewa kwenye vitabu vitakatifu vya maandiko..???. Au huwa wanarukaga hiYo page.... Na kutetea huo upunga....???
Mnavyojidai kuwatenga mashoga, utadhani ninyi mko safi rohoni. Hebu jichunguze kwa leo tu, tangu umetoka nyumbani hadi sasa hivi, haujamkosea Mungu wako? Na wewe utengwe kwa makosa yako? Kitu gani kinakufanya umuone mwenzako ana dhambi isiyomstahili kusaidiwa kiroho kuliko dhambi zako?
 
Hiyo kauli inademoralize watu kukemea UOVU.
Wametumia hii kauli watu weñgi kutetea wasichokitaka kisemwe.
Bibilia inasema ukimuona mwenzako anapotea na usimwambie damu yake itakuwa juu yako

Kuelewa vizuri biblia inahitaji utulivu wa ndani, ili roho mtatatifu akufunulie . Kemea maovu wakati wote, ila usihukumu mtu kwa uovu wake.
 
niombe msamaha kwa mtafunaji na mtafunwaji nanino ? i say no, no, no .big NO.
 
Kuelewa vizuri biblia inahitaji utulivu wa ndani, ili roho mtatatifu akufunulie . Kemea maovu wakati wote, ila usihukumu mtu kwa uovu wake.
kukuemea uovu lzm uendane na kuchukua hatua. ndio maana yesu aliwafukuza wafanyabiashara kanisani nao wangelilia kuhukumiwa, nehemia aliwafukuza hadi wanawake waliokuja kujiuza na kufanya bisness siku ya kusali aliwakata hadi nywele, yohana alikemea herode uovu wake akakatwa kichwa, paulo alimkemea petro alipoonyesha unafiki kwa wayahudi, man paciao alipigwa ban kuingia supermarket kisa kawasema mashoga. Ulimwengu wa leo case zote hizo hukimbilia kwenye kuhukumu. kanisani ukisema wadada wajisitiri vzr umehukumu, hatupaswi kutoa kauli zenye kuipa unafuu tabia flani ovu kwa namna yoyote ile. tulipofikia ulaya marekani na africa hakuna kiongozi wa dini mwenye ujasiri wa kukumea adharani mwenendo huu. maana dunia itakuona unahukumu,mbaguzi, huna huruma ikiwezekana kutengwa. tunapaswa kuuchukia uovu sio muovu lkn pia tunapaswa kumkemea na kumuonya muovu bila kupepesa macho. hii kazi dunia itakuona mchochezi na unahukumu na kubagua.
Ni mapepo tu yalipokemewa na Yesu yalilalamika kuhukumiwa kabla ya Muda wao
karibu
 
Sisi hatuhukumu bali tunaukemea huo ushenzi! Na yeye kama kiongozi wa kanisa anapaswa kuwa mstari wa mbele kukemea huo ujinga, Biblia iko wazi kabisa kuhusu hayo mambo au yeye ana Biblia yake nyingine? Yeye haitwi Mkristo? Haamini maandiko katika Biblia? Kwa nini asiwe na msimamo unaoeleweka?
 
Kwa hiyo hatupaswi kushangaa maneno ya Papa kwa sababu kwenye jamii kuna watu wanatoka nje ya ndoa, wanasema uongo na washirikina? Dini isikufanye uwe mvivu wa kufikiri, amka!

...unadhani kila mwenye uwezo wa kufikiri huwa anafikiria sahihi?!, amka mwenyewe!
 
Sawa Papa tusihukumu sasa tuwafanyeje?
Mbona km unakitu umekificha hukisemi? Km ni chukizo kwa Mungu kwann tusiwakemee na kuwakataza? Wakristo bhana kwann Biblia haijakemea haya maovu?
 
Hapo ndio utajua kuwa Islam ni dini ya Kweli
Hakuna kuiboresha zambi km imekemewa..
Tatizo wakristo wanatumia sana akili zao kuiongoza Biblia wakat tayar wameikuta imekamilika wanataka kuiongezea vitu kulingana na nafsi zao zinavyotaka
Qur'an haibadillishwi na hakuna kuongeza chochote bcz imekamilika na imetoamuongozo wa jins gan binadamu tuish hakuna kulegeza sheria hata km zinatubana
 
Sawa Papa tusihukumu sasa tuwafanyeje?
Mbona km unakitu umekificha hukisemi? Km ni chukizo kwa Mungu kwann tusiwakemee na kuwakataza? Wakristo bhana kwann Biblia haijakemea haya maovu?
Samahani lakin tangia uzaliwe ni dhambi ngapi umefanya na ulishawahi kuhukumiwa kwa hizo dhambi ulizo fanya? Kama bado kwann unataka kuhukumu mashoga au ww ni mwema sana kuliko wao. Sio kama na tetea ushoga hapana tena siupendi lakin chakufanga ukiona mtu anapotea inabidi umshauri na asipo sikiliza muache lakini sio kuhukumu kana kwamba ww ni bora kuliko yy papa alichosema ni tusiwahukumu sasa unacholalamika ww ni nn. Basi na ww tukuhukumu kwa dhambi unazofanya au unafikiri dhambi zako ni ndogo kuliko zao. Tumia busara kufanya mambo na hekima ina hitajika
 
Kama wazinzi wanatengwa wao kwa nini wasitengwe na kulaaniwa juu.. Nawakemea kwa jina la Yesu na ninawatenga
 
Kanisa haliwezi kukemea ushoga. kwanza wengi wa makasisi ni wale wanaooenda kuwanajisi watoto wadogo.
pili kanisa lenyewe viongozi wake wakuu wanapumuliwa kisogoni mfano Anglikana wamebariki hili.
Bora kaamua kuweka msimamo wa kanisa hadharani.
 
Back
Top Bottom