Msimamo wa Zitto Kabwe kuhusu Katiba mpya

MSIMAMO WA NDUGU ZITTO KABWE KUHUSU MCHAKATO WA KUANDIKA KATIBA MPYA

Jana tarehe 29 Julai, 2014 nimefanya mahojiano katika kipindi cha PowerBreakFast kinachorushwa na Clouds FM. Baadhi ya vyombo vya habari vimeandika mahojiano yale. Napenda nitoe ufafanuzi kidogo kuhusu msimamo wangu kuhusu mchakato wa Katiba.

Kwanza, Mimi sijawahi kuwa UKAWA wala kundi lolote lile katika Bunge Maalumu la Katiba isipokuwa kundi linalotaka maridhiano. Msimamo wangu kuhusu Muungano ni Serikali Tatu Zilizoboreshwa (S3z) ili kuwa na Muungano imara usio tegemezi wala egemezi kwa Washirika wake.

Pili, Mimi niliunga mkono ‘protest’ ya baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kupinga lugha za matusi na lugha za kibaguzi zilizokuwa zinaendelea ndani ya mkutano ule. Vilevile niliunga mkono kwamba Rasimu inayopaswa kujadiliwa ni Rasimu iliyotokana na Tume ya Marekebisho ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Sinde Warioba. Nasisitiza umuhimu wa kupata Katiba BORA itakayoimarisha DOLA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tatu, kwa hali ya sasa kuna mkwamo katika kupatikana kwa Katiba Bora. Mkwamo unaotokana na kutokuwepo kwa nia ya dhati ya kupata maridhiano ya pande zinazopingana. UKAWA hawataki mazungumzo na Viongozi wa Bunge la Katiba badala ya kujenga maridhiano kila siku wanawabeza UKAWA jambo ambalo kamwe haliwezi kujenga mwafaka. Ushauri wangu ni kuahirisha mchakato mzima wa kuandika Katiba mpaka mwaka 2016 baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Katiba ya sasa ifanyiwe marekebisho machache kama ifuatavyo;

i) Tume ya Uchaguzi ili iwe huru na ionekane kuwa huru, ikiwemo kuwaondoa watumishi wa Halmashauri za Wilaya, Miji na Majiji katika kusimamia uchaguzi

ii) Kuruhusu mgombea binafsi

iii) Kuondoa Mafuta na Gesi kama Jambo la Muungano ili Zanzibar ianze mara moja kusimamia kwa uhuru utafutaji wa Mafuta katika vitalu vilivyopo upande huo wa Muungano

Mkutano wa Bunge Maalumu utakaofanyika bila kuwepo kwa maridhiano utakuwa hauna maana yeyote na itakuwa ni sawa na kupoteza muda na fedha za walipa kodi ambazo zingeweza kununua madawa vijijini. Mimi binafsi sitahudhuria mkutano wa Bunge Maalumu kama makundi hasimu hayatakuwa yamefikia maridhiano.

Kabwe Zitto, MB/MBMK

sawa ila huna jipya, unataka uonekane mzuri kila upande na hilo ndio linalikumaliza.
 
Ni aibu sana kwa kijana kama ZZK kushiriki ktk harakati za kuangamiza Vyama Vya Upinzani Tanzania kwa lengo LA kukibakisha CCM madarakani iendelee kutawala kiimla ktk nchi yetu

Mkuu unahitaji opareshen ya akili kutatua tatzo ulilo nalo, kwan zito amekufanyaje? Au unalipwa sh ngapi kwa kumchafua? Cjui iman yako ila kama n ya mashariki ya kati jielimishe acha kukuriri
 
Naunga mkono msimamo wa zitto ni wa kizalendo zaidi. Kuendelea na bunge maalumu la katiba bila ukawa ni kuendekeza ufujaji wa pesa za walipa kodi bure, ambazo zingeweza kujenga madarasa na hata kupeleka dawa kwenye hospitali zetu!
 
Zitto yupi niyule alie pewa less name ccm ili anzishe chama au ni mpya kazaliwa
 
Kutokana na tamko lake hili kuna dalili kuwa ZZT anaomba suluhu kiaina kwa Chadema na UKAWA
 
Kwanza, Mimi sijawahi kuwa UKAWA wala kundi lolote lile katika Bunge Maalumu la Katiba isipokuwa kundi linalotaka maridhiano. Msimamo wangu kuhusu Muungano ni Serikali Tatu Zilizoboreshwa (S3z) ili kuwa na Muungano imara usio tegemezi wala egemezi kwa Washirika wake.

UKAWA inaundwa na wabunge wa Chadema ,NCCR na CUF , sasa wewe Zitto ni mbunge wa chama gani ? Au posho ndio zinakufanya uwe kinga ganzi kiasi hicho? Jipambanue rasmi sio posho unataka kwa jina la Chadema ila linapokuja suala la maamuzi ya msingi unajiondoa Chadema ......

Kwani katiba ya CDM inaitambua UKAWA?
 
Mara anasema yeye sio UKAWA mara ataingia na na UKAWA kutohudhuria Bunge , aeleweke vipi huyu Popo ?

