Msingi wa hii dhana kuwa wanasiasa wasilipe kodi, wasishitakiwe inatoka wapi?

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,323
24,192
Huwaga nashindwa kuelewa.
Mtu kwa kujitoa kuwahudumia wananchi, wengine wanaenda mbali kusema wanawahudumia wanyonge, halafu anaacha kulipa kodi kwa miamala anayolipwa.

Mbaya zaidi akikosea kisheria hata akiua, asishitakiwe.

Miye napataga kigugumizi kuwatetea hawa watu.
 
Huwaga nashindwa kuelewa.
Mtu kwa kujitoa kuwahudumia wananchi, wengine wanaenda mbali kusema wanyinge, halafu anaacha kulipa kodi kwa miamala anayolipwa.

Mbaya zsidi akikosea kisheria hata akiua, asishitakiwe.

Wanasiasa wa Tanzania (CCM wakiongoza) ni wabinafsi kuliko jamii nyingine yoyote duniani.
 
Kutoshitakiwa kiongozi maana yake anapewa tiketi ya kufanya uhalifu.----- na wabunge wa chi walivyokuwa Rubber stamps wanaojali matumbo yao wakafumba macho na masikio.
 
Huwaga nashindwa kuelewa.
Mtu kwa kujitoa kuwahudumia wananchi, wengine wanaenda mbali kusema wanyinge, halafu anaacha kulipa kodi kwa miamala anayolipwa.

Mbaya zsidi akikosea kisheria hata akiua, asishitakiwe.

Miye napataga kigugumizi kuwatetea hawa watu.
siyo wana siasa sema viongozi wa serikali na ccm
 
Huwaga nashindwa kuelewa.
Mtu kwa kujitoa kuwahudumia wananchi, wengine wanaenda mbali kusema wanyinge, halafu anaacha kulipa kodi kwa miamala anayolipwa.

Mbaya zsidi akikosea kisheria hata akiua, asishitakiwe.

Miye napataga kigugumizi kuwatetea hawa watu.
Yaani iko hivi wao ndio walioandika mpini wa maamuzi ndio maana Tanzania mtu kuacha taaluma yake Kama ualimu,uhandisi,udaktari au ufundi ili akafanye siasa ni mafanikio anakua ameukata au wanasema ametoboa zaidi hata wafanyabiashara na viongozi wa dini wanaenda huko kulinda maslahi yao binafsi kimsingi Tanzania siasa sio huduma na mchongo au dili
 
Wanasheria mliomo humu JF, tunawezaje ku petition ili suala hili liweze kufikishwa kunako husika na sheria zibadilishwe?
Issue ni kuanza na katiba bora itakayokua kwaajili ya wananchi yaani katiba itakayopeleka mamlaka,wajibu,haki na nguvu kwa wananchi kusimamia na kuamua juu mustakabali wa nchi yao
 
Tawala za zamani za wafalme na machifu.
Ni uthibitisho kuwa jamii bado kustaarabika na demokrasia haipo.
Hata hivyo, wananchi wanatakiwa kujua kuwa binadamu wote ni sawa na haikubaliki zama hizi kuwepo mabwana na watwana.
 
Huwaga nashindwa kuelewa.
Mtu kwa kujitoa kuwahudumia wananchi, wengine wanaenda mbali kusema wanyinge, halafu anaacha kulipa kodi kwa miamala anayolipwa.

Mbaya zsidi akikosea kisheria hata akiua, asishitakiwe.

Miye napataga kigugumizi kuwatetea hawa watu.
Tunajitengenezea ukoloni ndani ya nchi yetu kwa hizi sera na sheria mbovu za Bunge.
 
Wanasiasa wa Tanzania (CCM wakiongoza) ni wabinafsi kuliko jamii nyingine yoyote duniani.
Wanasheria mliomo humu JF, tunawezaje ku petition ili suala hili liweze kufikishwa kunako husika na sheria zibadilishwe?
Tunajitengenezea ukoloni ndani ya nchi yetu kwa hizi sera na sheria mbovu za Bunge.
Kweli mkuu, tunatengeneza tabaka ka watawala watakaoirthi nchi.
Sasa hivi Rais Mwinyi na mwanae Rais Mwinyi.
Huko mbele inaelekea tutaoata Rais Kikwete mwingine.

Mwalimu hakutuacha hivi, kutengeneza koloni la viongozi.
 
Wanasheria mliomo humu JF, tunawezaje ku petition ili suala hili liweze kufikishwa kunako husika na sheria zibadilishwe?
Kweli mkuu, tunatengeneza tabaka ka watawala watakaoirthi nchi.
Sasa hivi Rais Mwinyi na mwanae Rais Mwinyi.
Huko mbele inaelekea tutaoata Rais Kikwete mwingine.

Mwalimu hakutuacha hivi, kutengeneza koloni la viongozi.
Ukweli ndiyo huo.
 
Tunapoelekea kama hatutabadili huu mfumo uliopo,watoto wetu,wajukuu na vitukuu "watatawaliwa" na wakina Kikwete, Mwinyi, kama vile "tawala za kurithishana za kifalme".
 
Back
Top Bottom