Msichana atoweka Marekani akiwa mikononi mwa Balozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msichana atoweka Marekani akiwa mikononi mwa Balozi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Candid Scope, Sep 16, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Grace Mujuma (kulia) akiwa na Anneth Mangawo (kushoto) nchini Marekani.
  Msichana Anneth Mangawo kushoto ndiye anayejajwa kutoweka mikononi mwa Grace.

  Alimchukua kama ‘hausigeli’

  Baba amwomba JK amsaidie

  Binti Anneth Joseph Mangawo (25), wa ukoo wa Owenya anayedaiwa kuchukuliwa na Balozi wa sasa wa Tanzania nchini Zambia, Grace Mujuma, amepotea katika mazingira tatanishi wakati balozi huyo akifanya kazi ubalozi wa Tanzania jijini New York, Marekani. Balozi huyo anadaiwa kumchukua binti huyo kama msichana wa ndani na kwenda naye nchini Marekani mwaka 2004, ambapo kabla alichukuliwa kutoka kata ya Old Moshi Magharibi, ambako alikaa Dar es Salaam, na baadaye nchini Marekani.

  Baba mdogo wa binti huyo, Robinson Owenya, akizungumza na NIPASHE Jumapili, anasema kwa kipindi chote waliwahi kuwasiliana na binti huyo mara moja, hadi Balozi huyo alipomaliza muda wake wa kukaa nchini humo wa miaka minne na kurejea Tanzania mwaka 2008, bila binti huyo. Taarifa zinadai kuwa, mwanzoni mwa mwaka 2012, Balozi Grace akiwa ameshateuliwa na Rais kuwa Balozi wa Zambia, alikuja kwenye msiba wa baba yake mzazi eneo la Old Moshi, mkoani Kilimanjaro. “Tulimfuata kumuuliza juu ya mtoto wetu, majibu aliyotupa ni kuwa alikuwa ananyanyasa watoto wake na mama wa Anneth akamuuliza kwa nini hakumpakia kwenye ndege arudi, alidai kuwa alimpeleka shule akajifunze Kiigereza na ndipo akaiba pasi ya kusafiria na vitambulisho na akaondoka,” alisema Owenya. Alisema walikwenda kwa baba yake mdogo, anayemtaja kwa jina la Fredy Maro, ambapo waliondoka pamoja na kwenda kwa kaka yake, Dk. Prosper Maro, ambaye alimtetea dada yake na kueleza kwamba wakifuatilia kisheria, binti yao atakamatwa nchini humo na kupelekwa gerezani na hatarudi hadi baada ya kifungo. “Nilimweleza ninachotaka ni binti yetu apatikane akiwa hai, kama ambavyo alichukuliwa, hatuna mkataba na Mungu,” alisema.


  Aliongeza, “alinipa namba za simu za Balozi Grace, ili mama wa Anneth aweze kupata fedha kidogo, nilikataa na kumueleza shida si fedha bali mtoto wetu, akasema hana la kunisaidia.” Alisema haiingii akilini kuwa mhusika (Grace Fanuel Maro ambaye kwa sasa anaitwa Grace Mujuma), anajenga hoja ya kumhusisha binti huyo na unyanyasaji wa watoto kwenye nchi ya kigeni. Alisema alitoa taarifa polisi mkoani Kilimanjaro, na kufungua kesi namba KR/CID/PE/03/2012 Januari 16, mwaka huu, ambapo walimtuma kwenda kuichunguza nyumba ambayo inaelezwa Balozi Grace alikuwepo, eneo la Shanty Town, na kuwapa taarifa polisi. Alisema polisi waliambatana naye hadi eneo hilo, lakini hawakufanikiwa kumkuta kwani muda mfupi alikuwa ameshaondoka kurudi Dar es Salaam.


