Msimamo wa Zitto Kabwe kuhusu Katiba mpya

Msimamo wa Zitto Kabwe kuhusu Katiba mpya

UKAWA inaundwa na wabunge wa Chadema ,NCCR na CUF , sasa wewe Zitto ni mbunge wa chama gani ? Au posho ndio zinakufanya uwe kinga ganzi kiasi hicho? Jipambanue rasmi sio posho unataka kwa jina la Chadema ila linapokuja suala la maamuzi ya msingi unajiondoa Chadema ......[/QUOTE]

Nilichoelewa katika msimamo wa Zito yeye yupo huru, haongozwi na msimamo ya vyama wala makundi. Mimi naamini kwamba katiba bora itapatikana pale wajumbe wote watakapojitambua kama wapo pale kuandika katiba ya watanzania, sikatiba ya vyama vyao walivyotoka wala makundi yao. Ndugu yangu misimamo ya vyama ndiyo iliyotufikisha hapa unazani kama wajumbe wa ccm wangekuwa huru bila ya kubanwa na chama chao tungefika hapa? Tuwaache wajumbe wawe huru wajadili katiba ya watanzania.
 
Chadema wanatumia platform ya UKAWA kupambana na Zitto wanazidi kupoteza mweleko UKAWA wanafuata maelekezo kutoka UFIPA hii katiba za ya Mbowe wala Lema muwe makini nyie wapambe wa Mbowe mnaotumwa kuja kufungua uzi JF.

Mnaliambukiza taifa tabia mbaya sana ya uongo na unafiki,
jipime na uthubutu kutuambia tumepata medali ngapi kwenye mashindano ya jumuiya ya madola?!!!!!

Kolimba:- ccm imepoteza dira

dira imepotea moja kwa moja, hatuoni jitihada ya kuirejea wala kujipanga upya.
 
Viongozi wa UKAWA wamemuonya Mh.Zitto akae kimya asizungumzie mambo ya UKAWA kwa kuwa hayamhusu.

Kauli hiyo imekuja baada ya Zitto kutoa kauli kuwa hana uhakika kama umoja huo utadumu mpaka uchaguzi 2015.

Zitto ametakiwa aendelee na ubinafsi wake awaache UKAWA wawapiganie wananchi.

Source: Mtanzania.

My Take: Zitto acha chokochoko,huna credibility ya kuwanyooshea Ukawa kidole,kwani wewe ni mbinafsi.
KILA MWENYE AKILI NA atalidhihirisha hilo kwa kuonyesha dharau zake kwa UKAWA. hakuna hata mmoja ndani ya UKAWA mwenye uwezo wa kiakili,kimantiki,kielimu,kiadilifu wala kizalendo wa kumkaripia ZZK. he will always prevail dhidi ya makundi ya wajinga kama BAVICHA na dhidi ya wachumia tumbo na wenye uchu wa madaraka kama UKAWA
 
Zitto hana tena credibility ya kuongelea masuala yanayohusu mtanzania mnyonge!! Yeye akae kimya afanye harakati zake za kuhakikisha mabwana zake wanabaki madarakani.

Wanyonge tunasemewa na UKAWA kupitia Bunge la katiba. Zitto kaa kimya huna maana kwa sasa!!
huna mamlaka ya kumnyamizisha zitto, ana haki kikatiba ya kutoa maoni yake kama raia!
 
Mkuu umesema vema hawa ukawa lazima waelewe kuwa rasimu ya katiba ina mambo mengi siyo serikali tatu tu ni vema waache bangi wajue kuwa yapo mambo mengi yanayowahusu watanzania wasitusumbue.

Ni lazima nyie watu muelewe siyo kuropoka tuu kama mmekatwa vichwa uwezi kujadili kipengele chochote kwenye rasimu bila kuelewa unajadili serekali ngapi!! Lazima muelewe kwanza hilo!!
 
Eti ndo mpewe nchi? Thubutu!! Si mtamnyonga kila mtu atakayewakosoa! Nyie endeleeni tu kupaza sauti, nchi hamtapewa. Hakuna mtanzania ambaye yuko tayari kuongozwa na Matahira Chadema.
mkuu, wasamehe wameteleza, kila mwanadamu ana haki ya kutoa maoni yake!
 
Cdm ya mwaka 2010 inatofauti kubwa sana na hii iliyopo sasa coz tuliowengi tumeshaiona kuwa haina maana tena
Usiseme hayuko mtanzania sema mafisadi na wezi hawapo tayari.
Ila wanyonge ambao wameibiwa sana na nyie wapo tayari sana 2010 hukuona pamoja na uchakachuaji CHADEMA tu ilipata kura 2.6m subiri mwakani utaisomanamba
 
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), kwa mara ya kwanza ameibuka na kupingana na harakati za Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Zitto amesema hana uhakika wala hauamini Ukawa kama utakuwa umoja endelevu hadi kufikia Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, kwa sababu si mara ya kwanza vyama vya upinzani kuungana na kugawanyika.
Mbali ya kutokuwa na imani na umoja huo, pia ameitaka Serikali kusitisha mchakato wa Katiba Mpya hadi uchaguzi mkuu utakapomalizika.

