Msichana atoweka Marekani akiwa mikononi mwa Balozi

Umeona ee, tangu awali nimetahadharisha jambo hili kuwa makini kwa sababu ni la kimataifa. Ingekuwa kitaifa ingekuwa vyema kumwandama mama, lakini kwa hali ilivyo kuna umuhimu wa kulifuatilia kidiplomasia ili wazazi na ndugu zake wajue yuko wapi. Suala lilipofikishwa vyombo vya usalama Marekani walijibiwa ni mtu mzima huenda yuko na bf wake, ukisikia hivyo hawa jamaa wanajua yuko wapi na anaishi na nani, ila huwa hawapendi kuingilia private ya mtu aliyekwisha vuka 18. Muhimu kutumia njia za kawaida kumtafuta aliko ili wazazi na ndugu wake wajue alipo ili kupata amani mioyoni mwao.

Wengi sana wanakimbia wakifika US, wengine Canada na nchi nyingine, tuna mifano hata ya wake za watu walikuja huku na wakaingia mitini kimoja... zimebaki story tu.

Sisemi kwamba huyo dada katoroka, hapana, ila there is a possibility.... Hii kitu imetokea years and years

Ndio maana wengine wanaambiwa kabisa, ukipata chance ya kwenda nje, usichukue ndugu... kuna lawama badae

Anyway, i wish they find the lady and she is safe
 
Usiseme hivyo hata kidogo. kwa mimi ninayemfahamu, yule binti hawezi kufanya hivyo. Huyu mama aseme Aneth yuko wapi? Hadhi ya kibalozi mtu huvishwa vile vile huvuliwa. Ebu rais wetu lipe jambo hili uzito mwingi. Mama huyu avuliwe u-diplomasia, tujue kwanza raia wa Tanzania (ANNETH) yupo wapi. Tukisha jua mvisheni tena.

Simba mwenda kimya ndiye mla nyama. Nisiseme hivyo niseme nini? Kila mtu na mawazo yake, haiwezekani mimi na wewe na mwengine wote tuwe na mawazo aina moja.
 
Yanayonishangaza...

-huyu mama hakusema kwa familia au hata aliyemtafutia msichana

- huyu mama kweli ana roho sijui nisemeje, hakuogopa kutowatafuta familia miaka yote

- anakimbilia kutaka kutoa pesa kusaidia mama yake Annet

- anadai alimweleza mtu aliyekufa kuhusu binti huyu...mmmmhh ???

-kweli huyo sijui nani kama yeye tu alielezwa kwanini alificha kwani ni siri afe na info hiyo bila kumwambia hata wazazxi wa binti?

-AMEKIMBILIA KUTAFUTA MAWAKILI???????

-kama angekuwa anaogopa sheria asingenyamaza, aliona miaka imeenda akajua ameshinda, msibani wakampata vizuri.

-huyu mama anaficha kitu na ameshawasimulia mawakili wake. Mawakili kama tujuavyo wote wanajua kudanganya.

- mie sijui vipi ila nahisi huyu baloxi amemdhuru binti huyu. Sababu sijajua story yote as kwa nilivyosoma huyu mama ni suspect big time. Imagine hata kukasirika alitorokwa kama anavyodai si angejulisha watu jamani?

- mie nahisu amemzulu hata kumuua labda kafanya, au sijui cha kusema. Sielewi kwanini akae kimya miaka karibu saba hadi ndugu wakufate msibani, na baadae unajitetea sana na hata kuitisha lawyer.

-mambo ya msichana alipewa na jamaa zake, kwa nini hakuripoti???

-hii kesi ya FBI, huyu mama anaficha kitu kabisa duh wasimwachie kabisa.

-ndio mnasema sijui kakimbia ila why balozi anajitetea sanaaaaa hadi lawyers???? Hadi kuomba ndugu wasaini???

Anaojua ndugu wa Annet awashauri waende American Embassy kuripoti. Ukweli utakuja nje...
 
inanikumbusha Spika wetu na hausigeli wake ambae nae alipotea kwenye mazingira ya kutatanisha miaka ya themanini hadi leo...spika kabaki na mtoto wa hausigeli...so sad...wanawake mna roho ngumu sana
 
Suala hili ni gumu na la hitaji njia za kidiplomasia katika kulifuatilia na kutafutai ufumbuzi wake.
Tanzania
Inawezekana kumvuta mkono huyu Grace aeleze alipo huyu msichana ili aisaidie polisi kupatikana alipo kwa vile ametoweka mikononi mwake huku ndugu wakitaka kujua aliko.​

Marekani
Umri wa msichana ni zaidi ya miaka 18 na hivyo kwa sheria za nchi hiyo hayuko chini ya malezi ya wazazi na yuko huru kutafuta hifadhi au kuchagua kwenda popote anapotaka mradi havunji sheria.​

Kuna uwezekana huyu Grace alikuwa anamnyanyasa huyu msichana, kwa Marekani ukipata mwanya wa kumtoroka anayekunyanyasa ni haki yako inayolindwa ingawa vyombo vya dola vinaweza kujua wapi yupo ili mradi havunji sheria anabaki anatanua tu. Vinginevyo msichana angemfungulia madai Grace kumnyanyasa, angekuwa matatani, ashukuru msichana aliamua tu kumtoroka kwa sababu ya kutojua haki zake kisheria.

Tunapojadili jambo hili tujue taratibu za nchi mbili tofauti zinavyotetea haki za binadamu na watoto, na pengine kukuta sheria zinazopingana kati ya nchi na nchi. Ndio maana nasema bora kuwe na njia za kidiplomasia katika kushughulikia shauri hili badala ya kuchukua mkondo wa sheria tutashtukia kugonga mwamba maeneo fulani ndio maana jambo hili linampa kichwa huyu mama.
Kwa sheria za marekani huyu mama (Balozi ) anashukuru kwa binti kutokomea bila kumfungulia mashtaka,ingekula kwake vibaya mno kama angemshtakiwa kwa kosa la kumnyanyasa binti.

Familia ya huyu binti wawe wapole katika harakati zao za kumsaka binti yao ili kupata ukweli kuwa alitorokea marekani ama kwingineko na Je yu hai!?.Wakianza ushabiki bila kutumia akili inaweza ikawagharimu wao inderect kwa kumchoma binti yao kama alifanya any Illegal act.
 
Wengi sana wanakimbia wakifika US, wengine Canada na nchi nyingine, tuna mifano hata ya wake za watu walikuja huku na wakaingia mitini kimoja... zimebaki story tu.

Sisemi kwamba huyo dada katoroka, hapana, ila there is a possibility.... Hii kitu imetokea years and years

Ndio maana wengine wanaambiwa kabisa, ukipata chance ya kwenda nje, usichukue ndugu... kuna lawama badae

Anyway, i wish they find the lady and she is safe

Hapa nami naungana nawe kabisa ,tunaweza tukawa tunamlaumu mama (Balozi ) kumbe binti alishaona atarudishwa bongo akasepa. Hii inafanyika sana na sio kwa kina dada tu hata kwa wanaume wengi wanatokomea na wanajilipua (wanachoma nyaraka zote za uraia walikotoka)
 
Dada ashasepa ashazoe US mnataka aje bongo kukoga vumbi na kula jua? Kula raha huko tacobell,magnolia na crenshaw.
 
Hapa nami naungana nawe kabisa ,tunaweza tukawa tunamlaumu mama (Balozi ) kumbe binti alishaona atarudishwa bongo akasepa. Hii inafanyika sana na sio kwa kina dada tu hata kwa wanaume wengi wanatokomea na wanajilipua (wanachoma nyaraka zote za uraia walikotoka)

kuna wake za waandishi wa habari kama wawili hivi mmoja kanada na mmoja US wamezamia... ijekua housegirl?
 
Kwa sheria za marekani huyu mama (Balozi ) anashukuru kwa binti kutokomea bila kumfungulia mashtaka,ingekula kwake vibaya mno kama angemshtakiwa kwa kosa la kumnyanyasa binti.

Familia ya huyu binti wawe wapole katika harakati zao za kumsaka binti yao ili kupata ukweli kuwa alitorokea marekani ama kwingineko na Je yu hai!?.Wakianza ushabiki bila kutumia akili inaweza ikawagharimu wao inderect kwa kumchoma binti yao kama alifanya any Illegal act.

Umejibu kwa upeo wa kimataifa, maana masuala mengine wengine tunajibu kibongobongo kisha kuishia kulalamika ni kwa sababu hatukuchukua kuliangalia suala kwa hatua za juu zaidi.
 
Hapa nami naungana nawe kabisa ,tunaweza tukawa tunamlaumu mama (Balozi ) kumbe binti alishaona atarudishwa bongo akasepa. Hii inafanyika sana na sio kwa kina dada tu hata kwa wanaume wengi wanatokomea na wanajilipua (wanachoma nyaraka zote za uraia walikotoka)

Ukishaingia huko kusepa ni rahisi na huulizwi mbona umepotea njia, ila akili kumkichwa. Angerudi bongo ingabaki historia tu aliishi huko wakati hakuyapata aliyotegemea ndoto yake kufikia kwani kuishi ubalozini ni sawa tu kama alikuwa bado bongo kama vile ndege afugwaye ndani ya kiota kisicho na tundu la kujinasua.

Mambo muhimi ninayofikiria kuhusu suala hili ni kama ifuatavyo;
  • Mzunguko wa magazeti ya Tanzania mengi ni Tanzania tu wakati anayetafutwa yuko Marekani. Bora mitandao yenye kusomwa na wengi.
  • Msichana huyo kama anapata ujumbe huu kuwa anatafutwa ni vema ajitambulishe kuwa yu hai ili atulize nyoyo za ndugu.
  • Wanaojua msichana alipo wamshauri umuhimu wa kuwahabarisha ndugu kuwa wasiwe na shaka yu mzima.

  • Ndugu na jamaa watumie njia ambazo zinaweza kufahamu aliko kama mitandao mbalimbali ambayo wengi siku hizi hupitia, watundike picha zake, atapatikana tu kwani dunia sasa hivi ni global villege.
 
mabinti wengi wanoenda USA kama ma-hausigeli baada ya muda wanashawishika wanaota mbawa. wengi hukimbilia kukaa na marafiki zao au wanaume na kufanya kazi hizi za kawaida. kuna binti alishawahi kutoroka kwa mwajiri wake akatusimulia jinsi alivyovunja safe akaiba passport usiku wa manane na kutoroka, na alikuwa mpole sana.

mwenye makosa ni huyo aneth kwa hiyo acheni kumtetea, after all she is 25...meaning she is not a dependent anymore
 
Hao ndugu wa mtoto njaa inawasumbua wanajua mtoto wao atakuwa na dola. Na angekuwa ametoroka na anawatumia pesa wasingehangaika . Kama kupotea au kutoroka mbona wanawake wengi from singida, kigoma etc . Na wanakuja na wanaolewa , wanazaa hata miaka zaidi ya kumi. Huko marekani au uingereza kuna watanzania kibao wamechana pasport na wamejitambulisha kuwa ni waburundi au wasomali na wanapata posho toka serikali za huko . maisha yaanenda
 
Mi hapo sioni case. Binti wa miaka 25? Huyo kazamia ila kosa lake hatumi dolar home. Angekuwa kapoptealea Bongo ningeelewa; US; huyo kazamia mbona. Ila hana mapenzi nanfamilia yake; kakata mawasiliano.
 
Si unaona (japo nimesoma kwa kuruka ruka) mama wa Binti amekataa kutoa ushirikiano kwa waliotaka kumtafuta kwa interpol. Anajua wakimpata ni kum-deport. Na wao wanachotaka ni mawasiliano si kuwa arudi home. Wanataka pesa.

Wangekuwa makini

Back
Top Bottom