wakuu ni kweli hakusema? maneno ya "wanao comments No Reforms No election tutawapata"
=====
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Msemaji mkuu wa serikali ameandika;
"Sikusema maneno haya katika taarifa yangu ya jana, Ndugu zangu Waandishi wa Habari tuzingatie USAHIHI (ACCURACY) katika ripoti zetu"Gerson Msigwa Msemaji wa serikali.
Vikampeni vya kijinga vikoje wa kunyumba?
Je, kusema "No reforms No election" ni kosa?
Je, kulalamika kwamba kwanini serikali imeshindwa kudhibiti utekaji, utesaji, unyanyasaji, udhalilisha, na mauwaji kwa wananchi wanaohoji mambo ya msingi ya kijamii ni kosa?
Je, wananchi kulalamika kwamba viongozi wa serikali na umma hawashughulikii maslahi ya wananchi zaidi ni kujijali wenyewe huku wakiwatishia maisha ni kosa?
Je, kulalamika kwamba serikali imeshindwa kushughulikia kero za wananchi ambao ndio wapiga kura na waajiri wakuu katika kila kitu bila wenyewe kunufaika ni kosa?
Je, vyama vya upinzani na viongozi wa dini kupinga matumizi mabaya ya rasilimali za nchi , kuwanyanyasa na kuwabambikia kesi za kisiasa kisa wanakosolewa kwa utendaji mbovu na usiozingatia maadili ni kosa?
Kampeni za kijinga zinazoanzishwa na vijana wa KiTanzania ni zipoi wakati hamuwapi ajira wala kufanya juhudi zozote za maana kuwawezesha mitaji kila anayehitimu chuo imekosa kosa kwa raia?
Je, viongozi wa serikali na umma kuambiwa kwamba muache kukopa kopa ovyo na kuingia mikataba isiyo na maslahi na wananchi masikini ambao ndio watazilipa kupitia njia mbalimbali ni kosa?
Je, kuambiwa kwamba madaraka ni dhamana na muache kuwadharau wananchi wanapohoji sehemu ambazo hawaridhiki ni kosa?
Vizazi hivi hapa ni vya kuhoji ukivitishia vinaongeza sauti, ukiumiza vinakutangaza havikai kimya
Generation Names
1. The Greatest Generation – born 1901-1927.. (GreGen)
2. The Silent Generation – born 1928-1945. ... (SilGen)
3. The Baby Boomer Generation – born 1946-1964. ...(BaBoGen)
4. Generation X – born 1965-1980. ...(Gen X)
5. Millennials – born 1981-1996. ...(Millenia)
6. Generation Z – born 1996-2012. ...(Gen Z)..................age 13-29yrs (The sixth generation)
7. Gen Alpha – born 2013 – 2025......(Gen A)