Mzanzibari Huru
JF-Expert Member
- Apr 17, 2014
- 393
- 234
Ndugu Wana Jamii
Kwanza nakuamkieni kwa heshima na taadhima.
Mbele yetu zinakaribia siku za kampeni za kisiasa, zoezi muhimu sana linalowapa Watanzania uhuru wa kutowa ridhaa zao juu ya viongozi wanaowataka kusimamia maisha yao kiujumla. Kwa lugha nyingine, ni kwamba tunaingia katika uchaguzi mkuu.
Katika chaguzi fulani zilizopita nyuma, tumegundua baadhi ya wagombea walikuwa wakileta sera za kuwatukana Waarabu. Hatufamu ni kwasbabu gani wanachagua kufanya hivyo, ingawaje Tanzania ni nchi ya makabila tofauti, na yapo makabila mbali mbali hata ya kibantu ambayo asili yake sio Tanzania.
La kushangaza zaidi, wanashiriki kuwatukana Waarabu sio wanaogombania vyiti vya siasa tu bali hata viongozi wa didni fulani fulani hivi. Yaani hawa ndio wanaochokesha hata kuwasikliza, kwanini hawa wasiimbishe kwaya zao, wakapokea sadaka wakaenda kujinunulia magari tu, Waarabu wamewakosa nini? Mwengine alokuwa hata hana uwezo wa kuyapima maneno yake, akawa anasema Zanzibar wanataka nchi yao kwa sababu wanataka kujifundisha Kiarabu; huyu mzee sijui alikuwa anakula breakfast gani.
Ninalotaka kuwafahamisha hao ni kwamba binadamu wa kwanza kuweka mguu wake katika visiwa vya Unguja na Pemba, kabla ya kuitwa kwa majina hayo ni Washirazi kutoka Persia, sasa kunaitwa Iran. Wakifuatiliwa na Waarabu. Athari za watu kutoka Persia zipo hadi leo; kwanza katika lugha ya Kiswahili, maneno mengi sana yana asili ya Kifarsi (Farsi ni lugha ya Persia sasa Iran). Nitaweka hapa katika makala hii maneno machache maarufu zaidi:
Bibi, babu, dada, kaka, bwana, shanuo, gunia, kelele, mbuzi, karakana, bangi, jambazi, malaya, bandari, jahazi, nanga, nahodha, tumbaku, pamba, kitani, rangi, chapa, bahati, balungi na maneno mengi sana, yaani Kiswahili kimejengwa na Kiarabu na Kifarsi
Zaid ya hapo katika mambo ya kijamii, kule Makunduchi wanaendeleza utamaduni wauitao kogo la mwaka; wanafanya sherehe hizo mara moja kwa mwaka. Sehemu moja katika sherehe hizo ni kuzungumka moto. Wanachoma makuni mengi halafu wanafanya duwara kubwa la watu na kuzungumka moto huo. Kwa wale wanajuwa mambo ya dini mbali mbali, watajuwa kwamba huo ni utamaduni wa Zoroasterians; huo ni utamaduni uloletwa na Washirazi.
Zaidi ya hapo, ukimuuliza Mzanzibari, ni nani Mzanzibari asilia hapa visiwani, jawabu itakuwa ni Mshirazi. Munakumbuka Shirazi association waliojiunga na African Association wakafanya Afroshirazi Party, Ndio hao basi.
Tunajuwa mtu yoyote anayehama kwao kwa hiyari yake, huwa ananasabu mbali mbali lani zaidi ni za kimaisha, hadi leo hii. Waarabu na washirazi walilazimika kusafiri ili kutafuta maisha bora au mali ghafi za siku hizo. Watu kutoka Mrima na sehemu nyengine za mwambao wa Bara la Afrika Mashariki hawakuwa na sababu yoyote ya kundoka katika miji na vijiji vyao na kuja Visiwani. Sababu wao walikuwa na maisha yao kamili, wanyama, mashamba, mimea, misitu, na bahari ya kuvua samaki.
Watu kutoka Mrima, sasa Tanganyika, na bara nyenginezo, kama vile Nyasaland, Msumbiji na hata Uganda, waliletwa Zanzibar. Hio sio aibu kwa sababu waliletwa kuifanya kazi maalumu.
Watawala wote wanaotajwa katika historia yetu hapa Zanzibar walikuwa Waarabu, mukisia Makama ndume, Mwinyi Mkuu, na wengineo. Hakujawahi Zanzibar kuwa na kiongozi Muafrika isipokuwa kuanzia 1964.
Kwa ufupi sana, ningependa kuwaambia hao wanaojitaarisha kuwatakuna Waarabu kwamba Zanzibar ipo tu karibu na bara la Afrika.
Bora mungeendeleza shughuli zenu za kukusanya sadaka kabla watu hawaja amka; wakiamka baada ya kuimbisha kwaya mutatuta mejembe mukalime.
Ahsanteni.