Daudi Mchambuzi
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 62,190
- 128,264
Kweli kabisa, Zitto yuko makini sana kudhoofisha upinzani tz.Zitto ni mwanasiasa makini Wa kizazi chetu
Last edited by a moderator:
Kweli kabisa, Zitto yuko makini sana kudhoofisha upinzani tz.Zitto ni mwanasiasa makini Wa kizazi chetu
Msimamo upi sasa hapo kwamba Zitto ni Popo maana yuko kote kote ......Zitto ni historia
Mara anasema yeye sio UKAWA mara ataingia na na UKAWA kutohudhuria Bunge , aeleweke vipi huyu Popo ?
Ngoja msukule wake mwl.kaijage uje
anaposema anapenda ijadiliwe rasimu ya warioba maana yake naye ni UKAWA. Aache kuendeleza siasa zake za KINAFIKI na KINDUMILA KUWILI.Anatamani kula kote kote.Is opportunistic
huyu jamaa anakuwaga na kauli mbilimbili haswa anaporopoka jambo, akiona upepo unamwendea vibaya anarudi na kauli nyingine
Ni aibu sana kwa kijana kama ZZK kushiriki ktk harakati za kuangamiza Vyama Vya Upinzani Tanzania kwa lengo LA kukibakisha CCM madarakani iendelee kutawala kiimla ktk nchi yetu
Huyu jamaa anaizihilishia jamii ya kitanzania kwamba yeye ni msaliti mkubwa ana upande na anaonekana ana ajenda ya siri na Ccm na hii ina onyesha kwamba wapinzani jamani wanacho pigania kwa wananchi wa TZ ni haki Zitto mwenyewe ana kubali lakini asemi duuuh wana JF mnajua ni aibu Kubwa sana kwa huyu kija ameonyesha dhahili shahili kwamba ana njaa yakufamtu eee Mwenyezi Mungu humuremu madhambi yake Amen!!!!
ZZK ni kigeugeu
Exactly. anakubaliana na ukawa na wazo la kutorudi bungeni kama rasimu ya Warioba haitojadiliwa lakini amekiri kuwa yeye sio Ukawa.Kimsingi anakubaliana na Madai ya UKAWA.
Hiki ndio cha msingi ambacho Mpaka huyu mnafik anakubaliana nacho...
Tangu lini mbunge wa mahakama akawa na upande.Mahakama haina upandeMSIMAMO WA NDUGU ZITTO KABWE KUHUSU MCHAKATO WA KUANDIKA KATIBA MPYA
Jana tarehe 29 Julai, 2014 nimefanya mahojiano katika kipindi cha PowerBreakFast kinachorushwa na Clouds FM. Baadhi ya vyombo vya habari vimeandika mahojiano yale. Napenda nitoe ufafanuzi kidogo kuhusu msimamo wangu kuhusu mchakato wa Katiba.
Kwanza, Mimi sijawahi kuwa UKAWA wala kundi lolote lile katika Bunge Maalumu la Katiba isipokuwa kundi linalotaka maridhiano. Msimamo wangu kuhusu Muungano ni Serikali Tatu Zilizoboreshwa (S3z) ili kuwa na Muungano imara usio tegemezi wala egemezi kwa Washirika wake.
Pili, Mimi niliunga mkono protest ya baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kupinga lugha za matusi na lugha za kibaguzi zilizokuwa zinaendelea ndani ya mkutano ule. Vilevile niliunga mkono kwamba Rasimu inayopaswa kujadiliwa ni Rasimu iliyotokana na Tume ya Marekebisho ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Sinde Warioba. Nasisitiza umuhimu wa kupata Katiba BORA itakayoimarisha DOLA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tatu, kwa hali ya sasa kuna mkwamo katika kupatikana kwa Katiba Bora. Mkwamo unaotokana na kutokuwepo kwa nia ya dhati ya kupata maridhiano ya pande zinazopingana. UKAWA hawataki mazungumzo na Viongozi wa Bunge la Katiba badala ya kujenga maridhiano kila siku wanawabeza UKAWA jambo ambalo kamwe haliwezi kujenga mwafaka. Ushauri wangu ni kuahirisha mchakato mzima wa kuandika Katiba mpaka mwaka 2016 baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Katiba ya sasa ifanyiwe marekebisho machache kama ifuatavyo;
i) Tume ya Uchaguzi ili iwe huru na ionekane kuwa huru, ikiwemo kuwaondoa watumishi wa Halmashauri za Wilaya, Miji na Majiji katika kusimamia uchaguzi
ii) Kuruhusu mgombea binafsi
iii) Kuondoa Mafuta na Gesi kama Jambo la Muungano ili Zanzibar ianze mara moja kusimamia kwa uhuru utafutaji wa Mafuta katika vitalu vilivyopo upande huo wa Muungano
Mkutano wa Bunge Maalumu utakaofanyika bila kuwepo kwa maridhiano utakuwa hauna maana yeyote na itakuwa ni sawa na kupoteza muda na fedha za walipa kodi ambazo zingeweza kununua madawa vijijini. Mimi binafsi sitahudhuria mkutano wa Bunge Maalumu kama makundi hasimu hayatakuwa yamefikia maridhiano.
Kabwe Zitto, MB/MBMK
Hapana jamani. Deus Kibamba na yeye amependekeza ijadiliwe rasimu ya Warioba inamaana na yeye Deus ni UKAWA?
Mbona tunakuwa biased jamani!!
ndibalema unapomchukia mtu unamchukia na.lolote lile
alichokionyesha hapo huyo HAKISAWA ni aina ya raia tulio nao, gullible,stupid etc
kwa kauli ya zitto i would think yy ni Ukawa na hayuko against nao
analalamika ukawa kusemwa vibaya
anashauri bunge livunjwe
SIJAONA TATIZO LA KAULI YA ZITTO Hapo
Ndibalema ndio tulipofika hapa na hawa watanzania wenzetu....
sijui tuombe
ndibalema unapomchukia mtu unamchukia na.lolote lile
alichokionyesha hapo huyo HAKISAWA ni aina ya raia tulio nao, gullible,stupid etc
kwa kauli ya zitto i would think yy ni Ukawa na hayuko against nao
analalamika ukawa kusemwa vibaya
anashauri bunge livunjwe
SIJAONA TATIZO LA KAULI YA ZITTO Hapo
Ndibalema ndio tulipofika hapa na hawa watanzania wenzetu....
sijui tuombe
Mimi binafsi sitahudhuria mkutano wa Bunge Maalumu kama makundi hasimu hayatakuwa yamefikia maridhiano.umeelewa sasa
kidogo lisu anamkaribia.Zitto ana akili kuliko machadema wote.
Zitto, alikuwa zamani huyu wa leo ni kama chui wa karatasi tu...........hana madhara hata kidogo....
Mkuu naona kama hujaelewa...mbona naona kama Zitto yuko kivyake-vyake?
..hata anapotaja Ukawa anawataja kama "wale" na siyo "sisi."
..kwa mfano anasema "viongozi wa Bunge la Katiba wanawabeza Ukawa..." badala ya kusema "viongozi wa Bunge la Katiba wanatubeza sisi tulioko Ukawa..."
..sasa hii inatoka kwenye written statement ya Zitto ambapo alikuwa na muda wa kutafakari maana ya kile alichoandika.
..pia Ukawa wamefanya mikutano kadhaa mikoani na sidhani kama Zitto amewahi kushiriki mkutano wowote ule.
cc Ndibalema, Haki sawa