Msimamo Rasmi: Wakati Umefika kwa Freeman Mbowe (MB) Kujiuzulu; na Sekretariati Yake...

Yaani, sasa ni "takakata" wakati alikuwa ni Katibu Mkuu mtendaji wa chama? siyo wadhifa mdogo huo...

Huenda ulikuwa hufuatilii ukweli kuhusu huyo Mashinji, yeye alikuwa mzigo kama mizigo mingine. Kwenye post yako namba moja kuna sehemu nakubaliana na ww baadhi, hasa hapo kuwa Mbowe kafikia mwisho. Ila sioni ni kwa vipi unaweza kumtenganisha Magufuli na hizi siasa za kihuni zinazoendelea dhidi ya wapinzani wa ukweli wa nchi hii.

Ukweli ni kuwa Mbowe kafikia mwisho wa uwezo wake, na hakustahili kugombea uwenyekiti wa cdm, bila kujali cdm ingeshinda uchaguzi, au ikiwa imepoteza. Sijawahi kuamini kiongozi kuongoza zaidi ya miaka 10, na bado akabakia na ubora wake. Mbowe Kawa mwenyekiti wa cdm zaidi ya miaka 15, na kwa uchaguzi huu uliopita atakaa madarakani mpaka 20yrs. Sitegemei lolote jipya toka kwa Mbowe. Huu uhamaji na kushindwa uchaguzi siupi nafasi sana kuwa ni udhaifu wa uongozi wa Mbowe, kwani mazingira ya siasa ya sasa yako wazi kuwa rais aliyeko, anatumia madaraka yake vibaya kuhujumu upinzani. Hata kama mazingira ya siasa nchi yangekuwa mazuri au ya kuridhisha, ukweli ni kuwa Mbowe kafikia tamati ya uwezo wake.
 
mbele ya ruzuku mbowe humwambii kitu, chama limekuwa jumba bovu sasa,muda wote linadondoka na kuwaponda wote waliomo.Sijui kama watasalimika.
 
Kuna watu huwa wanakua wakali sana pindi linapokuja suala la kujadili nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA. Hii hali ikiendelea chama kitazidi kupukutika watu wenye msaada na ushawishi...
Mbowe ni Kiongozi wa kimila mnasahau hilo, ni Chief wa Wamachame, hivyo Wamachame hawawezi kukubali kwani hawaoni jinsi muonavyo ninyi, na ndo maana wanakuwa emotional linapokuja swala la kumwajibisha Mbowe, wanaona the clan is under attack hivyo wanatetea, ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah kweli never say never.. Miaka ya 2005 ungeambiwa iko siku chadema kitakuwa sawa na vyama kama SAU, UDP nk kwa maana ya chama bila mbunge hata mmoja ungebisha hadi miti ikakauka ila leo hii tena sio ndoto ila ni uhalisia.. Kuanzia Oct 2020 Mbowe atakuwa sawa na Hashim Rungwe
 
Sasa unanilazimsha niwe kabila ambalo siyo?Mimi ni Muha mzaliwa wa Kibondo kijiji cha kifura!
Naamini Mbowe ni mtu sahihi zaidi kuiongoza CDM!Iko hivyo mpaka nitakavyoona vinginevyo!

Hakuna mahali nilipokulazimisha chochote, isitoshe mambo ya ,,kabila“ wewe ndo umeleta.
 
Kuna TLP,CUF,UDP nk hamvioni mnaona CDM mtatapatapa sana,haijuzulu wala nini,tena tunabadilisha katiba awe wa kudumu tuone sasa,wachumia tumbo tu ninyi.
Kwa haki na kwa kulinda heshima ya chama, Mbowe hakutakiwa kugombea uenyekiti wa chama, kwa maana nyakati zilizopo zimebadirika zinahitaji mbinu nyingine ili kuuvusha upinzani kwenye huu mkwamo uliopo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Hili ni swali ambalo linahitaji jibu. Kwenye nchi na vyama vya kidemokrasia mojawapo ya kanuni muhimu ni ile inayotaka viongozi wa juu wa chama kuwajibika mara moja pale vyama vyao vinaposhindwa uchaguzi. Hili ni kweli hasa pale kiongozi anapowekeza mkakati mzito na kuwaaminisha wanachama na mashabiki wake kuwa mkakati au msimamo waliochukua utakipa chama ushindi mkubwa. Mkakati au msimamo huo unaposhindwa viongozi wale hawatakiwi kuendelea na madaraka na badala yake hutangaza kuachia ngazi ili kutoa nafasi kwa viongozi wengine kuja na msimamo na mkakati mwingine ambao ni tofauti na ule mwingine. Nitatoa mifano michache.

