Msinunue Namba za magari badala ya Gari lenyewe

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,272
23,046
Nina kagari Toyota IST ambako kana namba CYZ jamaa mmoja alikuwa anakapenda haka kagari kutokana na condition yake na jamaa ni mbahili pia.binafsi nlikanunua sababu ya mamsap awe anaendea salon na sokoni.baadaye akaja akawa anataka Crown "Toyota" so haka kakabaki hakana kazi.

Kiukweli gari ipo vizuri imetembea kms 60000 plus.jamaa akaja nikamwonesha gari akakagua na kumtafuta fundi wake mtalaam. Fundi akanishtua chamber kuwa yeye ntampa tsh ngap.nikamuuliza kwa kazi gani?yeye hakagui kwa niaba yangu.so why nimlipe?akadai ili jamaa anunue anahitaji maoni yake.nlimkatalia.

Wakaondoka jamaa hakusikika tena kuzungumzia gari.bahati nzuri ni workmate wangu after a week namwona ana IST namba DPU.sikumuuliza kitu.

But nlishangaa mlio wa ile gari na inatoa moshi kama gari moshi.unaweza sema ina smoke weed. week mbili baadaye anakuja job kwa daladala.akawa hasemi kitu ila maji yakazidi unga akaamua vunja ukimya. Kuwa fundi wake alimwambia ile gari yangu haifai sababu ni namba C akampeleka kwa jamaa mwingine. Ile gari alinunua baada ya siku mbili ikawa haiwaki.akampigia muuzaji.muuzaji akamtumia namba ya simu ya fundi umeme wa magari,gear box na fundi wa engine.

Yaani alimuuzia gari na kumkabidhi namba za mafundi.kigari kinapiga kelele.,kinavibrate...kama kina majini sometime kinajiongeza speed chenyewe.hapo kama kimefurahi.

Kikiudhika kinajishusha speed unakanyaga mafuta mpaka mwisho kinakuwa hakitaki kwenda...hapo kimeamua kususa.mimi gari yangu nafanya service tu sijawahi gusa engine wala gearbox.

Jamaa kaenda nunua plate number kigari kinamtesa balaaa...kauziwa gari na kupewa namba za mafundi kakikata umeme anaitwa fundi wa umeme.kakigoma kuingia gear anaitwa wa gearbox n.k

Wadau mnaponunua magari zingatieni ubora wa gari siyo plate namba.pateni mafundi wastaarabu na wa kweli siyo fundi dalali.
 
Vijana wa leo utasikia nitaftie namba DP, DQ, Mara DS
Mi nina CH ila mashine imenyooka kama imetoka Japan juzi. Ikiwa kwenye gear husikii kitu yani nisipopiga honi naweza nikakukanyaga hata miguu maana hutajua kuna gari nyuma yako. Body nimeanza kuichakaza mimi hasa bumper tokana na njia mbovu kuelekea kwangu. Inshort Ni gari nimeuziwa na mtu makini sana nikitaka gari ingine namtafuta maana ana gari zaidi ya moja.

Kilichosumbua mwanzo ni battery tu lilikufa nikaweka jipya la Mkorea. Tangu hapo ni mwendo wa kumwaga oil na kubadilisha filter. Zaidi ya hapo ni regular maintanance kama kuweka Hydraulic na Brake Fluid zinapoisha, wiper na matairi.
 
Kupara gari isiosumbua ni bahati tu unaweza agiza gari toka Japan ikaja bongo na ikasumbua wiki kadhaa nyuma nimewahi ona Passo DSE wanaifungua gearbox Reverse inasumbua na juzi hapa nimeona Landcruiser Cynagus DQQ wanaifungua gearbox pia...gari zingine zinazochezewa ni zilizotoka Zanzibar unakuta gari iliingia Zanzibar 2017 inaletwa bongo inapewa usajili DSX, DTG etc kumbe wameshusha KM
 
Mafundi wa kuokota hao fundi wako unaemwamini hawezi kukufanyia kitu kama icho
 
59 Reactions
Reply
Back
Top Bottom