Msinunue Namba za magari badala ya Gari lenyewe

Nina kagari Toyota IST ambako kana namba CYZ jamaa mmoja alikuwa anakapenda haka kagari kutokana na condition yake.binafsi nlikanunua sababu ya mamsap baadaye akaja akawa anataka Crown "Toyota"

Kiukweli gari ipo vizuri imetembea kms 60000 plus.jamaa akaja nikamwonesha gari akakagua na kumta fundi wake mtalaam. Fundi akanishtua chamber kuwa yeye ntampa tsh ngap.nikamuuliza kwa kazi gani?yeye hakagui kwa niaba yangu.so why nimlipe?akadai ili jamaa anunue anahitaji maoni yake.nlimkatalia...
Nakubaliana na wewe asilimia 100.

Nina harrier namba C tena zile za mwanzo.

Ila inaendeshwa na mwanamke tena weekend tu.

Haijafikisha km 80,000 toka miaka hiyo.
 
Ila hizi engine za 2NZ na 1NZ za IST zikikushinda basi wewe muharibifu mana ka hujanunua kimeo IST kusema kweli hazina magonjwa ya ovyo nilichukua IST june 2015 namba DE hadi leo namwaga oil tu kikubwa huwa sizidishi kilomita 3000 zoezi kubwa nililofanya ni kubadili betri tu....

Kamechoka bampa tu sababu ya barabara mbovu ila injini kinanda
 
Kupara gari isiosumbua ni bahati tu unaweza agiza gari toka Japan ikaja bongo na ikasumbua wiki kadhaa nyuma nimewahi ona Passo DSE wanaifungua gearbox Reverse inasumbua na juzi hapa nimeona Landcruiser Cynagus DQQ wanaifungua gearbox pia...gari zingine zinazochezewa ni zilizotoka Zanzibar unakuta gari iliingia Zanzibar 2017 inaletwa bongo inapewa usajili DSX, DTG etc kumbe wameshusha KM
Japo ni asilimia kidogo sana kuagiza gari alafu ukute ni kimeo. Mara nyingi huwa nzima sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nina CH ila mashine imenyooka kama imetoka Japan juzi. Ikiwa kwenye gear husikii kitu yani nisipopiga honi naweza nikakukanyaga hata miguu maana hutajua kuna gari nyuma yako. Body nimeanza kuichakaza mimi hasa bumper tokana na njia mbovu kuelekea kwangu. Inshort Ni gari nimeuziwa na mtu makini sana nikitaka gari ingine namtafuta maana ana gari zaidi ya moja.

Kilichosumbua mwanzo ni battery tu lilikufa nikaweka jipya la Mkorea. Tangu hapo ni mwendo wa kumwaga oil na kubadilisha filter. Zaidi ya hapo ni regular maintanance kama kuweka Hydraulic na Brake Fluid zinapoisha, wiper na matairi.
Mota za kupandisha na kushusha vioo bado hazijaanza kukuzingua?
 
Kupara gari isiosumbua ni bahati tu unaweza agiza gari toka Japan ikaja bongo na ikasumbua wiki kadhaa nyuma nimewahi ona Passo DSE wanaifungua gearbox Reverse inasumbua na juzi hapa nimeona Landcruiser Cynagus DQQ wanaifungua gearbox pia...gari zingine zinazochezewa ni zilizotoka Zanzibar unakuta gari iliingia Zanzibar 2017 inaletwa bongo inapewa usajili DSX, DTG etc kumbe wameshusha KM
Mara chache sana tena sana kuagiza gari Japan ikaanza kusumbua!

Nasema hivi coz hizi kampuni za minada shindani hasa ( SBT na BEFOWARD) hawataki kuharibu reputation yao ya miaka na miaka! Unless ziwe ni kampuni uchwara..
 
Kwa mtu makini hawezi kubabaisha na D, yeye anaangalia condition ya gari
D nyingi za bei ya kitonga huwa sio nzima. Aidha inazingua umeme au gearbox au ishu yeyote ambayo itakula hela nyingi kuisolve.

Huu ni mfano tu:
IMG-20200606-WA0021.jpg

Hii gari nimetumiwa inaachiwa kwa 5M! Kwa mtu anayejua gari za kibongo hii gari huwa ina maswala ya kijinga sana ya kuzingua umeme. Saingine ni engine yake 1az huwa inamambo ya kijinga sana nayo hata kwenye Rav 4 kilitime imezoeleka kuzingua.
 
Mara chache sana tena sana kuagiza gari Japan ikaanza kusumbua!

Nasema hivi coz hizi kampuni za minada shindani hasa ( SBT na BEFOWARD) hawataki kuharibu reputation yao ya miaka na miaka! Unless ziwe ni kampuni uchwara..
Hio Landcruiser ilikua na nembo ya beforward, hio passo sikumbuki ilikua imeagizwa kutoka wapi
 
Hahahahah watu wanaamini kwamba gari zote za kutoka Japan ndio gari ambazo ni flawless. Kumbe kuna gari vichomi toka viwandani hata zikifika Japan zinatesa raia na zikishatoka mwendo ni ule ule!
Mimi mwenyewe nilikua najua hivyo ila pia kuna Legacy moja ilitoka huko Japan yenyewe ukifika 100km/h inawasha taa ya check engine
 
Mafundi wa kuokota hao fundi wako unaemwamini hawezi kukufanyia kitu kama icho
Kuna kitendo niliwah kuona kwa macho mteja anafanyiwa na mafundi...
Nasema hivii....fundi wa kibongo si ndugu yako....kua naye makini..

Unaenda na fundi wako,anakonyezwa kuwa baada ya biashara kuna laki 2 yake, unafikiri atakataa? tena unakuta huyo fundi kakaa kijiweni wiki hajaona hata elfu 30...
 
Kweli aisee huwa wanakonyezwa hao..
 
D nyingi za bei ya kitonga huwa sio nzima. Aidha inazingua umeme au gearbox au ishu yeyote ambayo itakula hela nyingi kuisolve.

Huu ni mfano tu:
View attachment 1472433
Hii gari nimetumiwa inaachiwa kwa 5M! Kwa mtu anayejua gari za kibongo hii gari huwa ina maswala ya kijinga sana ya kuzingua umeme. Saingine ni engine yake 1az huwa inamambo ya kijinga sana nayo hata kwenye Rav 4 kilitime imezoeleka kuzingua.
Hizi Noah naona watu wengi wakilalamika sana...sema tu ndiyo vile watu wanakomaa kibishi....kwa sababu mbongo huwezi kumtenganisha na Toyota..
 
Back
Top Bottom