Uingereza: Jeremy Corbyn
Bw. Corbyn alikuwa ni kiongozi wa chama cha Labour cha Uingereza akiwa kinyume kimisimamo na mwelekeo na uongozi wa Boris Johnson wa chama cha Conservatives. Katika mjadala wa kuondoka ama kuondoka au kubakia ndani ya Jumuiya ya Ulaya Corbyn aliongoza harakati za kubakia kwa muda mrefu. Alibeza misimamo na mipango ya chama cha Conservatives na hata kutaka uchaguzi mwingine ufanyike kuona wananchi wanasemaje.

Kufuatia matokeo ya uchaguzi mwezi Disemba mwaka jana ambayo yaliona Bw. Johnson akishinda na kupata wabunge wengi zaidi Corbyn alijua kuwa msimamo na mkakati wake umekataliwa na wananchi. Japo yeye mwenyewe alichaguliwa katika jimbo lake lakini alikiri kuwa hatokuwa tayari kukiongoza chama hicho kuelekea kampeni nyingine ya uchaguzi.

India: Rahul Gandhi
Licha ya kuwa na jina kubwa katika siasa za India, kiongozi wa chama cha Congress Gandhi alitarajiwa kubeba chama hicho ambacho familia na ukoo wake ulikuwa kama umekihodhi katika ngazi za juu kwa karibu nusu karne. Hata hivyo, baada ya kushindwa chaguzi za April na Mei mwaka jana, Gandhi alijikuta hana namna nyingine isipokuwa kukubali kuwa yeye hakuwa tena mtu sahihi wa kukiongoza chama hicho.

Katika kauli yake ya kujiuzulu Gandhi alisema "kuwajibika ni muhimu sana katika kuhakikisha chama chetu kinakua huko mbeleni. Ni kwa sababu hiyo nimeamua kujiuzulu nafasi yangu kama Rais wa chama". Hii haina maana hakuwa na mchango, au kuwa alikuwa kiongozi mbaya. Alichofanya ni somo la kawaida la demokrasia; kiongozi akishndwa kuongoza chama chake kushinda uchaguzi anatakiwa kujiuzulu siyo kutafuta udhuru.

Korea Kusini: Hoong Joon Pyo (kiongozi wa upinzani)
Mwaka 2018 chama cha Liberty Korea Party chini ya uongozi wa Bw. Pyo kilijikuta kinabwagwa vibaya kwenye uchaguzi mkuu kiasi cha kumfanya kiongozi huyo kukubali kubeba lawama zote za kushindwa huko na kuamua kujiuzulu.

Taiwan: Mwenyekiti Wu Den yii wa KMT
Baada ya kubwagwa vibaya kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka Huu uongozi mzima wa chama cha KMT uliandika barua zake kujiuzulu ili kuwajibikwa kwa matokeo mabaya ya uchaguzi huo. Mwenyekiti Wu Den yii (cheo sawa na cha Mbowe) akiongozi Sekretariati yake waliandika barua ya kujiuzulu mbele ya Kamati Kuu. Wu alikuwa ameapa kuwa mkakati wake wa uchaguzi utakipatia chama hicho angalau nusu ya viti vyote vya wabunge. Hilo halikutokea! na Walishindwa kwenye Urais kwa tofauti ya asilimia 20 ya kura!

Afrika Kusini: Mmusi Maimane wa DA
Kiongozi huyo alikuwa ni moto moto na alijaribu sana kukivutia chama cha DA kwa weusi wa Afrika ya Kusini. Hata hivyo, juhudi zake hizo hazikuweza kukifanya chama hicho kufanya vizuri zaidi kulinganisha na ANC ambayo ilikuwa inakumbwa na kashfa nyingi. Licha ya kashfa hizo chama cha DA hakikuweza kuvutia weusi wengi. Maimane aliamua kujiuzulu baada ya mikakati na mbingu zake zote kushindwa.

Mifano yote hiyo michache na ipo mingine mingi inatuonesha mambo mengi. Kubwa ni kuwa kiongozi wa chama cha siasa anaposhindwa kutimiza ndoto aliyowahidi wananchi wake yampasa yeye ajiuzulu na kama katika maamuzi hayo aliungwa mkono na viongozi wengine wa juu nao pia yawapasa kujiuzulu.

Mbowe na CHADEMA
Katika siasa zetu za Tanzania inasikitisha kuwa mikakati mbalimbali iliyobuniwa na MBowe na kutekelezwa na harakati mbalimbali imeonesha kufeli zaidi. Watu wamebakia kujivunia mavazi na rangi za magari na wingi wa misemo yenye kuvutia. Wakati umefika kwa Mbowe kujipima kama hawa viongozi wengine na kuona kama kweli anastahili kuiongoza CHADEMA kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 baada ya kukiongoza chama hicho katika kufanya maamuzi mabovu, ya hatari na yenye kukidhoofisha zaidi.