  Alisema waliacha maagizo kwa mama yake (Grace) afike kituo cha polisi na kuandika maelezo ambapo alifanya hivyo na kuweka namba za simu za mwanaye. “Nilikaa kwa muda, askari mmoja akatumwa Dar es Salaam kufuatilia, ambapo alikuta Grace ameshaapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia na wakati anamchukua binti yetu alikuwa Afisa wa Ubalozi,” alisema. Hivyo, alisema askari polisi hawana uwezo wa kumkamata kwa kuwa anakinga ya kibalozi na kibali cha kumkamata kinatoka kwa Rais,” alisema.

  Alisema alikwenda kwenye kituo cha msaada wa sheria na haki za binadamu jijini Dar es Salaam, ambao waliahidi kumsaidia ikiwa ni pamoja na kutoa kwenye vyombo vya habari lakini hatua hiyo haijafanyika. “Nimeamua kuyasema haya nikijua kwamba hakuna mwenye mkataba na Mungu, nimefanya hivi ili ifahamike,” alisema. “Ninamuomba Rais Jakaya Kikwete kuingilia kati suala hili, kwani aliyechukua binti yetu ni Balozi wake na kumekuwa na ubabaishaji mkubwa, familia yetu ni Maskini…” “Mama yake hajiwezi lakini tunachangishana kupata fedha za kufuatilia suala hili, hatujui tulie msiba au tufanye nini, kama alikufa tungeona hata mwili wake au kujulishwa,” alisema.

  Mama mzazi wa Anneth, Judica Owenya, alisema dada yake, Edora Maro, (ambaye ameolewa na baba mkubwa wa Grace), alikwenda
  nyumbani kwake na kumuomba binti huyo kwa ajili ya kwenda kufanya kazi. Akizungumza huku akilia, alisema mwanaye huyo ni uzao wake wa saba, na kwamba anajisikia vibaya kwani hajui kama yupo hai au la, Hivyo kuiomba serikali kumsaidia kumtafuta mwanaye ambaye hata kwenye msiba wa baba yake mzazi hakufika. Aidha, kwa mujibu wa barua ya Machi 16, mwaka huu, kutoka kwa kampuni ya uwakili ya Rex Attorneys, yenye kumbukumbu namba REX/GMM/171/12 ambao ni mawakili wa Balozi Grace, akijibu barua ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

  Barua ya LHRC yenye kumbukumbu LHRC/LAC.VOL.XVII/9 ya Februari 27, mwaka huu, ambapo Grace alithibitisha kumchukua binti huyo na kwenda naye Marekani kwa ajili ya kufanya kazi za ndani nyumbani kwake. Alisema baada ya kufika alifanya kazi kwa mwaka mmoja, ambapo mnamo Desemba 2, 2005, alitoroka baada ya kuchukua hati yake ya kusafiria na vitambulisho vyake vingine, ambapo alitoa taarifakwa polisi wa nchini Marekani (New York Police Department), ambao walisema kwa mujibu wa sheria za Marekani kwa kuwa binti huyo ana umri wa mtu mzima hawana la kufanya bali wanahisi kuwa amepata mpenzi na kwenda kukaa naye. Alisema pia alitoa taarifa za tukio hilo kwa mjomba wake, ambaye kwa sasa ni marehemu, ambapo baada ya miezi nane kupita tangu kupotea kwake alitoa taarifa kwa vyombo husika kufuta visa yake, ambapo Januari, mwaka 2012 kwa barua ya kumbukumbu namba CID/HQ/PE/16/ 2012 alitoa taarifa kwa Kitengo cha Polisi wa Kimataifa (Interpol) na mnamo Januari 13, mwaka huu, aliieleza familia ya Anneth.


  Hata hivyo, Owenya alisema mnamo Julai 14, mwaka huu, aliitwa jijini Dar es Salaam na kukutanishwa na Grace akiwa na mawakili wake wawili, ambapo baada ya mazungumzo ambayo mengine yalikuwa na utata kutokana na muda mwingi walitumia lugha ya kiingireza asiyoifahamu. Alisema walimshinikiza kuandika barua Interpol kuomba wamsaidie kumtafuta binti yake, lakini alikataa na kueleza kuwa anayemdai ni Grace kwa kuwa ndiye aliyemchukua kijijini na hata walipomuuliza aliwajibu jeuri mara baada ya kukutana kwenye msiba wa baba yake na endapo wasingeuliza asingewajulisha.


