Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Moshi Mjini asitisha Mkutano wa CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Moshi Mjini asitisha Mkutano wa CHADEMA

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kamende, Oct 17, 2010.

 1. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2010
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwa wale wanaoujua mji wa Moshi wataweza kufuatilia kirahisi sana namna ambavyo uamuzi huu uluvyofanyika bila kufuata ukweli wa kisheria wala kimazingira.

  Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi Mgombea Mwenza wa kiti cha urais kwa tiketi ya CCM Dr. Ghalib Bilal alikuwa awe mjini Moshi kesho tr. 18/10/2010. Badala yake amefika leo.

  Baada ya CCM kujua kuwa Bilal atakuwepo Moshi leo walimwandikia barua Msimamizi wa uchaguzi wakimtaka ahamishe mkutano wa mgombea ubunge bw. Salakana kutoka katika kata ya Longuo B kwenda Pasua. Barua hiyo badala ya kusubiri ama kuitishiwa kikao cha pamoja cha makatibu wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi mjini Moshi ilijibiwa na Msimamizi mwenyewe kwa kuwaruhusu kufanya mkutano wanavyoona wenyewe inawafaa.

  Hatua iliyofuatia Msimamizi leo amepeleka barua kwa Katibu wa CHADEMA Manispaa ya Moshi akimweleza kusitisha mkutano wa chama hicho katika kata ya Bondeni ili kupisha mkutano wa Bilal ufanyike bila usumbufu wowote.

  Akielezewa kuwa mikutano hiyo iko kata tofauti Msimamizi alijibu kuwa Mkutano uko katika barabara ambayo CCM watapita wakienda kwenye mkutano wao.

  Nalo jeshi la polisi mkoani hapa baada ya kupewa nakala ya barua hiyo wamepeleka magari yaliyojaza askari wa FFU wenye silaha katika uwanja ambao CHADEMA wangefanyia mkutano. Kuanzia saa 7.30 mchana leo gari la maji ya kuwasha limekuwa likivinjari katika mitaa ya Moshi kama tishio kwa yeyote atakayethubutu kwenda katika mkutano wa CHADEMA.

  Muda huu nimepata habari kuwa mkutano wa Bilal ambao ulikuwa upambwe kwa kurejeshwa kwa kadi za CHADEMA ambazo wamezitengeneza wenyewe umekuwa na mahudhurio mabaya sana.
   
 2. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2010
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,550
  Likes Received: 1,307
  Trophy Points: 280
  Wanasema you can for a while but not forever..... wananchi tumechoka, hatudanganiki na wala hatutishiki na sisiem
   
 3. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2010
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hawa ccm hawa, dawa ni kuwavote out ili waache hii monopoly waliyonayo kwenye siasa za Tanzania
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Moshi hawataki upumbavu.

  Wana akili. Wana Elimu. Wana mali. HAWAITAKI CCM. This is the kind of people we want in Tanzania.

  CCM inawauma kweli kuhusu Moshi!!
   
 5. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Haisaidii kitu ni ulimbukeni tu . Mwisho umefika na miti yote inateleza
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,575
  Likes Received: 18,491
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli kwa msimamo, watu wa Moshi ni mwisho, t-shirt na kofia wanavaa, nauli wanapokea na pilau wanakula, ila siku ya siku, kurua wanapeleka Chadema.

  Naamini hivi ndivyo itakavyokuwa kwa Watanzania wote wanaitakia mema nchi hii, October 31, watapigia kura zao kwenye ukweli dhidi ya ubatili, japo wapendaubatili pia wapo na watapendelea ubatili uendelee ili wazidi kuneemeka na ubatili huu.
   
 7. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Kura yangu CHADEMA tu;
   
 8. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wao waendelee tu lakini watavuna chuya
   
 9. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  huyo aliyekuletea habari ni muongo kwani mimi nilikuwepo ktk mkutano huo na mahudhurio ya wananchi yalikuwa makubwa na yakutia moyo hivyo wacheni propaganda zenu!!!

  kama moshi ni ngome ya chadema mbona manispaa ya moshi tangu uchaguzi wa 1995 mpaka leo inaongozwa na madiwani wengi ni ccm na meya ni ccm!! Yaani hapa kuna mbunge kweli wa chadema lakini hana nguvu yoyote ya kuchangia sera za chadema kwani wenye kura nyingi ni madiwani wa ccm!!!

  sasa ngome iko wapi?
   
 10. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hii ishu ni kweli namlidhani kuwa mtapata wananchi wengi kwa kuwateka kisaikolojia watu wa chadema. pia inaonesha namna gani CCM haiheshimu utawala wa sheria kwa kunyonga demokrasia. mmelazimisha mkutano huo. Mmmekosa wasikilizaji mpaka wale wanachama feki wa kurejesha kadi mmekosa pia.

  halafu mnatumia pesa ya umma kutoa ulinzi wa UwT kwa mgombea mwenza wakati hana status yeyote bado. Mnaona mlivyo malunatic????? Tunajua kuliko mnavyofahamu.


   
 11. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2010
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,971
  Likes Received: 243
  Trophy Points: 160
  Watu wengine hawatumii hata hekima. Yaani, watu unaenda kuwaomba kura, bado unawafanyia ubabe hao hao! Labda wameshakata tamaa ya kupata kura za wananchi wa kawaida sasa wanajaribu kulinda za wanaccm wenzao.
   
 12. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 315
  Trophy Points: 180
  Watendaji wa serikali wanaopindisha sheria kwa ajili ya kupendelea CCM wanakosa busara. Watatimuliwa siku za karibuni.
   
 13. kisu

  kisu JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 802
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  People Poweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeer!!!!!!!!!!!!!!!
   
 14. MANI

  MANI Platinum Member

  #14
  Oct 18, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  UmkhontoweSiwezi niliwahi kuuliza CCM inategemea kura za maruhani kushinda? Kwani vitendo vyao dhidi ya wapiga kura si vya mtu anaetegemea kura za huyo anayemdhihaki na kumdhalilisha.
   
 15. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2010
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Someni sheria mbona iko wazi mno? Mgombea urais anapewa priority kuliko wagombea ubunge au udiwani.

  Kama kwenye eneo husika kuna mgombea urais, kampeni zingine zote zinasimama.

  Bila kuzielewa sheria mtakuwa mnalia kila siku na kusingizia kuonewa.

  Hata Slaa akienda eneo husika, mikutano ya wabunge inabidi isimame.
   
 16. M

  MILKYWAY GALAXY JF-Expert Member

  #16
  Oct 18, 2010
  Joined: Dec 12, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Nimecheka sana hii:

  upambwe kwa kurejeshwa kwa kadi za CHADEMA ambazo wamezitengeneza wenyewe
  Imenikumbusha ile ya Mr. Bien ya kujiandikia kadi ya birth day.
  Kazi ipo!
   
 17. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #17
  Oct 18, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tupe picha tafadhali. Lazima hapa watu walambe buku buku au zaidi kuhudhulia kikao hiki
   
 18. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #18
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  :A S thumbs_up:
   
 19. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #19
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  :dance:kilaza unaongea nini wewe...............hoooop lesssss hooop lessssss
   
Loading...