Msikilizeni Waziri mwenye Dhamana

Pale kijitonyama kuna chuo cha ustawi, semina ya wiki moja tu inakutosha ili kupata majibu yote ya maswali yako. Mimi nilishapita huko, zamu yako sasa
Jibu swali bwana wewe, una zunguka zunguka tuu😂😂😂

Wanaotekwa ni jamii ipi na wanaobakwa ni jamii gani na wewe ni Waziri wa ustawi wa jamii ipi.
Mbona uko kimyaa

Leo umeyakanyaga
 
Aisee,jibu swali madam,
Achana na maswala ya D madam ,D ndio ya kwanza kwenye jina lako,
Sasa sijui unataka D ipi?😂😂
Wewe huna adabu kabisa. Kwa utovu wa nidhamu huna cha maana cha kurithisha kizazi chako. Hiyo legacy yako itakuwa ya matusi na kiburi.
 
Ukatili wa kihisia kwetu wanaume umeongezeka Mheshimiwa.

Kwa mfano siku hizi imeibuka tabia ya wadada kuomba umtumie nauli ili aje kukutembelea. Ukimtumia tu anakublock au anazima simu.

Pia wameanzisha utaratibu, ukimuomba Namba ya simu na ukaja kumpigia anaanza kukueleza matatizo kibao ili tu umtumie Pesa ambayo mwenyewe unakuwa huna.

Ingefaa wizara mlitazame na hili maana Ni ukatili wa kihisia pia.
 
Jiunge na chama cha wanaume wakupe mawaidha
 
Unawajua TABOA na LATRA?
Mh. Dkt Gwajima Mungu akurejeshe kwenye uwaziri wa hii sekta, nadhani hao LATRA na TABOA hawana interest ya kulinda haki za mtoto (under age) kwenye vyombo vya usafiri zaidi ya wewe na wizara yako. Nadhani wewe ndiye unaweza kuwaamsha na kujua umuhimu wa haki za mtoto kulindwa kwenye vyombo vya usafiri wa umma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…