Ni Tanzania tu ambapo kiongozi wa upinzani anakiongoza chama katika kushindwa katika kila uchaguzi na bado anatarajiwa kuendelea kukiongozi miaka mingine. Ni Tanzania tu kiongozi wa upinzani anahukumiwa siyo kwa kuwezesha kuingia madarakani bali kwa kuangalia ni kura ngapi zimeongezeka kwenye mahesabu!

Binafsi naamini kuondoka kwa Kashinji leo kuwe ndio msumari wa mwisho wa kuonesha ubaya, na upotofu wa maamuzi ya Mbowe kama Mwenyekiti. Suala hili ni suala la kidemokrasia na siyo suala la binafsi. Na ninaamini Sekretariati nzima ya CHADEMA isijiuzulu na kutoa nafasi kwa wanachama wengine kushika hatamu za uongozi wa chama kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020. Kuendelea kujificha kwenye kumlaumu Magufuli na CCM ni kujaribu kutafuta visingizio visivyoisha. Tangu 2005 hadi leo hii bado upinzani chini ya MBowe haujapata dawa sawasawa ya kukabiliana na CCM.

Kuukataa ukweli huu ni sawasawa na mtu anayejifumba macho kujificha na mwanga wa tochi unaommulika. Ni kweli anaweza asiuone mwanga huo lakini haina maana kwenye mwanga huo yeye haonekani.

Kudai ati "CCM iweke usawa" ati "tunapambana na dola" na kuwa "Magufuli ameminya demokrasia" ni visingizio vilivyopitwa na wakati na ambayo havina msingi katika uelewa wa siasa za kawaida za upinzani mahali popote duniani. Wale wapinzani wanaotaka chama tawala kiwatengenezee mazuria, kuwapambia maua na kuwaimbia nyimbo za kuwatia moyo hawafai hata chembe kuendelea kuuongoza upinzani huo.

Ni wakati wa Ndg. Freeman Mbowe kuamua kujiuzulu mara moja na siyo kutafuta udhuru na visingizio vya kushindwa. Afuate mfuano wa viongozi wengine ambao waliweza kuuangalia ukweli wa kushindwa kwao na kuusalimu kwa kujiuzulu.

Labda, Labda, UPINZANI wa kweli unaweza kuibuka.

MM. Mwanakijiji
Sipotez muda kusoma huu utumbo, ulitaka cdm ifanye makosa ya nccr na tlp? Shame
 
Hakuna mahali nilipokulazimisha chochote, isitoshe mambo ya ,,kabila“ wewe ndo umeleta.
Nimeleta mimi au wewe unayeniforce kuwa ni mtu wa kaskazini?Propaganda zenu zimefeli,mnashindwa kuamini Mbowe anaungwa mkono ndani na nje ya kanda anakotoka!
 
Hilo genge lenu la kigaidi linalotumia mabavu ya dola kutawala mwisho wake umefika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeleta mimi au wewe unayeniforce kuwa ni mtu wa kaskazini?Propaganda zenu zimefeli,mnashindwa kuamini Mbowe anaungwa mkono ndani na nje ya kanda anakotoka!

Mbowe anaungwa mkono na miguu Machame + Marangu tu, Rombo hawataki hata kumsikia hata Mbunge wa Rombo Selasini ataimwaga chadema muda si mrefu nimesikia.
 
Hahahaaa,huko ndio kuishiwa hoja!Angalia wajumbe wa mkutano mkuu wa CDM na angalia alipitishwa kwa asilimia ngapi!Hizo ulizoandik ni porojo tu kama porojo nyingine!
Nikiwakilisha vijana wa kibondo,twasema twende Mbowe!
 
Hata kama Mama Samia Suluhu akiwa mwenyekiti wa Chadema hayo mafanikio unayoyataka kwa Mbowe hayawezi kutokea kama hakuna tume huru ya uchaguzi.

Kama kweli una nia njema ya kuishauri Chadema juu ya kufikia mafanikio unayoyaona wewe yanafaa hebu uwe unaandika kwa urefu namna hii kila serikali ya CCM inapowachezea rafu wapinzani kwa mtutu wa bunduki including Tundu Lissu saga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa haki na kwa kulinda heshima ya chama, Mbowe hakutakiwa kugombea uenyekiti wa chama, kwa maana nyakati zilizopo zimebadirika zinahitaji mbinu nyingine ili kuuvusha upinzani kwenye huu mkwamo uliopo.
Mbinu zipi???
Mbowe ndiyo anastahili ndiyo maana CCM wote wanalia ajiuzulu.

Yani mashabiki wa Lipuli mnalia kocha wa Mbeya City ajiuzulu 🤣🤣🤣

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom