Lindi: Bei ya korosho kwa mnada wa tano kwa msimu wa mwaka 2019/20 katika chama kikuu cha ushirika cha RUNALI imeongezeka

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
1575276400152.png


Bei ya korosho kwa mnada wa tano, msimu wa 2019/2020 katika chama kikuu cha ushirika cha RUNALI, mkoa wa Lindi imeongezeka ikilinganishwa na mnada wa wanne.

Akizungumza na Muungwana Blog mara tu ya kukamilika kwa mnada huo uliofanyika katika ghala la Umoja, lililopo mjini Liwale. Meneja mkuu wa chama hicho, Jahida Hassan alisema bei ya juu katika mnada huo ilikuwa shilingi 2,857 kwa kila kilo moja. Wakati bei ya chini ilikuwa shilingi 2,817.

Jahidi alisema bei hizo ni tofauti na bei za mnada wa nne uliofanyika mjini Nachingwea kwenye viwanja vya ofisi za chama kikuu hicho. Kwani bei ya juu ilikuwa shilingi 2,812 na bei ya chini ilikuwa shilingi 2,795 kwa kila kilo moja.

Meneja huyo alizitaja kampuni zilizofanikiwa kununua korosho ni 5 kati ya 17 zilizoshiriki na kuomba kununua. Ambazo ni Kasuga, Royol nuts, Imperial, MGM na Iscon.

'' Korosho zilizofikishwa mnadani ni tani 2554.697. Hata hivyo mahitaji ya kampuni hizo yalikuwa tani 11860.124. Utaona yakuwa mahitaji yalikuwa makubwa kuliko kiasi cha korosho zilizofikishwa mnadani,'' alisema Jahida.

Meneja huyo alisema katika ghala la Umoja lililopo Liwale kampuni ya Royal nut ilinunua tani 158 kwa bei ya shilingi 2,857 kwa kila kilo moja, kampuni ya Kasuga tani 150 kwa bei ya shilingi 2,857, kampuni hiyo ya Kasuga ilinunua tena tani 150 kwa bei ya shilingi 2,830. Huku kampuni ya Royal nut ilinunua tena katika ghala hilo tani 55 kwa bei ya shilingi 2,827.

'' Katika ghala la Lindi farmers kampuni ya Iscon imenunua tani 600 kwa bei ya shilingi 2,836, kampuni ya Imperial imenunua tani 250 kwa bei ya shilingi 2,830. Na kampuni ya Iscon kwa mara nyingine kwenye ghala hilo imenunua tani 337 kwa bei ya shilingi 2,828,'' alisema Jahida.

Mbali na maghala hayo makuu mawili yaliyopo katika wilaya za Nachingwea na Liwale. Meneja huyo alizitaja kampuni zilizonunua korosho zilizopo katika ghala la Lipande lililopo katika wilaya ya Ruangwa.

Alisema katika ghala hilo la Lipande kampuni ya Iscon imenunua tani 459 kwa bei ya shilingi 2,826, kampuni ya MGM tani 250 kwa bei ya shilingi 2,819. Wakati kampuni ya Iscon kwa mara nyingine kwenye ghala hilo imenunua tani 144 kwa bei ya shilingi 2,817.

Wakati bei ikiendelea kupanda, huku mahitaji ya kampuni yakiwa makubwa wakati korosho zinazofikishwa mnadani ni kidogo. Uchunguzi uliofanywa na Muungwana umebaini kwamba korosho nyingi zipo kwenye maghala ya vyama vya msingi vya ushirika zikiwa zimemwagwa sakafuni.

Hali hiyo ambayo inatokana na uhaba wa vifungashio, imesababisha baadhi ya maghala hayo kufungwa kutokana na kukosa nafasi. Hivyo ununuzi kwenye maghala hayo yaliyofungwa umesimama. Huku korosho za wakulima wengi zilizouzwa katika minada namba tatu na nne zikiwa hazijapelekwe kwenye maghala makuu kwa ajili ya mauzo.
 
elivina shambuni, Wewe uwache kuwa unaandika habari za uongo kila siku, bei hiyo ni pungufu sana kwani bei ya juu kabisa ilikuwa ni 2898
 
Eti zao linaloingza fedha nyng za kigen, wakulima wanashndwa kuuza kwa kuwa hakuna magunia, haya ni maajabu sana, mpk gunia ni mtihan?
Halafu kuna waziri,

Manaibu wawili,

Wakurugenzi ofisini, Bodi za korosho n.k n.k.
 
Back
Top Bottom