Msichana jini aibuka dar



iodvfb.jpg


Msichana mmoja (jina tunalihifadhi) mkazi wa Mbezi Salasala Kizudi A jijini Dar es Salaam anadaiwa kuwa jini kwani wanaume waliomtongoza au kuzini naye hufa huku mmoja akiwa hoi kitandani, Amani lina data za kushiba.

Tukio hilo la kusisimua limegundulika hivi karibuni huko huko Salasala eneo maarufu kwa jina la Mtaa wa Wakurya baada ya vijana watatu waliomtongoza ‘jini’ huyo kudaiwa kupoteza maisha huku mmoja akiwa ‘tiamajitiamaji’ hadi sasa.


Akisimulia ishu nzima, jirani mmoja wa msichana huyo (naye jina tunalo) alisema kuwa, karibu mwaka mmoja sasa, watu kadhaa wamekuwa wakimlalamikia bibi wa msichana huyo kuwa, amekuwa akuhusika na nguvu za mjukuu wake za kuua vijana wanaomtongoza au kufanya nao mapenzi.

“Yaani naweza kusema kuwa, karibia mwaka sasa, watu wanamlalamikia bibi yake …(anamtaja jina) kuwa, ndiye mwenye hizo nguvu za kijini kwa mjukuu wake,” kilisema chanzo hicho.

Aidha, kiliendelea kudai kwamba, tofauti na kupoteza maisha, wengine waliowahi kumgusia bibi hilo tatizo la mjukuu wake, walipoteza fahamu, kuugua kwa muda mrefu au kuchanganyikiwa akili na kuwa vichaa.

Mei 15, 2010, kijana aliyefahamika kwa jina la Muddy amefariki dunia mara baada ya kushiriki tendo la ndoa na ‘jini’ huyo hali iliyozua minong’ono kibao msibani.


Marehemu Muddy alizikwa Mei, 16 makaburi ya Salasala na msiba wake kupelekwa kwao, Lindi na rafiki yake wa karibu ambaye jina halijajulikana mara moja.

Hali hiyo ilisababisha vijana wengine waliowahi ‘kumtokea’ msichana huyo kushtuka na kutoboa siri zao.


Kijana Edson ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita Shule ya Msingi Kunduchi, Mkazi wa Mtaa wa Kizudi ‘B’ Salasala ambaye kwa sasa yupo hoi kitandani, yeye alidai kuuvaa mkenge huo siku moja alipokuwa akitoka shuleni ambapo alikutana na mrembo huyo njiani.

Anasema alikutana na msichana huyo na kuvutiwa naye sana, “hivyo niliamua kumtongoza bila wasiwasi wowote,”anasema Edson.

Edson, anaendelea kusema kuwa, msichana huyo alikubali na kuahidiana wakutane siku ya tatu baada ya siku hiyo.


Anasema siku moja ‘jini’ huyo alituma ujumbe wa barua kwake akimwomba wakutane Disco maeneo ya jirani na anapoishi (‘jini’ huyo).

Akasema kuwa, kwa sababu roho ya zinaa ilikuwa imemkamata, alikubali na usiku huo walikutana disco na kukandamiza burudani kwa kwenda mbele pasipo kufahamu kwamba, kidosho huyo bomba ana nguvu za ajabu za maangamizo mwilini mwake.

Anasema walipoachana, walipanga kukutana siku nyingine kwa ajili ya ‘hafla’ fupi ya uzinduzi wa penzi lao.

Aprili 9, 2010, Edson anasema kuwa, alipata ‘apointimenti’ nyingine kutoka kwa mlimbwende huyo akitaka wakutane majira ya saa kumi na mbili jioni maeneo ya kwao demu huyo.


Edson anasema: “Muda ulipofika nilikwenda Kizudi A anapoishi ambapo tulikutana na tukaamua kwenda kichakani kwaajili ya kukamilisha tendo lenyewe.”
Anasema kuwa, hata wakati wa shughuli yenyewe hakuona dalili zozote za ajabu zaidi ya kumalizana na kila mmoja kuchukua kasi kuelekea kwao salama.

Edson akasema kuwa, muda mfupi baada ya kuwasili kwao, ghafla alianza kujisikia vibaya, miguu ilikosa nguvu na baadaye kutokwa damu jicho la upande wa kushoto huku akijisikia maumivu makali mwilini.


Akiwa kwenye hali hiyo, kaka yake, Philipo Elias alimpeleka Zahanati ya Salasala ambako madaktari walipompima hawakuona ugonjwa, wakamwongeza damu na kesho yake kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Hata hivyo, Edson anadai kuwa, mwishowe kaka yake alimpeleka kwa mganga wa kienyeji ambaye alipochanganya manyanga yake alibaini kuwa, kijana huyo alifanyiwa mchezo mbaya na msichana aliyefanya naye mapenzi.


Mganga huyo aliwaambia kuwa, jino moja upande wa kushoto la msichana huyo ni jini na jingine moja upande wa kulia ni binadamu.

Akiongelea jambo hilo, kaka mtu huyo alisema kuwa, baada ya mganga kutoboa siri hiyo, yeye alifunga safari hadi nyumbani kwa msichana huyo na kumkuta akiwa na bibi yake, bila kusita aliwaambia wafanye wawezavyo wahakikishe mdogo wake anapona ingawa bibi huyo alishtushwa na maneno ya kaka mtu hivyo kuahidi kushughulikia jambo hilo.


Siku zilikwenda bila mafanikio, Mei 17 mwaka huu ‘braza’ huyo alikwenda tena nyumbani kwa bibi huyo na kuwasha moto ambapo walifikishana kwa Mjumbe wa Mtaa na suala hilo kusikilizwa ambapo Mjumbe aliwaambia warudi siku iliyofuata (Mei 18) kwa kuhofia vurugu kutokana na watu wengi kufurika nyumbani hapo kusikiliza shauri hilo. Fuatilia sakata hili wiki ijayo kwani Amani linamsaka Mjumbe wa mtaa huo kusikia kauli yake.
ndo mkome kutongozatongoza, wahaya wahaya, sasa wamekuwa majini!!

yangu macho na masikio
 
Hakuna kitu kama hicho story ya kichina hii, bora watunzi wa hii story feki wangesema kijana wa kidato cha sita wangenishawishi ni fikirie kidoogo. Wameharibu story yao walivyosema darasa la sita.
 
Hivi yule dada aliyegeuka MANYOWA pale Manyowa bridge ameisharudi kwao? Nauliza tu wakuu
 
Hii story haina mantic yni kijana wa darasa la sita,pia wana uwezo wa kupar disco then wanaenda kud vichakan!so amazing
 
ni kweli 'majini mapenzi' yapo google 'sicubus' wao wenyewe wanaweza wasiwe wanania ya kukudhuru lakini ktk kufanya tendo la ndoa wasuck energy from the sex partner kitendo ambacho kinaweza kumuua huyo partner au kumpa madhara makubwa...mbaya zaidi huwezi kumjua kwa kumuangalia huyo jini wanakuwa just like any other normal woman and in most cases much attractive than ordinary woman......so kazi kwenu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom