Msimamo wa Zitto Kabwe kuhusu Katiba mpya

Msimamo wa Zitto Kabwe kuhusu Katiba mpya

ni wahuni tu kama watu wengine.UKAWA wanapewa 450000 na wafadhili toka nje ya nchi kila mmoja wakwamishe katiba yetu.hawataweza nawaambia

Tutajie hizo nchi ili Raia wema tuzijue.Kama hamwezi kuzitaja basi Serikali ya ccm inapoteza uhalali wa kutuongoza kwa sababu haina ujasiri wa kuwataja maadui wa taifa.
 
Hata mm sina imani na UKAWA!Muundo wa serikali 3 haijathibitika kama tukipata ndiyo tutaondokana na umaskini huu wa kutisha!

UKAWA wanapoteza nafasi adimu ya kuwapa watz katiba yenye mustakabali wao!Rasimu ya Warioba ina vipengele vingi muhimu vitakavyo badilisha maisha ya Watz zaidi ya serikali tatu wanayotaka tuamini ndiyo tiba ya maisha hoe hae ya Mtz!!

Vipengele muhimu ktk rasimu ya Warioba ni:
(1)Tume huru ya uchaguzi
(2)Bunge tu liwe na uwezo wa kupeleka nchi vitani
(3)Majaji wateuliwe na Rais waidhinishwe na Bunge na Rais asiweze tena kuwafukuza
(4) Kufutwa kwa viti maalum vya Ubunge
(5)Pesa za serikali zidhibitiwe na Bunge sio kama sasa Gavana anaipa serikali pesa yyt wakiomba!Madai tajwa hapo juu yana umuhimu mno kurekebishwa now zaidi hata ya muundo wa serikali yetu uweje!

UKAWA eleweni kuwa katiba ni compromise sio kila kitu mnachotaka mtapewa na sio kila kitu CCM wanachopewa watapata!Wapeni CCM serikali 2 na wao wawapeni madai hayo 5 juu mtakuwa na nafasi nzuri ya kuiondoa CCM mwakani!

Bila Tume huru hamuiondoi CCM kwenye sanduku la kura hata iweje!
CC MwanaDiwani Lizabon ifweero Simiyu Yetu


hujafikiri nje ya boksi, kama wameweza kuua moyo wa katiba washindwe na kidole? tume si kidole tu, watakinyofoa na hayo mengine yote wataweka watakavyo wao.

na mkiwepo mtageuzwa mashahidi
 
hujafikiri nje ya boksi, kama wameweza kuua moyo wa katiba washindwe na kidole? tume si kidole tu, watakinyofoa na hayo mengine yote wataweka watakavyo wao.

na mkiwepo mtageuzwa mashahidi

Mkuu sasa wakifanya hivyo ndiyo tutajua ni wakorofi CCM lkn kwa sasa wana point nzuri tu kuwa UKAWA wanataka kila dai lao lipite wakati katiba ni compromise!

Maoni yangu kuna madai ya maana UKAWA hawaongelei lkn wao wamejikita kwenye muundo wa serikali as if ndiyo jambo pekee lililomo ndani ya rasimu
 
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), kwa mara ya kwanza ameibuka na kupingana na harakati za Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Zitto amesema hana uhakika wala hauamini Ukawa kama utakuwa umoja endelevu hadi kufikia Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, kwa sababu si mara ya kwanza vyama vya upinzani kuungana na kugawanyika.

Mbali ya kutokuwa na imani na umoja huo, pia ameitaka Serikali kusitisha mchakato wa Katiba Mpya hadi uchaguzi mkuu utakapomalizika.

Alisema ni vema mchakato huo ukasitishwa kwa sasa, kwani inaonekana wajumbe wa Bunge hilo wanafuja fedha za umma.

Zitto alitoa kauli hiyo jana, wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa na kituo cha redio cha Clouds cha jijini Dar es Salaam.

Alisema Watanzania wanakabiliwa na changamoto nyingi na si Katiba pekee.

Alisema siku zote Watanzania wamekuwa wakipenda kuwa na upinzani imara ambao watu wanaweka tofauti zao pembeni na kuungana dhidi ya chama ambacho kinaongoza, lakini haoni kama Ukawa utaendelea hadi kufikia kipindi cha Uchaguzi Mkuu.

Alisema hatua ya kusimama kwenye ajenda moja ya Katiba haitausaidia umoja huo, kwani kipindi cha uchaguzi mkuu kinakuwa na ajenda nyingi.

Alisema wananchi watapenda kusikia masuala ya kushughulikia rushwa, matumizi ya rasilimali, maji, umeme, afya na barabara.

