IROKOS
JF-Expert Member
- Aug 13, 2011
- 10,182
- 7,844
Habari zenu wakuu,
mimi nina mchumba wangu ambaye tunatarajia kufunga ndoa. Lakini kuna jambo moja dogo sana ambalo kwakweli huwa simuelewi yaani hapendi nimshike kiuno kitu ambacho mimi napenda nijivunie kwake.
Yaani nikimshika tu tunapokuwa matembezi au hata kwenye tukio kama harusi huwa hapendi na anawahi sana kutoa mkono. Sasa najiuliza kwanini awe hivyo?
Na naomba niwaulize wasichana/wanawake hivi unajisikiaje unaposhikwa kiuno na mpenzi wako au mume?
Sasa siku ya harusi Mziki mtafunguaje? Maana itakuwa blues...