Msigwa afunika Iringa Mjini

Msigwa afunika Iringa Mjini

Aisee hapana. Niseme ukweli Iringa kurudi CCM haitawezekana. Hakuna mtangaza nia hata mmoja mwenye nusu ya mvuto wa mchungaji. Siongei unafiki Ila kwa macho yangu nimeona watu wengi tena wa hali ya chini sana wakitembea kwa mguu toka nduli kwa kupitia milimani ili kukwepa ffu wafike kwenye huo mkutano. Ilikua AMAZING
 
Jimbo lishaondoka hilo, hakuna alichokifanya cha maana kwa muda wa miaka mitano, yeye aendelee na kazi yake ya zamani ya kulisha Kondoo wa BWANA, hiyo ndio inamfaa!

Musalani haya muambie mama lwakatare
 
Tunataka Wabunge wanaoonesha uhai Bungeni, Msigwa ni mmoja wapo. Viva Chadema, Viva Msigwa
 
Ni katika mkutano uliofanyika Leo 19/7/2015.Mkutano ulikuwa wa kuwashukuru wananchi kwa kumchagua na kuwataarifu wananchi mambo aliyoyafanya kwa miaka mitano ya uwakilishi wake.

Duuuu,nyomi hii ndio ilistahili aipate makofuli kule chato
 
Watu wa Iringa mmetufurahisha kwa kumpokea kamanda, hakika mmechagua fungu jema

Na tunawaomba wamchague tena kwenye uchaguzi wa mwezi october ili awawakirishe wao na taifa zima.
 
Kama alifanya mema hakuwa na haja ya kuitisha mkutano tena wa kusema alichokifanya, kwani kingeonekana!
Namkubali sana Msigwa, unajua kuna watu, wanahitaji tunuku bila kujali itikadi za vyama. kujitekenya mwenyewe na kucheka mwenyewe ni insanity. kwani mbunge kuwashukuru wananchi wake kuna kosa gani? halafu kumbuka sio wte wanaojua aliyoyafanya, kwa ufafanuzi wake wanaelewa zaidi. Ndugu na hako ka avatar kako, nilitegemea ungekua more constructive in your philosophy. emancipate yuorsele from mental slavery of thinking that, it is only CCM that has good people. Msigwa has written his history in this country. stop GIGO.
 
Mch. Msingwa mpaka Iringa nyomi lote hilo...Lakini nawe na weeeeeeeeee....!
 
Mh! hii sasa sifa! watu wote hao khaa..

Mkuu nilidhani labda mleta uzi kakosea labda hii picha ni ya kutoka chato kwa rais wa ccm,kumbe ni kamanda wa jimbo la iringa!hongereni wana wa iringa
 
Aisee hapana. Niseme ukweli Iringa kurudi CCM haitawezekana. Hakuna mtangaza nia hata mmoja mwenye nusu ya mvuto wa mchungaji. Siongei unafiki Ila kwa macho yangu nimeona watu wengi tena wa hali ya chini sana wakitembea kwa mguu toka nduli kwa kupitia milimani ili kukwepa ffu wafike kwenye huo mkutano. Ilikua AMAZING

Watu wa Ndulu si mchezo..nakumbuka 2010 walipita kule mlimani ni nyimbo maarufuya" Freedom is coming tomorrow"
 
Back
Top Bottom