Naomba sana ujumbe huu uwafikie wahusika.
Miongoni mwa njia wanazotumia viongozi wa vyama vya msingi kujitajirisha kwa kuwaibia wakulima ni kuwa na mawe ya mzani yanayoiba.
Tatizo hili ni kubwa kuliko inavyodhaniwa lakini halijaguswa wala kuzungumzwa. Na mwaka huu hali imekuwa mbaya zaidi.
Mfano katika kijiji cha Chitowe kilichopo Nanyumbu, Masasi kati ya kilo 1200 ambazo nilishazipima, kiasi cha kilo 70 zimepungua na hali hiyo ni kwa kila mtu anayekwenda kupima anakutana nayo.
Ajabu ni kwamba, jambo hili linafahamika miaka nenda rudi lakini hakuna hatua zozote stahiki zinazochukuliwa. Au labda ni mpango wa upigaji unaofadhiliwa na wakubwa?
Hebu Waziri na Naibu Waziri fanyeni jambo kunusuru hali hii wakulima wanaumia sana.