“Mambo haya ndiyo yatakayowafanya wananchi waamue namna gani watakabidhi dhamana ya uongozi, si suala la Katiba pekee,” alisema Zitto.

Alisema tusijitoe ufahamu kwa kudhani kwamba hii ndio mara ya kwanza kwa upinzani kuungana.

“Kulikuwa na Kamati ya Mabadiliko ya Katiba (KAMAKA) pia katika chaguzi za mwaka 1995, mwaka 2000 wapinzani waliungana vilevile, lakini kila inapokaribia uchaguzi wamekuwa hawaelewani kwa kuwa kila mtu anataka chama chake kipeperushe bendera.

“Lakini kama Ukawa wataweza kuweka ajenda yao mpaka mwisho itakuwa jambo jema kwa wananchi wenyewe. Kwa sababu nchini kwetu tatizo kubwa ni usimamizi na uwajibikaji, kama ajenda itachukua nafasi naamini hali haitakuwa mbaya, lakini bado siamini na sina uhakika kama umoja huu ni endelevu kwa namna ambavyo tunaona, ni umoja ambao unatokana na matakwa ya sasa ya Katiba, wameungana kwa sababu ya serikali tatu, lakini aina gani ya serikali bado hili linaweza kuwagawa,” alisema.

… mchakato wa Katiba Mpya usitishwe

Akitolea ufafanuzi hoja yake ya kusitisha mchakato wa Katiba Mpya, Zitto alisema ni vyema serikali ikausitisha ili kunusuru fedha za umma zisiteketee.

Alisema fedha hizo zinastahili kutumika kununua madawa, kuendeleza miradi ya maji na kusomesha Watanzania, hivyo hakuna sababu fedha hizo kutumika kwa ajili ya kupiga porojo na kutukanana ndani ya Bunge.

“Nashauri tuahirishe mchakato huu mpaka baada ya uchaguzi mkuu mwaka kesho, ndipo hapo tuwe na mamlaka ya kujadili mchakato huu na kumaliza.

“Pia uchaguzi unaweza kuchekecha na ukaondoa baadhi ya watu ambao ni vikwazo katika mchakato kwa sababu uchaguzi hauna muamala, mtu ambaye alikuwa mbunge anaweza kuondolewa,” alisema.

Aidha, alisema kabla ya kwenda kwenye uchaguzi mkuu, Katiba ya sasa inatakiwa kurekebishwa baadhi ya maeneo ambayo ni vikwazo, kama vile Tume huru ya uchaguzi, kipengele cha wagombea binafsi kiwekwe na maeneo ambayo Zanzibar wamekuwa wakiyahitaji katika Katiba mpya, kwa mfano suala la mafuta na gesi yawekwe.

Alisema hakuna sababu ya kugawa nchi na kutumia rasilimali zilizopo kwa kufanya kazi ambayo haina matunda.

…amtetea January

Katika hatua nyingine, Zitto, ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, alisema amesikitishwa na mashambulizi yanayoelekezwa kwa Mbunge wa Bumbuli (CCM), Januari Makamba, baada ya kutangaza nia ya kuwani urais mwaka 2015.

Alisema kila kijana anapojitokeza kwa ajili ya kutaka kushiriki katika mamlaka za nchi, hasa katika nafasi kama hiyo ya urais, kumekuwa na mashambulizi makubwa dhidi yake.

“Ni hatua ambayo sio nzuri kwa sababu kwa mujibu wa takwimu, idadi ya watu asilimia 72 wapo chini ya miaka 30, asilimia 65 ya wapiga kura ni vijana wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 40, hivyo vijana wana haki ya kushiriki katika uongozi wa nchi, tufahamu changamoto za maendeleo ya nchi yetu zinahitaji uongozi mpya wa kizazi kipya.

“Ni dhahiri neno ujana si sifa, lakini neno uzee pia si sifa, hivyo tunatakiwa kuwapima vijana kwa sifa zilizopo, kama vile za kikatiba na zile za ziada, badala ya kusema vijana hawajakomaa… nilisikitika sana na mashambulizi ambayo yalielekezwa dhidi ya Makamba, natoa wito kwamba tuache, kwani wenye uamuzi wa mwisho ni wananchi.

“Mtu akigombea na kama akitoa sera zake vizuri wananchi wakamwelewa, akichaguliwa ni wananchi wameamua, hakuna mtu mwenye mamlaka kuwa fulani ni kijana, nadhani lazima tubadilishe uongozi na watu wajue nchi hii ni ya vijana, hatusemi wazee hawawezi ila wao wabaki kuwa washauri kama wao walivyokuwa vijana katika kipindi cha Nyerere nao walikuwa na miaka 40. Hivyo kuna haja ya kuweza kufikia hapo, changamoto za nchi ni kubwa, kuna haja ya aina mpya ya uongozi na mimi naamini aina hiyo itatoka kwa viongozi vijana,” alisema.

