Msimamo Rasmi: Wakati Umefika kwa Freeman Mbowe (MB) Kujiuzulu; na Sekretariati Yake...


Ndiyo, wanachama wa CHADEMA ndiyo wenye haki na uwezo wa kuamua nani awe mwenyekiti wao na kwa muda gani. Kwa mihula au milele. Hilo ni juu yao.

Lakini pia, CHADEMA kama chama cha umma, tena kinachopewa ruzuku na serikali, ruzuku hiyo ambayo kimsingi ni pesa za walipa kodi, basi pia ni haki ya kila Mtanzania kuweza kujieleza na kutoa maoni yake juu ya yale yanayoendelea kwenye chama hicho.

Sidhani kuwa, kwa Mtanzania yeyote yule, kutoa maoni yake juu ya uongozi wa chama cha umma kilicho cha kisiasa, hata kama yeye si mwanachama mshika kadi wa chama hicho, ni kukipangia au kukiamrisha chama hicho kifanye hiki au kile.

Hata mimi binafsi, kwa maoni yangu, naona kabisa wakati wa Mbowe kujiuzulu ulishafika siku nyingi sana.

Ni maoni yangu tu kama Mtanzania. Katiba inanipa haki ya kuwa na maoni kama hayo.

Uongo?
 
Unaruhusiwa kuwa na maoni, lakini, itakuwa vipi kama wanachama wa CHADEMA wanaona Mbowe anawaongoza vizuri sana, halafu wanachama wa CCM hawapendi Mbowe anavyowaongoza vizuri sana CHADEMA, wakaanza kuleta zengwe aondolewe ili CHADEMA kisiwe na uongozi mzuri?

Hapo ndipo umuhimu wa wanachama kuwa na maamuzi juu ya uongozi wao.

Watu wasio wanachama wanaruhusiwa kuwa na maoni, lakini hii ngoma si yao.
 
Mbowe hafai hata kuongoza kijiji katika awamu hii inayohitaji akili kubwa sana na Maarifa mengi huku ukiweka Ubinafsi pembeni.

Mtu yeyeote mbinafsi awamu hii hawezi kuwa kiongozi kamwe.

Mbowe ni Mbinafsi ,Mkabila,Mdini, Bepari ,Beberu mkubwa ,Mhuni ,Mkwepa kodi na fisadi Mla ruzuku kamwe hawezi kuungwa mkono na mtu yeyote safi na mwenye madili.

Mbowe alipaswa aweke mbali ukabila,na ubinafsi wote na kila aina ya sanaa kisha Amshauri vizuri Komredi Tundu Lisu Profesa wa kweli wa sheria Duniani na kukaa mezani na kuweka maridhiano na Ikulu ya Tanzania chini ya Mh.Rais kuachana na siasa za kuchafuana na kutukana na kuanza siasa za hoja na kuweka mbele maslahi ya nchi.
Baada ya hapo wamuombe Rais pawe na maridhiano ya kitaifa kama alivyoandika barua Mbowe. Then Mbowe aachie madaraka na kumkabidhi Chama Tundu Lisu. Katibu Mkuu awe ni Juma Mwalimu.Makamu wa Mwenyekiti awe ni John Mnyika .
Mwenezi awe ni John Heche, Msemaji wa Chama awe ni Msigwa.
Hivi hapo nani anguza Chama ??
Kwa nini tunadanganyana kwa kusikiliza Porojo za Mbowe?
Karne hii msomi gani atakubali kuongozwa na Mbowe asiye na uteuzi wowote kisiasa na kiutawala ? Angekua Mbowe ni Rais watu wangemvumilia kwa kulinda Maslahi yao na usalama wao kijamii lakini kwa Chama cha upinzani haiwezekani msomi kubaki Chadema chini ya udikteta wa Mbowe.
Ni bora mtu akimbilie kwenye nafasi ya udikteta utakaompa kula vizuri na familia yake.Chama ni cha Mbowe na genge lake manasubiri nini huko mpaka muitwe mamluki na wasaliti.

Nitoe wito kwa Wasomi na wote wenye Uwezo wa kupata uteuzi wowote wenye heshima na maslahi bora wamwachie Mbowe Chama Chake wajiunge na CCM na kuweza kupata maisha bora yenye heshima na amani mana ndani ya Chadema ya Mbowe hakuna ndoto ya mtu itakayotimia zaidi ya kuitwa majina mabaya ya usaliti na mamluki.
Chadema sio mama wala baba yenu.
Hongera sana Dk. Mashinji umeona Mbali. Najua unakipenda Chama Chako cha Chadema lakini unalipenda zaidi Taifa letu na familia yako na Kabila lako. Umeona Mbali zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kwa ‘zengwe’ unamaanisha kuingilia mambo yao ya ndani ya chama? Kama ni hilo, hapana. Hilo si vyema.