Popo baba yako uliyemning'iniza juu ya mti
Safari inaendeleya
Tunawabayiza na kuwasilimisha
Kwa kuvuwa magamba
Kuvuwa gwanda
Na kuuvaa uzalendo
 
Connected dots....msimamo wa ACT ni serikali tatu zilizoboreshwa (sijui lini tumekuwa na s3 hadi tudai maboresho) na msimamo wa zzk pia ni s3 zilizoboteshwa
 
Hana jipya na kadhihirisha kuwa yeye ni ACT. Mapendekezo ya Serikali tatu zilizoboreshwa aliwahi2 kuyatoa akiwa Dom kwenye BMK na ACT nao walitoa msimamo huo wa ser3 zilizoboreshwa na msimamo huo kaurudia tena na hii inadhihirisha kuwa yeye ndiye kinara wa ACT.

Serikali zilizoboreshwa ni zipi wakati hazipo? Maboresho ya namna gani ziwe ni ndani ya BMK. UKAWA wanataka rasmu ya tume ijadiliwe na si vinginevyo ambayo ina mapendekezo ya ser3, maboresho yatafanyika wakati wa kuijadili rasmu. Huu ni usanii wa Zitto as msimamo wake ni wa ukawa na kwa aibu anasema hatoingia BMK kama ukawa hawataingia.

Swala la kuirisha mchakato liliisha tolewa mapendekezo na kamati kuu ya Chadema na mapendekezo kuhusu maboresho ya tume ya uchaguzi pia yalitolewa na kamati kuu ya cdm.
 
MSIMAMO WA NDUGU ZITTO KABWE KUHUSU MCHAKATO WA KUANDIKA KATIBA MPYA

Jana tarehe 29 Julai, 2014 nimefanya mahojiano katika kipindi cha PowerBreakFast kinachorushwa na Clouds FM. Baadhi ya vyombo vya habari vimeandika mahojiano yale. Napenda nitoe ufafanuzi kidogo kuhusu msimamo wangu kuhusu mchakato wa Katiba.

Kwanza, Mimi sijawahi kuwa UKAWA wala kundi lolote lile katika Bunge Maalumu la Katiba isipokuwa kundi linalotaka maridhiano. Msimamo wangu kuhusu Muungano ni Serikali Tatu Zilizoboreshwa (S3z) ili kuwa na Muungano imara usio tegemezi wala egemezi kwa Washirika wake.

Pili, Mimi niliunga mkono ‘protest’ ya baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kupinga lugha za matusi na lugha za kibaguzi zilizokuwa zinaendelea ndani ya mkutano ule. Vilevile niliunga mkono kwamba Rasimu inayopaswa kujadiliwa ni Rasimu iliyotokana na Tume ya Marekebisho ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Sinde Warioba. Nasisitiza umuhimu wa kupata Katiba BORA itakayoimarisha DOLA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tatu, kwa hali ya sasa kuna mkwamo katika kupatikana kwa Katiba Bora. Mkwamo unaotokana na kutokuwepo kwa nia ya dhati ya kupata maridhiano ya pande zinazopingana. UKAWA hawataki mazungumzo na Viongozi wa Bunge la Katiba badala ya kujenga maridhiano kila siku wanawabeza UKAWA jambo ambalo kamwe haliwezi kujenga mwafaka. Ushauri wangu ni kuahirisha mchakato mzima wa kuandika Katiba mpaka mwaka 2016 baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Katiba ya sasa ifanyiwe marekebisho machache kama ifuatavyo;

i) Tume ya Uchaguzi ili iwe huru na ionekane kuwa huru, ikiwemo kuwaondoa watumishi wa Halmashauri za Wilaya, Miji na Majiji katika kusimamia uchaguzi

ii) Kuruhusu mgombea binafsi

iii) Kuondoa Mafuta na Gesi kama Jambo la Muungano ili Zanzibar ianze mara moja kusimamia kwa uhuru utafutaji wa Mafuta katika vitalu vilivyopo upande huo wa Muungano

Mkutano wa Bunge Maalumu utakaofanyika bila kuwepo kwa maridhiano utakuwa hauna maana yeyote na itakuwa ni sawa na kupoteza muda na fedha za walipa kodi ambazo zingeweza kununua madawa vijijini. Mimi binafsi sitahudhuria mkutano wa Bunge Maalumu kama makundi hasimu hayatakuwa yamefikia maridhiano.

Kabwe Zitto, MB/MBMK
Nilikuwa nakuamini na kukuheshimu kwa hili wewe ni -------- na kigeugeu sana yaana hueleweki haupo UKAWA wala CCM hakika CHADEMA hawakukosea kukutimua you are so stupid yaani umenipandisha hasira ungekuwa jirani ningekulima makofi
 
Zitto anajua wazi kuwa hata wakirudi huko Bungeni,kitakachojadiliwa ni matusi kwa UKAWA tu hakuna kingine ndiyo maana ametoa tahadhari mapema.

Kazi tunayo watanzania.Tusipo lisimamia hili limekula kwetu.
 
Msimamo upi sasa hapo kwamba Zitto ni Popo maana yuko kote kote ......Zitto ni historia
Usischokielewa nini!!! hats asiyejua kusoma na kuandika ukimsomea anakuelewa,wewe kama sio SHIRIMA basi MASAWE.
 
Mkuu hebu nionyesha aliposema maneno hayo kwenye hilo tamko lake.

Kimsingi anakubaliana na Madai ya UKAWA.
Hiki ndio cha msingi ambacho Mpaka huyu mnafik anakubaliana nacho...
 
Back
Top Bottom