Hiyo ni mara ya kwanza kwa Zitto, ambaye yuko ndani ya Chadema kwa sababu za kisheria, kuibuka na kuuzungumzia Ukawa.
Mwanasiasa huyo kijana amekuwa kimya kwa muda mrefu, hata kwenye harakati za Ukawa amekuwa aghalabu kuonekana, hali ambayo imekuwa ikiibua maswali yuko upande gani katika mchakato huu wa Katiba Mpya.

Kauli hii ya Zitto inaweza kuibua fikra mpya kwa baadhi ya watu ambao wamekuwa na imani kubwa na umoja huo unaoviunganisha baadhi ya vyama vya siasa nchini.

Makamba aufananisha na Paka

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba, ameufananisha Ukawa kuwa ni sawa na paka, kwa kuwa tambo za wajumbe wa kundi hilo zitakwisha mwaka 2015 katika kuusaka urais.

Makamba alitoa kauli hiyo alipozungumza na MTANZANIA Jumatano katika mahojiano maalumu yaliyofanyika nyumbani kwake Tegeta, jijini Dar es Salaam.

Alisema Ukawa ni umoja ulioundwa kwa lengo la kuwahadaa wananchi katika kipindi hiki cha mchakato wa Katiba Mpya, lakini hautakuwapo mwaka 2015.

“Mimi ni mwana CCM, nasema kwa hali hii tutawachapa kweli wapinzani katika uchaguzi ujao… kwa sababu huu Ukawa ni umoja wa paka, paka walikaa siku moja wakasema jamani tuungane, wakachukua kamba wakajifunga mikia ili wawe wamoja, lakini alipotokea panya wote walisambaratika, kwa sababu kila mmoja alikuwa anamtaka panya.

“Kwa kuwa kila chama kinataka kuwa na rais, nina hakika huu muungano wao hautaendelea, watasambaratika kama walivyosambaratika paka. Wakati wa urais hakuna Ukawa!” alisema.

Alisema hata Ukawa wasiporudi ndani ya Bunge Maalumu la Katiba na kukwamisha upatikanaji wa Katiba Mpya, Uchaguzi Mkuu utafanyika kwa kutumia Katiba iliyopo.

“Nakumbuka vyama vya upinzani wakati mimi nikiwa Katibu Mkuu moja ya hoja walizokuwa waking’ang’ania ni Katiba Mpya na Dk. Slaa alikuwa akiwaahidi Watanzania kuwa wakimpatia nchi atawapatia Katiba Mpya… sasa Rais Kikwete amesema uchaguzi ujao ufanyike na Katiba Mpya, kwanini wanatoka Bungeni? Mnataka nini? Rudini Katiba ipatikane kama kweli mna nia ya dhati!

“Usilalamikie wingi wa CCM kwa sababu ndio uzuri wa kushinda. Hata wao wangekuwa wengi wangefanya hivi ili sera za chama zipite, warudi bungeni katiba mpya ipatikane. Wasikimbie hoja,” alisema.

Aidha alizungumzia mfumo wa Serikali tatu uliopendekezwa ndani ya rasimu ya pili ya Katiba na kusema huo ni mzigo kwa Watanzania.



SOURCE: MTANZANIA

Mimi kwa maoni yangu namuunga zitto mkono kwamba ni vigumu upinzani kuungana kwa sababu zitto yeye mwenyewe ni mpinzani dhidi ya vyama vya upinzani. yeye ndio bingwa wa mipango hii yote wakisaidiana na ccm na ACT yake. eti anataka Lowasa akiwa rais ampe uwaziri mkuu. kwa hiyo tusishangae anachokisema zitto kwa sababu yeye zitto+mwigamba+kitila mkumbo wameanzisha mradi wa kuhakikisha upinzania kaukuwi tanzania.

Vile vile kwenye swala la rushwa zitto hana maadili kuzungumzia vita ya rushwa na ufisadi maana na yeye ameishaanza harakati za kukuza rushwa. wale madiwani wa shinyanga wanaoomba kurudi chadema wamesema zitto anashirikiana na wana ccm kama nchemba+ridhiwani,nape,masele kuhonga madiwani ili waondoke chadema. zitto huna credibility ya kupambana na rushwa.
 
Zitto, alikuwa zamani huyu wa leo ni kama chui wa karatasi tu...........hana madhara hata kidogo....
 