Hapo ndipo umuhimu wa wanachama kuwa na maamuzi juu ya uongozi wao.

Watu wasio wanachama wanaruhusiwa kuwa na maoni, lakini hii ngoma si yao.

Naona umekubaliana nami! 👍🏾
 
Hiyo akili kubwa ni ya kuipindua nchi? Ulitaka afanyeje sasa? mnatafuta kutukanwa tu na kuharibu reputaion za watu
 

..aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Prof.Safari ni Msukuma.

..aliyekuwa Katibu Mkuu Dr.Mashinji ni Msukuma.

..aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu John Mnyika ni Msukuma.

..sasa kusema Mbowe ni mkabila mnakuwa hamumtendei haki.
 
..aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Prof.Safari ni Msukuma.

..aliyekuwa Katibu Mkuu Dr.Mashinji ni Msukuma.

..aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu John Mnyika ni Msukuma.

..sasa kusema Mbowe ni mkabila mnakuwa hamumtendei haki.

Hmm....Prof. Safari na Mnyika ni Wasukuma kweli?
 
..nimemsikia Prof kwa kinywa chake akisema yeye ni Msukuma.

..John Mnyika pia amedai kwao ni Misungwi. Na majuzi alikuwa huko kumzika baba yake mdogo.

Hmmm

Safari mbona ni jina la watu wa Kaskazini...

Na Mnyika naye nina shaka...
 
Kwa haki na kwa kulinda heshima ya chama, Mbowe hakutakiwa kugombea uenyekiti wa chama, kwa maana nyakati zilizopo zimebadirika zinahitaji mbinu nyingine ili kuuvusha upinzani kwenye huu mkwamo uliopo.
Kweli kabisa,ilibidi apewe Cecil Mwambe,hii ingekuwa habari njema sana,kwani mpaka sasa angekuwa ameunga mkono juhudi na nchi ingepiga hatua kubwa kimaendeleo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hmmm

Safari mbona ni jina la watu wa Kaskazini...

Na Mnyika naye nina shaka...

..wapo wakina Safari toka kabila la Wairaqw / Wambulu.


..lakini mimi nimemsikia Prof.Safari akisema yeye ni Msukuma. Nitatafuta video clip nikuletee usikie.


..kuhusu John Mnyika na asili yake ya Usukuma sikiliza video clip hapo chini kuanzia dakika 2:50.

NB.

..hata jina Chadema kuna wanaofahamu historia ya kuasisiwa kwa chama wanadai lilipendekezwa na Mzee wa Kisukuma toka Shinyanga ambaye ni mmoja wa waasisi wa chama.

 
Kwa ‘zengwe’ unamaanisha kuingilia mambo yao ya ndani ya chama? Kama ni hilo, hapana. Hilo si vyema.



Naona umekubaliana nami!
Unaruhusiwa kuwa na maoni, hiyo ni haki yako ya kikatiba.

Ila ujianza kushikia bango uongozi wa chama ambacho si tawala na si chako, unawe,a kuambiwa umetumwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I am very much worried, some 🧠 are frozen.
How can you celebrate such catastrophic and failure? 99% of the members are complaining!
Is it because they don't have ways to act against it?
75% of your members of Parliament are not happy,
Come on folks you will pay the price of the people tears!
 
Mzee mwanakijiji umekuwa ukitoa ushauri mzuri kila mara kwa hiki chama mfu.wenye chama Chao wameziba macho na masikio hawaishi kejeli na matusi.
Sikio la kufa halisikii dawa!
 
Kwa haki na kwa kulinda heshima ya chama, Mbowe hakutakiwa kugombea uenyekiti wa chama, kwa maana nyakati zilizopo zimebadirika zinahitaji mbinu nyingine ili kuuvusha upinzani kwenye huu mkwamo uliopo.
Sio kwamba Kuna watu walimchukulia fomu na yeye akakubali kwa kuzingatia idadi(sauti) ya Watu waliomshawishi?
 
Nikajua utatoa mifano ya Kenya,Uganda, Rwanda,Burundi,Zambia unatuletea habari za Uingereza,Korea na wapi sijui..bro siasa za ni afrika zina njia zake na kwa bahati nzuri tunajua kwann mnapiga kelele mbowe aondoke ni kwa sababu jamaa ni mgumu na ni Hatar sana kwenu so hatushangai..kwa roho mbaya hujataka kuonesha hata machache mazuri ambayo Mbowe kayafanya katika kipindi chake lengo ni kutuaminisha kwamba jamaa hajafanya kitu katika kipindi chake...waTanzania Wa aina hiyo walishaisha boss..tunaona,tunajua,tunaelewa na tunakumbuka so kakae andaa andiko lingine urudi huu ni uchafu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…