G4rpolitics
JF-Expert Member
- Jul 29, 2015
- 4,333
- 5,182
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema mpinzani wake katika uchaguzi mkuu mpya utakaofanyika mwezi ujao akifanikiwa kushinda chama chake kitamuondoa madarakani muda mfupi baadaye kupitia bunge.
"Leo hii katika Bunge, tukiwa na wabunge zaidi ya mia mbili na ishirini na kitu, tumepungukiwa na wabunge 13 pekee tuwe na wingi wa theluthi mbili, hii ina maana kwamba tunaweza hata kubadilisha katiba bila kuwa na mbunge wa NASA." "Atafanya nini, hata mkimpatia kura zote, atafanya nini? Anaweza kufanya nini? Hata akichaguliwa, tuna fursa na Bunge, katika kipindi cha miezi miwili mitatu hivi, tumemtoa."
Aidha leo katika ufunguzi wa Bunge, Majaji wa mahakama kuu pamoja na wabunge wa chama cha upinzani cha Nasa walisusia sherehe ya ufunguzi kwa sababu ambazo inasemekana kwa hao majaji ni vitisho ambavyo amekuwa akiwatolea tangu watengue urais wake.
BBC
My take;- unaweza ukamtoa kwa njama za wabunge wako na chuki zako, ngoma ikarudi kwa wananchi wakamrudisha tena, hiyo si kuipa nchi hasara?