Msigwa afunika Iringa Mjini

Msigwa afunika Iringa Mjini

Mkuu hizi picha ni za umati uliofurika katika uwanja wa mwembetogwa mjini Iringa Jana.

Viva CDM

Safi sana, nchi hii ni kubwa chama kimoja hakiwezi kuiongoza. Wanaobeza juhudi za upinzani ni kama wako kwenye kiza kinene
 
Kama alifanya mema hakuwa na haja ya kuitisha mkutano tena wa kusema alichokifanya, kwani kingeonekana!

Umesahau JK alitumia Masaa matatu kujieleza bungeni,pia TBC kila siku inanadi mafanikio ya serikali ya awamu ya 4? Umesahau hayo?
 
Ni katika mkutano uliofanyika Leo 19/7/2015.Mkutano ulikuwa wa kuwashukuru wananchi kwa kumchagua na kuwataarifu wananchi mambo aliyoyafanya kwa miaka mitano ya uwakilishi wake.
11749634_674302662699782_119222844_n.jpg

11750690_10206128734150408_4998628468766549878_n.jpg

Chadema nao kwa kupenda sifa mnajaza watu wengi namna hyo tena wamekuja kwa hiyali yao,vibaya hivyo jamani.
 
Mkuu nilidhani labda mleta uzi kakosea labda hii picha ni ya kutoka chato kwa rais wa ccm,kumbe ni kamanda wa jimbo la iringa!hongereni wana wa iringa

Ahahaha,chato maloli yalikosekana,af anaogopa mji mdogo upo chini ya Chadema
 
Acheni kudanganya watu nyinyi bavicha, binafsi nilifika kwenye ule mkutano wa jana pale kwenye viwanja vya mwembetogwa na Msigwa hajaongea lolote la maana zaidi ya kumkashifu Rais Kikwete kwa kumuita profesa wa kichina na pia kubeza juhudi za serikali katika ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali ikiwemo barabara akidai eti hiyo ni miradi tu (projects) ambazo hazimsaidii raia wa kawaida.

Msigwa jana kaongea yafuatayo kwa ufupi:-
1: magufuli sio suluhisho sababu haikuwa plan yeye apeperushe bendera ya ccm kwenye urais. (upuuzi mtupu)
2: pia amenukuu baadhi ya misemo ya wachina kama ifuatavyo...!
A. Ukiwa na plan ya mwaka 1 panda mpunga maana utavuna ndani ya kipindi hicho.
B. Ukiwa na plan ya miaka 25 panda miti maana utaweza kuivuna ndani ya muda huo.
C. Ukiwa na plan ya miaka 100 jenga fikra za watu kutambua haki zao.

NB: kwa maana hiyo Msigwa jana ame-declare kuwa ana plan ya miaka 100 kwahiyo yupo bize kutoa elimu ya uraia ndo maana masuala kama huduma za kijamii kama vile maji,barabara,elimu,afya na mengineyo sio VIPAUMBELE vyake na hata vishughurikia.

3: alipotakiwa aeleze ameifanyia nini iringa alidai eti MUDA hautoshi kuelezea sababu ni wakati wa msanii Frola Mbasha na wenzake kama mike T mnyalu,Izzo bizness na Roma mkatoliki KUTUMBUIZA.

4: pia anajivunia kwa kipindi cha miaka 5 ya ubunge wake watu wa iringa sasa wanatambua haki zao,pia ni MAJASIRI wa kupigana na polisi maana hawawaogopi tena polisi.

5: pia anajivunia kulala selo ingawa ana kitanda kizuri na mke mzuri nyumbani. ( mke wa msigwa ni meneja wa crdb tawi la iringa anaitwa mama Kisa)

6: pia anajisifu jinsi spika Anna Makinda anavyomuogopa pindi akiona jina lake kwenye orodha ya wachangiaji.

Mwisho.

Msigwa kama mbunge hajafanya lolote hapa iringa hata jambo la kipuuzi hajafanya achilia mbali jambo la maana.
Kuthibitisha nisemayo namnukuu "wana iringa mnahitaji mtambue haki zenu na sio madaraja maana mvua ikija yatabomoka" mwisho wa kunukuu.

Kiukweli wana iringa tunahitaji tumpate mbunge baada ya kuishi miaka 5 bila ya mbunge maana huyu anaemaliza muda wake hajafanya lolote lile liwe dogo au kubwa na mwenyewe amethibitisha hilo jana.
 
Uzuri wa mwaka huu wananchi wengi sana watapiga kura
 
Back
Top Bottom