Msiotumia pombe, mnapotezea wapi muda?

Mkuu haya mambo unayoyafanya sio kupoteza muda
Nimekuelewa mkuu. Hapa key word ni ''kupoteza muda'' au ''killing time'' kama wanavyosema waingereza. Kwangu mimi kupoteza muda ni ku-engage kwenye activities ili muda uende, hasa hasa mtu anapokuwa yupo free na anataka muda uende kwa haraka(kwa sababu kukaa bila ya kufanya kitu mtu anaboreka). Ukichukulia neno ''kupoteza muda'' kama ni kukaa bila kufanya chochote, sidhani kama ni sahihi kwa sababu neno linatumika kama ''idiomatic expression'' yaani maneno yake hayamaanishi tendo linalotendeka. Kwa mfano ''kutafuta kipande cha mkate''. Hii inamaanisha kutafuta kipato na siyo mkate wenyewe.
 
Very nice.
 
Napenda mpira na starehe za kwenye kahawa, idara ya uteuzi zipo wapi
 
Huna kazi yoyote ya kukuingizia kipato?
Binafsi natoka kazini A nahamia kazini B, nikitoka kazini B mpaka nafika nyumbani siku imeisha.
 
Aisee Mimi ni mtu wa tizi
 
Mara nyingi nakuwa na familia,nasaidia kupika,kufua ,kuchek movie,kuchek jf na n.k
 
Kwann upoteze muda mzee, wakati wengine muda tunautafuta. Ingekuwa kuna kuuziana muda, tungekuomba utuuzie wako.
 
well put.
 
Hatupotezi muda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…