  Alisema Agosti 15, mwaka huu, alitumiwa kwa njia ya mtandao makubaliano yenye maelezo ya malalamiko yake na sahihi ya Grace na wakili wake, ikiwa na makubaliano yaliyosomeka na kutakiwa kuyasoma na kuridhika nayo na kisha kuweka sahihi.
  “Grace Mujuma ambaye alikwishatoa taarifa Interpol aendelee kufuatilia kupata taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa Anneth na ashirikiane na kitengo hicho kumtafuta na kumrudisha kwa wazazi wake mapema iwezekanavyo mara baada ya kupatikana kwake,”alisema. Alisema anaiomba serikali kulifanyia kazi suala hilo kwani linatia utata na hakuna hatua zinazochukuliwa ili hali muhusika ni mtu mwenye kinga ya kushtakiwa na wenye mtoto ni watu wanyonge wasio na uwezo wa kifedha. Jitihada za kuwasiliana na Grace kupitia simu za ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Zambia, hazikufanikiwa kutokana na kuita mara kadhaa pasipo kupokewa.
   
 2. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2012
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 2,004
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  ....Tukubali/tusikubali....bila kuitoa serikali hii mamlakani mnyonge siku zote hatatendewa haki....hivi angekuwa ni raia wa kawaida tu mtaani akafungulia MBUZI, wa jirani yake na kisha MBUZI huyo asionekane tena je, angejibu KIFEDHULI kama mama huyu (ambassador)?

  ....inanikumbusha ile kesi ya KINJEKITILE (mtoto wa mzee Kingunge) alipoua mtu kwa makusudi....na hakufanywa lolote lile...

  ...It's very sad...
   
 3. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Mhhhhhh!Huyo mama ana kiburi sana inaonekana,lakini aangalie sana,anawezapata pigo kubwa sana toka kwa Mungu kama amemdhuru mtoto wa watu
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Suala hili ni gumu na la hitaji njia za kidiplomasia katika kulifuatilia na kutafutai ufumbuzi wake.
  Tanzania
  Inawezekana kumvuta mkono huyu Grace aeleze alipo huyu msichana ili aisaidie polisi kupatikana alipo kwa vile ametoweka mikononi mwake huku ndugu wakitaka kujua aliko.​

  Marekani
  Umri wa msichana ni zaidi ya miaka 18 na hivyo kwa sheria za nchi hiyo hayuko chini ya malezi ya wazazi na yuko huru kutafuta hifadhi au kuchagua kwenda popote anapotaka mradi havunji sheria.​

  Kuna uwezekana huyu Grace alikuwa anamnyanyasa huyu msichana, kwa Marekani ukipata mwanya wa kumtoroka anayekunyanyasa ni haki yako inayolindwa ingawa vyombo vya dola vinaweza kujua wapi yupo ili mradi havunji sheria anabaki anatanua tu. Vinginevyo msichana angemfungulia madai Grace kumnyanyasa, angekuwa matatani, ashukuru msichana aliamua tu kumtoroka kwa sababu ya kutojua haki zake kisheria.

  Tunapojadili jambo hili tujue taratibu za nchi mbili tofauti zinavyotetea haki za binadamu na watoto, na pengine kukuta sheria zinazopingana kati ya nchi na nchi. Ndio maana nasema bora kuwe na njia za kidiplomasia katika kushughulikia shauri hili badala ya kuchukua mkondo wa sheria tutashtukia kugonga mwamba maeneo fulani ndio maana jambo hili linampa kichwa huyu mama.
   
 5. a

  assuredly4 JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 1,215
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  asije akawa amemuuza kama mtumwa kufanya kazi ktk makasino, madanguro nk? atueleze ukweli
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Msichana mwenyewe hana akili iliyokomaa vizuri, iweje apoteze mawasiliano na ndugu zake, jamaa na marafiki? Yakimpata matatizo nani atakayemsaidia?
   
