Msinunue Namba za magari badala ya Gari lenyewe

Alijitibu mwenyewe, 🤣🤣🤣 hilo litakuwa funzo kwake, awache kusikiliza mafundi, ajisikilize mwenyewe
 
Nina kagari Toyota IST ambako kana namba CYZ jamaa mmoja alikuwa anakapenda haka kagari kutokana na condition yake na jamaa ni mbahili pia.binafsi nlikanunua sababu ya mamsap awe anaendea salon na sokoni.baadaye akaja akawa anataka Crown "Toyota" so haka kakabaki hakana kazi.

Kiukweli gari ipo vizuri imetembea kms 60000 plus.jamaa akaja nikamwonesha gari akakagua na kumtafuta fundi wake mtalaam. Fundi akanishtua chamber kuwa yeye ntampa tsh ngap.nikamuuliza kwa kazi gani?yeye hakagui kwa niaba yangu.so why nimlipe?akadai ili jamaa anunue anahitaji maoni yake.nlimkatalia.

Wakaondoka jamaa hakusikika tena kuzungumzia gari.bahati nzuri ni workmate wangu after a week namwona ana IST namba DPU.sikumuuliza kitu.

But nlishangaa mlio wa ile gari na inatoa moshi kama gari moshi.unaweza sema ina smoke weed. week mbili baadaye anakuja job kwa daladala.akawa hasemi kitu ila maji yakazidi unga akaamua vunja ukimya. Kuwa fundi wake alimwambia ile gari yangu haifai sababu ni namba C akampeleka kwa jamaa mwingine. Ile gari alinunua baada ya siku mbili ikawa haiwaki.akampigia muuzaji.muuzaji akamtumia namba ya simu ya fundi umeme wa magari,gear box na fundi wa engine.

Yaani alimuuzia gari na kumkabidhi namba za mafundi.kigari kinapiga kelele.,kinavibrate...kama kina majini sometime kinajiongeza speed chenyewe.hapo kama kimefurahi.

Kikiudhika kinajishusha speed unakanyaga mafuta mpaka mwisho kinakuwa hakitaki kwenda...hapo kimeamua kususa.mimi gari yangu nafanya service tu sijawahi gusa engine wala gearbox.

Jamaa kaenda nunua plate number kigari kinamtesa balaaa...kauziwa gari na kupewa namba za mafundi kakikata umeme anaitwa fundi wa umeme.kakigoma kuingia gear anaitwa wa gearbox n.k

Wadau mnaponunua magari zingatieni ubora wa gari siyo plate namba.pateni mafundi wastaarabu na wa kweli siyo fundi dalali.
Mkuu chukua 4m niachie mimi hiyo
 
Dar gari nyingi za zamani zimeshaliwa na chumvi huku chini. Sishauri saaana kununua namba A mazingira ya Dar, labda mikoa mingine isiyo na chumvi.
Nielekeze hapo chumvi inamaliza nini kwenye vyombo vya moto kuna mtu aliwahi nambia watu wananunua bajaj za singida sana sababu body zake hazijaliwa na chumvi
 
Ushauri mzuri sana! Halafu hakuna gari imara km namba B na C.
Umeshaambiwa nunua gari yenyewe na si namba, what i want to say ni kuwa zipo namba B au C ambazo mashine bado ipo mwake but zipo pia namba B, C na D ambazo ni Achokile Mwaimbaya.

Gari vile ilivyotumika not otherwise!!
 
Pia, kama unataka kununua gari second hand usinunue kwa m'bongo utaliwa nunua kwa wahindi/warabu Ni watunzaji wazuri wa magari.
 
Back
Top Bottom