MSIMAMO WA NDUGU ZITTO KABWE KUHUSU MCHAKATO WA KUANDIKA KATIBA MPYA

Jana tarehe 29 Julai, 2014 nimefanya mahojiano katika kipindi cha PowerBreakFast kinachorushwa na Clouds FM. Baadhi ya vyombo vya habari vimeandika mahojiano yale. Napenda nitoe ufafanuzi kidogo kuhusu msimamo wangu kuhusu mchakato wa Katiba.

Kwanza, Mimi sijawahi kuwa UKAWA wala kundi lolote lile katika Bunge Maalumu la Katiba isipokuwa kundi linalotaka maridhiano. Msimamo wangu kuhusu Muungano ni Serikali Tatu Zilizoboreshwa (S3z) ili kuwa na Muungano imara usio tegemezi wala egemezi kwa Washirika wake.

Pili, Mimi niliunga mkono ‘protest' ya baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kupinga lugha za matusi na lugha za kibaguzi zilizokuwa zinaendelea ndani ya mkutano ule. Vilevile niliunga mkono kwamba Rasimu inayopaswa kujadiliwa ni Rasimu iliyotokana na Tume ya Marekebisho ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Sinde Warioba. Nasisitiza umuhimu wa kupata Katiba BORA itakayoimarisha DOLA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tatu, kwa hali ya sasa kuna mkwamo katika kupatikana kwa Katiba Bora. Mkwamo unaotokana na kutokuwepo kwa nia ya dhati ya kupata maridhiano ya pande zinazopingana. UKAWA hawataki mazungumzo na Viongozi wa Bunge la Katiba badala ya kujenga maridhiano kila siku wanawabeza UKAWA jambo ambalo kamwe haliwezi kujenga mwafaka. Ushauri wangu ni kuahirisha mchakato mzima wa kuandika Katiba mpaka mwaka 2016 baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Katiba ya sasa ifanyiwe marekebisho machache kama ifuatavyo;

i) Tume ya Uchaguzi ili iwe huru na ionekane kuwa huru, ikiwemo kuwaondoa watumishi wa Halmashauri za Wilaya, Miji na Majiji katika kusimamia uchaguzi

ii) Kuruhusu mgombea binafsi

iii) Kuondoa Mafuta na Gesi kama Jambo la Muungano ili Zanzibar ianze mara moja kusimamia kwa uhuru utafutaji wa Mafuta katika vitalu vilivyopo upande huo wa Muungano

Mkutano wa Bunge Maalumu utakaofanyika bila kuwepo kwa maridhiano utakuwa hauna maana yeyote na itakuwa ni sawa na kupoteza muda na fedha za walipa kodi ambazo zingeweza kununua madawa vijijini. Mimi binafsi sitahudhuria mkutano wa Bunge Maalumu kama makundi hasimu hayatakuwa yamefikia maridhiano.

Kabwe Zitto, MB/MBMK

 
Tunasubir muda tu nasema bora Zitto anachakusema kwa watu kuhusu maendeleo ya wananchi kuliko yyte ndan ya CDM,
 
Msimamo upi sasa hapo kwamba Zitto ni Popo maana yuko kote kote ......Zitto ni historia
 
Mara anasema yeye sio UKAWA mara ataingia na na UKAWA kutohudhuria Bunge , aeleweke vipi huyu Popo ?
 
anaposema anapenda ijadiliwe rasimu ya warioba maana yake naye ni UKAWA. Aache kuendeleza siasa zake za KINAFIKI na KINDUMILA KUWILI.Anatamani kula kote kote.Is opportunistic
 
mara anasema yeye sio ukawa mara ataingia na na ukawa kutohudhuria bunge , aeleweke vipi huyu popo ?

huyu jamaa anakuwaga na kauli mbilimbili haswa anaporopoka jambo, akiona upepo unamwendea vibaya anarudi na kauli nyingine
 
anaposema anapenda ijadiliwe rasimu ya warioba maana yake naye ni UKAWA. Aache kuendeleza siasa zake za KINAFIKI na KINDUMILA KUWILI.Anatamani kula kote kote.Is opportunistic
Hapana jamani. Deus Kibamba na yeye amependekeza ijadiliwe rasimu ya Warioba inamaana na yeye Deus ni UKAWA?

Mbona tunakuwa biased jamani!!
 
Ni aibu sana kwa kijana kama ZZK kushiriki ktk harakati za kuangamiza Vyama Vya Upinzani Tanzania kwa lengo LA kukibakisha CCM madarakani iendelee kutawala kiimla ktk nchi yetu
 
Back
Top Bottom