Msichana jini aibuka dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msichana jini aibuka dar

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, May 20, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  [​IMG]

  Msichana mmoja (jina tunalihifadhi) mkazi wa Mbezi Salasala Kizudi A jijini Dar es Salaam anadaiwa kuwa jini kwani wanaume waliomtongoza au kuzini naye hufa huku mmoja akiwa hoi kitandani, Amani lina data za kushiba.

  Tukio hilo la kusisimua limegundulika hivi karibuni huko huko Salasala eneo maarufu kwa jina la Mtaa wa Wakurya baada ya vijana watatu waliomtongoza ‘jini’ huyo kudaiwa kupoteza maisha huku mmoja akiwa ‘tiamajitiamaji’ hadi sasa.


  Akisimulia ishu nzima, jirani mmoja wa msichana huyo (naye jina tunalo) alisema kuwa, karibu mwaka mmoja sasa, watu kadhaa wamekuwa wakimlalamikia bibi wa msichana huyo kuwa, amekuwa akuhusika na nguvu za mjukuu wake za kuua vijana wanaomtongoza au kufanya nao mapenzi.

  “Yaani naweza kusema kuwa, karibia mwaka sasa, watu wanamlalamikia bibi yake …(anamtaja jina) kuwa, ndiye mwenye hizo nguvu za kijini kwa mjukuu wake,” kilisema chanzo hicho.

  Aidha, kiliendelea kudai kwamba, tofauti na kupoteza maisha, wengine waliowahi kumgusia bibi hilo tatizo la mjukuu wake, walipoteza fahamu, kuugua kwa muda mrefu au kuchanganyikiwa akili na kuwa vichaa.

  Mei 15, 2010, kijana aliyefahamika kwa jina la Muddy amefariki dunia mara baada ya kushiriki tendo la ndoa na ‘jini’ huyo hali iliyozua minong’ono kibao msibani.


  Marehemu Muddy alizikwa Mei, 16 makaburi ya Salasala na msiba wake kupelekwa kwao, Lindi na rafiki yake wa karibu ambaye jina halijajulikana mara moja.

  Hali hiyo ilisababisha vijana wengine waliowahi ‘kumtokea’ msichana huyo kushtuka na kutoboa siri zao.


  Kijana Edson ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita Shule ya Msingi Kunduchi, Mkazi wa Mtaa wa Kizudi ‘B’ Salasala ambaye kwa sasa yupo hoi kitandani, yeye alidai kuuvaa mkenge huo siku moja alipokuwa akitoka shuleni ambapo alikutana na mrembo huyo njiani.

  Anasema alikutana na msichana huyo na kuvutiwa naye sana, “hivyo niliamua kumtongoza bila wasiwasi wowote,”anasema Edson.

  Edson, anaendelea kusema kuwa, msichana huyo alikubali na kuahidiana wakutane siku ya tatu baada ya siku hiyo.


  Anasema siku moja ‘jini’ huyo alituma ujumbe wa barua kwake akimwomba wakutane Disco maeneo ya jirani na anapoishi (‘jini’ huyo).

  Akasema kuwa, kwa sababu roho ya zinaa ilikuwa imemkamata, alikubali na usiku huo walikutana disco na kukandamiza burudani kwa kwenda mbele pasipo kufahamu kwamba, kidosho huyo bomba ana nguvu za ajabu za maangamizo mwilini mwake.

  Anasema walipoachana, walipanga kukutana siku nyingine kwa ajili ya ‘hafla’ fupi ya uzinduzi wa penzi lao.

  Aprili 9, 2010, Edson anasema kuwa, alipata ‘apointimenti’ nyingine kutoka kwa mlimbwende huyo akitaka wakutane majira ya saa kumi na mbili jioni maeneo ya kwao demu huyo.


  Edson anasema: “Muda ulipofika nilikwenda Kizudi A anapoishi ambapo tulikutana na tukaamua kwenda kichakani kwaajili ya kukamilisha tendo lenyewe.”
  Anasema kuwa, hata wakati wa shughuli yenyewe hakuona dalili zozote za ajabu zaidi ya kumalizana na kila mmoja kuchukua kasi kuelekea kwao salama.

  Edson akasema kuwa, muda mfupi baada ya kuwasili kwao, ghafla alianza kujisikia vibaya, miguu ilikosa nguvu na baadaye kutokwa damu jicho la upande wa kushoto huku akijisikia maumivu makali mwilini.


  Akiwa kwenye hali hiyo, kaka yake, Philipo Elias alimpeleka Zahanati ya Salasala ambako madaktari walipompima hawakuona ugonjwa, wakamwongeza damu na kesho yake kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

  Hata hivyo, Edson anadai kuwa, mwishowe kaka yake alimpeleka kwa mganga wa kienyeji ambaye alipochanganya manyanga yake alibaini kuwa, kijana huyo alifanyiwa mchezo mbaya na msichana aliyefanya naye mapenzi.


  Mganga huyo aliwaambia kuwa, jino moja upande wa kushoto la msichana huyo ni jini na jingine moja upande wa kulia ni binadamu.

  Akiongelea jambo hilo, kaka mtu huyo alisema kuwa, baada ya mganga kutoboa siri hiyo, yeye alifunga safari hadi nyumbani kwa msichana huyo na kumkuta akiwa na bibi yake, bila kusita aliwaambia wafanye wawezavyo wahakikishe mdogo wake anapona ingawa bibi huyo alishtushwa na maneno ya kaka mtu hivyo kuahidi kushughulikia jambo hilo.


  Siku zilikwenda bila mafanikio, Mei 17 mwaka huu ‘braza’ huyo alikwenda tena nyumbani kwa bibi huyo na kuwasha moto ambapo walifikishana kwa Mjumbe wa Mtaa na suala hilo kusikilizwa ambapo Mjumbe aliwaambia warudi siku iliyofuata (Mei 18) kwa kuhofia vurugu kutokana na watu wengi kufurika nyumbani hapo kusikiliza shauri hilo. Fuatilia sakata hili wiki ijayo kwani Amani linamsaka Mjumbe wa mtaa huo kusikia kauli yake.
   

  Attached Files:

 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,173
  Trophy Points: 280
  Bongo mtu anaweza kuwa na Ebola -au ugonjwa mwingine wa ajabu- halafu watu wakasema jini.
   
 3. p

  pori Member

  #3
  May 20, 2010
  Joined: Mar 12, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na bado! mtaangamia wengi nyie mnaopenda kufunua kila 'sketi' ipitayo mbele yenu.
   
 4. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,936
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Ni kweli ukimwi wenyewe mpaka leo ndugu wa marehemu wanasema alilrogwa. Au mgonjwa wao wa ukimwi wanampa dawa za kienyeji za kuondoa kurogwa - nimeshuhudia haya kwa macho yangu.
   
 5. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,936
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Sasa serikali au mahakama itahakikisha vipi? Watu wengine ufa kwenye gemu hasa wanapotumia energy nyingi kuliko iliyopo mwilini, yawezekana dada huyo ni wa shoka na anavuta kasi kwenye gemu sio mchezo; jamani kabla ya kumfuata basi tule balance diet ya kutosha lakini hata ukimtongoza tu unakufa, hii kali!
   
 6. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mimi sichangii kitu ila fanyeni gwalide vijana. Kiunoooooo nyumaaaaaa ! shaaaaap zipuuuu funga ! geuka rudi home
   
 7. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Choma moto wote, kwanza tungeanza na waganga yeyote anae practise uganga ni moto tu no sympathy. These people are no good to us. Then we go to those who are corrupted in the belief either wachawi or not burn burn no sympathy.
   
 8. Mkosoaji

  Mkosoaji JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Duh! Balaa! Kuishi kwingi utaona mengi!!!
   
 9. P

  Preacher JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2010
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mshahara wa dhambi ni mauti
   
 10. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #10
  May 21, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  ...Eeeh Mwenyezi Mungu ukirehemu kizazi hiki.
   
 11. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #11
  May 21, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Hii habari inashangaza ....
   
 12. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mbona mi siamini!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 13. d

  damn JF-Expert Member

  #13
  May 21, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Me too. but yawezekana ni kweli. Duniani **** maajabu. Wachapishe picha yake kweli ili fijana wamjue wasiendelee kufa.
   
 14. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #14
  May 21, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Ahh Jamani STANDARD SIX; anaona poa tu kutongoza! Mungu atusaidie!
   
 15. w

  wakumbuli Senior Member

  #15
  May 21, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  sasa darasa la sita unapiga gemu na unajua kutongoza,kwa kweli kama hilo jini lingekua haliui mpaka sidhani kama ungefika chuo na kama ungefika basi ungekuwa na wanawake 15,750
   
 16. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #16
  May 21, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Acheni kuvunja amri ya sita aliyopewa Mussa na mungu wake,sasa mnaona!
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  May 21, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Dawa yake unajipaka mafuta ya kitimoto na kumtokea huyo mpenzi jini!
   
 18. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #18
  May 21, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Kwa nini hadithi za popobawa na majini zinakuja wakati uchaguzi unakaribia kuna uhusiano wowote jamani. Na siku zote majini na popobawa hawaendi masaki upanga na oysterbay? Tuliangalie hili kwa makini
   
 19. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #19
  May 21, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  only God will keep you safe, if you obey his Ten commandment
   
 20. Mgoneke

  Mgoneke Member

  #20
  May 21, 2010
  Joined: May 11, 2010
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siamini kama ni kweli....hii ni waandishi wanajaribu kutafuta njia ya kujipatia pesa na umaarufu..hii issue imekuwa framed kama ile ya manyoya
   
Loading...