Alisema ni vema mchakato huo ukasitishwa kwa sasa, kwani inaonekana wajumbe wa Bunge hilo wanafuja fedha za umma.

Zitto alitoa kauli hiyo jana, wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa na kituo cha redio cha Clouds cha jijini Dar es Salaam.

Alisema Watanzania wanakabiliwa na changamoto nyingi na si Katiba pekee.

Alisema siku zote Watanzania wamekuwa wakipenda kuwa na upinzani imara ambao watu wanaweka tofauti zao pembeni na kuungana dhidi ya chama ambacho kinaongoza, lakini haoni kama Ukawa utaendelea hadi kufikia kipindi cha Uchaguzi Mkuu.

Alisema hatua ya kusimama kwenye ajenda moja ya Katiba haitausaidia umoja huo, kwani kipindi cha uchaguzi mkuu kinakuwa na ajenda nyingi.

Alisema wananchi watapenda kusikia masuala ya kushughulikia rushwa, matumizi ya rasilimali, maji, umeme, afya na barabara.

“Mambo haya ndiyo yatakayowafanya wananchi waamue namna gani watakabidhi dhamana ya uongozi, si suala la Katiba pekee,” alisema Zitto.

Alisema tusijitoe ufahamu kwa kudhani kwamba hii ndio mara ya kwanza kwa upinzani kuungana.

“Kulikuwa na Kamati ya Mabadiliko ya Katiba (KAMAKA) pia katika chaguzi za mwaka 1995, mwaka 2000 wapinzani waliungana vilevile, lakini kila inapokaribia uchaguzi wamekuwa hawaelewani kwa kuwa kila mtu anataka chama chake kipeperushe bendera.

“Lakini kama Ukawa wataweza kuweka ajenda yao mpaka mwisho itakuwa jambo jema kwa wananchi wenyewe. Kwa sababu nchini kwetu tatizo kubwa ni usimamizi na uwajibikaji, kama ajenda itachukua nafasi naamini hali haitakuwa mbaya, lakini bado siamini na sina uhakika kama umoja huu ni endelevu kwa namna ambavyo tunaona, ni umoja ambao unatokana na matakwa ya sasa ya Katiba, wameungana kwa sababu ya serikali tatu, lakini aina gani ya serikali bado hili linaweza kuwagawa,” alisema.

… mchakato wa Katiba Mpya usitishwe
Akitolea ufafanuzi hoja yake ya kusitisha mchakato wa Katiba Mpya, Zitto alisema ni vyema serikali ikausitisha ili kunusuru fedha za umma zisiteketee.

Alisema fedha hizo zinastahili kutumika kununua madawa, kuendeleza miradi ya maji na kusomesha Watanzania, hivyo hakuna sababu fedha hizo kutumika kwa ajili ya kupiga porojo na kutukanana ndani ya Bunge.

“Nashauri tuahirishe mchakato huu mpaka baada ya uchaguzi mkuu mwaka kesho, ndipo hapo tuwe na mamlaka ya kujadili mchakato huu na kumaliza.

“Pia uchaguzi unaweza kuchekecha na ukaondoa baadhi ya watu ambao ni vikwazo katika mchakato kwa sababu uchaguzi hauna muamala, mtu ambaye alikuwa mbunge anaweza kuondolewa,” alisema.

Aidha, alisema kabla ya kwenda kwenye uchaguzi mkuu, Katiba ya sasa inatakiwa kurekebishwa baadhi ya maeneo ambayo ni vikwazo, kama vile Tume huru ya uchaguzi, kipengele cha wagombea binafsi kiwekwe na maeneo ambayo Zanzibar wamekuwa wakiyahitaji katika Katiba mpya, kwa mfano suala la mafuta na gesi yawekwe.

Alisema hakuna sababu ya kugawa nchi na kutumia rasilimali zilizopo kwa kufanya kazi ambayo haina matunda.

…amtetea January
Katika hatua nyingine, Zitto, ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, alisema amesikitishwa na mashambulizi yanayoelekezwa kwa Mbunge wa Bumbuli (CCM), Januari Makamba, baada ya kutangaza nia ya kuwani urais mwaka 2015.

Alisema kila kijana anapojitokeza kwa ajili ya kutaka kushiriki katika mamlaka za nchi, hasa katika nafasi kama hiyo ya urais, kumekuwa na mashambulizi makubwa dhidi yake.

“Ni hatua ambayo sio nzuri kwa sababu kwa mujibu wa takwimu, idadi ya watu asilimia 72 wapo chini ya miaka 30, asilimia 65 ya wapiga kura ni vijana wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 40, hivyo vijana wana haki ya kushiriki katika uongozi wa nchi, tufahamu changamoto za maendeleo ya nchi yetu zinahitaji uongozi mpya wa kizazi kipya.

“Ni dhahiri neno ujana si sifa, lakini neno uzee pia si sifa, hivyo tunatakiwa kuwapima vijana kwa sifa zilizopo, kama vile za kikatiba na zile za ziada, badala ya kusema vijana hawajakomaa… nilisikitika sana na mashambulizi ambayo yalielekezwa dhidi ya Makamba, natoa wito kwamba tuache, kwani wenye uamuzi wa mwisho ni wananchi.

“Mtu akigombea na kama akitoa sera zake vizuri wananchi wakamwelewa, akichaguliwa ni wananchi wameamua, hakuna mtu mwenye mamlaka kuwa fulani ni kijana, nadhani lazima tubadilishe uongozi na watu wajue nchi hii ni ya vijana, hatusemi wazee hawawezi ila wao wabaki kuwa washauri kama wao walivyokuwa vijana katika kipindi cha Nyerere nao walikuwa na miaka 40. Hivyo kuna haja ya kuweza kufikia hapo, changamoto za nchi ni kubwa, kuna haja ya aina mpya ya uongozi na mimi naamini aina hiyo itatoka kwa viongozi vijana,” alisema.

Hiyo ni mara ya kwanza kwa Zitto, ambaye yuko ndani ya Chadema kwa sababu za kisheria, kuibuka na kuuzungumzia Ukawa.

Mwanasiasa huyo kijana amekuwa kimya kwa muda mrefu, hata kwenye harakati za Ukawa amekuwa aghalabu kuonekana, hali ambayo imekuwa ikiibua maswali yuko upande gani katika mchakato huu wa Katiba Mpya.

Kauli hii ya Zitto inaweza kuibua fikra mpya kwa baadhi ya watu ambao wamekuwa na imani kubwa na umoja huo unaoviunganisha baadhi ya vyama vya siasa nchini.

Makamba aufananisha na Paka
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba, ameufananisha Ukawa kuwa ni sawa na paka, kwa kuwa tambo za wajumbe wa kundi hilo zitakwisha mwaka 2015 katika kuusaka urais.

Makamba alitoa kauli hiyo alipozungumza na MTANZANIA Jumatano katika mahojiano maalumu yaliyofanyika nyumbani kwake Tegeta, jijini Dar es Salaam.

Alisema Ukawa ni umoja ulioundwa kwa lengo la kuwahadaa wananchi katika kipindi hiki cha mchakato wa Katiba Mpya, lakini hautakuwapo mwaka 2015.

“Mimi ni mwana CCM, nasema kwa hali hii tutawachapa kweli wapinzani katika uchaguzi ujao… kwa sababu huu Ukawa ni umoja wa paka, paka walikaa siku moja wakasema jamani tuungane, wakachukua kamba wakajifunga mikia ili wawe wamoja, lakini alipotokea panya wote walisambaratika, kwa sababu kila mmoja alikuwa anamtaka panya.

“Kwa kuwa kila chama kinataka kuwa na rais, nina hakika huu muungano wao hautaendelea, watasambaratika kama walivyosambaratika paka. Wakati wa urais hakuna Ukawa!” alisema.

Alisema hata Ukawa wasiporudi ndani ya Bunge Maalumu la Katiba na kukwamisha upatikanaji wa Katiba Mpya, Uchaguzi Mkuu utafanyika kwa kutumia Katiba iliyopo.

“Nakumbuka vyama vya upinzani wakati mimi nikiwa Katibu Mkuu moja ya hoja walizokuwa waking’ang’ania ni Katiba Mpya na Dk. Slaa alikuwa akiwaahidi Watanzania kuwa wakimpatia nchi atawapatia Katiba Mpya… sasa Rais Kikwete amesema uchaguzi ujao ufanyike na Katiba Mpya, kwanini wanatoka Bungeni? Mnataka nini? Rudini Katiba ipatikane kama kweli mna nia ya dhati!

“Usilalamikie wingi wa CCM kwa sababu ndio uzuri wa kushinda. Hata wao wangekuwa wengi wangefanya hivi ili sera za chama zipite, warudi bungeni katiba mpya ipatikane. Wasikimbie hoja,” alisema.

Aidha alizungumzia mfumo wa Serikali tatu uliopendekezwa ndani ya rasimu ya pili ya Katiba na kusema huo ni mzigo kwa Watanzania.
chanzo:Mtanzania
 
mnajua babu yangu, mzee Mperela once told me " it's difficult to talk with somebody who didn't graduate University". Zitto katoa msimamo wake, yeye kama mbunge wa Kigoma, aliye ingia bungeni kwa kura za wananchi. Kusema ukweli kwenye dunia ya sasa ina tafsiliwa kama umbea, unafiki na usaliti. Ukiwa mnyonge kufwata wakubwa wanavyo taka basi wewe uta kuwa ndio kiongozi safi kama Naibu wa wizara ya fedha na uchumi. Zitto kafukuzwa, sawa na ame omba kuwa na mgombea huru wa urais, hapo patamu, nataka kumwona Zitto, Salim Ahmed Salim wakisimama kama wagombea binafsi.
 
Mkuu wewe kweli umedata, yani umeamua kuileta mwenyewe? Vp jana hukuridhika kuichqngia hapa?
 
Back
Top Bottom