Msiotumia pombe, mnapotezea wapi muda?

Kama Kijiwe cha JF hakikutoshi basi jitafakari utakuwa na shida sehemu.

70% ya Watanzania ni wachawi tu, ni Bora hata marafiki wa online kuliko hivyo vijiwe vyenu ni wachawi kamili waliokosa vitendea kazi Tu.
Kama unaamini marafiki wa online kuliko mtaani, basi wewe ndie una shida zaidi.
 
Maskani kwa wanangu wauza maduka wana madini sana.
 
kwenye kahawa na kashata
 
Niliishawahi kuleta uzi kuhusu vijiwe vya kahawa kuwa sehemu hatari kukaa eti unajumuika kupoteza muda! Wengi wa magwiji wa pale ni wachawi, waganga, na wasoma nyota! Ukienda pale ukiwa mgeni ujue usiku wanakutumia kujaribisha silaha zao za kichawi! Epuka sana vijiwe vya kahawa
 
Ntarud kujifunza kitu hapa.....
 
Nilikomenti kama utani tu ila hata hivyo mimi nikitafakari kupoteza muda ni kufanya jambo ambalo halina maana. Mfano mtu anasema kufanya mazoezi, kujisoma kama shughuli za kupotezea muda ilhali mimi najua mambo hayo yanapaswa kuwemo kwenye ratiba zako maana ni muhimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…