Msinunue Namba za magari badala ya Gari lenyewe

Kama unauzoefu wa magari, naona ni bora ukague gari mwenyewe, tena uliendeshe umbali fulani kwenye lami na barabara mbovu...Hawa mafundi wetu hawa..
ukague na wire za plug, usije zimwagia maji
kiujumla magari yanaangaliwa make yake km ni toleo la 2004 hadi 2006 yatafanana kinachobaki ni mileage ikivuka 100.000 kaangalie Body
lkn kusema hili No DZZ limeingia leo Nchini ukaacha No c maumivu utayapata hata ukitest kilomita 10 km mileage ni 200000 jiandae na engine ingene kwani timing gear/belt bearing diff tie-rod vyote vimechoka
 
Wanunuzi Wengine wanaangalia kilometa, wakati kuna waengine wana adjust kilometa za gari inaonekana haijatembea sana kumbe gari imekata kilometa za kutosha
 
Mi nina CH ila mashine imenyooka kama imetoka Japan juzi. Ikiwa kwenye gear husikii kitu yani nisipopiga honi naweza nikakukanyaga hata miguu maana hutajua kuna gari nyuma yako. Body nimeanza kuichakaza mimi hasa bumper tokana na njia mbovu kuelekea kwangu. Inshort Ni gari nimeuziwa na mtu makini sana nikitaka gari ingine namtafuta maana ana gari zaidi ya moja.

Kilichosumbua mwanzo ni battery tu lilikufa nikaweka jipya la Mkorea. Tangu hapo ni mwendo wa kumwaga oil na kubadilisha filter. Zaidi ya hapo ni regular maintanance kama kuweka Hydraulic na Brake Fluid zinapoisha, wiper na matairi.
Mbona tunabambikiwa sana huku mtaani, halafu pia ukizidisha umakini ndiyo unagongwa mule mule, kupata gari nzuri ni bahati, mafundi wengine unamuamini anaikagua gari anakuambia ipo sawa kumbe gari inamshida yake balaa
 
Kupara gari isiosumbua ni bahati tu unaweza agiza gari toka Japan ikaja bongo na ikasumbua wiki kadhaa nyuma nimewahi ona Passo DSE wanaifungua gearbox Reverse inasumbua na juzi hapa nimeona Landcruiser Cynagus DQQ wanaifungua gearbox pia...gari zingine zinazochezewa ni zilizotoka Zanzibar unakuta gari iliingia Zanzibar 2017 inaletwa bongo inapewa usajili DSX, DTG etc kumbe wameshusha KM
Unajua ujanja wa kungalia kilometa kama imeshushwa, kuna watu makini sana wanajua
 
Mbona tunabambikiwa sana huku mtaani, halafu pia ukizidisha umakini ndiyo unagongwa mule mule, kupata gari nzuri ni bahati, mafundi wengine unamuamini anaikagua gari anakuambia ipo sawa kumbe gari inamshida yake balaa
Hahahah gari inabidi uwe na ka uzoefu kidogo na sikio zuri.
 
Ila hizi engine za 2NZ na 1NZ za IST zikikushinda basi wewe muharibifu mana ka hujanunua kimeo IST kusema kweli hazina magonjwa ya ovyo nilichukua IST june 2015 namba DE hadi leo namwaga oil tu kikubwa huwa sizidishi kilomita 3000 zoezi kubwa nililofanya ni kubadili betri tu....

Kamechoka bampa tu sababu ya barabara mbovu ila injini kinanda
Why 3000km, weka oil ya 9000km
 
Why 3000km, weka oil ya 9000km
Duh hiyo Oil kali sijui na Filter yake ipo au utafungua mara 3
recommended 3000km mpaka 4500km ingia service maana kuna vingi vya kucheck, belt, plug, breckfluid. power stearling, pressure etc
lkn km ni la ofisini na sokoni sawa, isiwe la Dar-Bukoba-Bujumbura 1500km sasa go-return trip 6??
 
Engene, gearbox hizo ni spear tu. Anaweza kubadili, tatizo ni alinunua bei gani? Kama ni bei ya chini haina shida.

Mkuu gari yako pia ina dosari sababu km ni chache sana kulinganisha na miaka iliyokaa nchini. Namba c iwe na km 60,000? Unless uliingiza ikiwa 0km.

Watanzania tunapenda sana kuchezea magari. Kama silijui gari na bodi ipo vizuri, ni bora ninunue bei ya kutupa halafu nibadili engine. Lakini kwann ninunue ist m7 namba C wakati nikiagiza tofauti ni mil 3 hadi 4 tu napata.

Mil 4 namba D ya karibu nanunua naweka engine mpya nabadili bush zote na mashock up sitafika hiyo saba na baada ya miaka 4 naiuza hata 4m au 5m.
 
Kutembelea gari yenye namba D, ni fahari ya mtanzania.. Nimeshauza magari kama matano, matatu kati ya hayo nimeuzia mikoani na jingine niliuzia hapa Dar kwa mbinde kwa kuwa lilikuwa na namba C!
 
sometime kinajiongeza speed chenyewe.hapo kama kimefurahi

ndo mana boss kidukulilo anawaambia hvi vi ist, passo, porte, vits sio magar bali n tuvitu twa usafiri. haiwezekan kagar ukiwasha kanapiga chafya kwanza ndo engne inastart. "in kiduku's voice"
 
Ila hizi engine za 2NZ na 1NZ za IST zikikushinda basi wewe muharibifu mana ka hujanunua kimeo IST kusema kweli hazina magonjwa ya ovyo nilichukua IST june 2015 namba DE hadi leo namwaga oil tu kikubwa huwa sizidishi kilomita 3000 zoezi kubwa nililofanya ni kubadili betri tu....

Kamechoka bampa tu sababu ya barabara mbovu ila injini kinanda
sorry hv mwaka 2015 hapa bongo usajili wa magar ulikuwa ushafika namba D?
 
Back
Top Bottom