 7. a

  assuredly4 JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 1,215
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  sio jambo jepesi kutoa uamuzi, mara nyingi watu wanapouzwa kama watumwa, wale wanaowauza huhakikisha hawana hata contact moja wala travel doc yoyote ili kuepusha kujulikana nn kimewatokea na wasaidiwe vp.
  pls take care
   
 8. Githeri

  Githeri JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 820
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Wanafanya vibaya sana wanaochukua watoto wa watu na kuwanyanyasa au kuwafukuza bila kujua hatima yao. Ila Mungu anawalipa hapa hapa duniani soon or later. Huyo balozi anajua ukweli
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Uuzwaji wa aina hii nchini Marekani kuna nafasi mtu ya kuchomoka kama alivyochomoka kutoka kwa yule mama. Maana mwaya ukiupata tu kimbilia polisi watasaidia kunyoosha mambo.
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Tatizo kama alitorokea kwa mwanaume mhamiaji mwenzake ambaya hata paper hapo ndo kazi ni maisha ya woga yasiyokifani, ni kubaki kama ulivyo kama huna mtu wakukusaidia kupata njia ya kujinasua.
   
 11. a

  assuredly4 JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 1,215
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  nashukuru kwa taarifa lkn mm nijuavyo jinsi watu wanavyochukulia na kuelezwa kwenda kutaafutiwa kazi huwa hawapati wasiwasi na watu wanaowachukua,\. na kweli wakifika huko huanza kufanya hizo kazi na kulipwa ujira lkn kadri muda unavyoenda bila wao kujua kinachoendelea huuzwa na kukabidhiwa kwa wamiliki. baada ya kuuzwa hunyangánywa passport na id zote na kufungiwa katika majumb amkubwa ambayo yako monitored na cctv. very few in rare occassion hufanikiwa kutoroka. lkn wengi wakitoroka wakikamatwa na polisi hufungwa ndipo hurudishwa kwao, wengi kwa kuogopa vifungo hubaki mtaani wakifanya kazi zao za ukahaba, na biashara ndogo ndogo za kujipatia kipato bila kujua wao watarudije tz. wale wanaosafiri sana canada, Ulaya na USA, wanaweza kuchangia mada hii kutupa uzoefu wa kina. pia wasiliana na IOM wana research kuhusu masuala haya na jinsi inavyokuwa ngumu kutoka baada ya watu kuuzwa wkati mwingine inalazimu polisi ijue na kuvamia majengo ndipo mtu hupata msaada
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nchi za Marekani, Canada na Ulaya biashara ya ukahaba kwa mhamiaji ni kitanzi ambacho ni kuishia jela na tuokapo huko ni kurudishwa ulikotoka kwa vile ni criminal case. Sijaridhika sana na hoja hii ya watu kurudi mitaani kufanya kazi ya umalaya hasa kwa wahamiaji.

  Ninachoweza kufahamu ni wengi wetu kujawa na woga ambao hawajiamini na kujua haki zao ambapo kama watakuwa open kwa vyombo vya sheria na haki za binadamu na kwa kuwa waliingia katika nchi hizo kihalali kwa visa, wanaweza kusaidiwa kupata haki za kujikimu kisheria kwa vile yaliyowakuta si makosa yao, Nchi hizi zina sheria za huruma kwa wahanga.

  Ninachoweza kuhisi kama wahanga wa aina hiyo wanakutana na wazamiaji, kwa vile wazamiaji na waliopitisha muda wa kukaa katika nchi hizo kisheria wamekiuka utaratibu kwa kutofanyia marekebishe hati zao za ukazi, basi wakikutana ni kudanganyana kwa kutoeleweshana haki zao. Watanzania wengi wana tabia ya wivu kama kuna uwezekano wa mwingine kufanikiwa, ni kubaki kutishiana na kukatishana tamaa, hivyo maisha ya woga na kuishia kufanya vibarua visivyo na tija kushika njia. Wanadiriki hata kukata mawasiliano na ndugu zao kwa kufikiria watalipuliwa waliko kosa ambalo mbele ya safari watalijutia.
   
 13. D

  Danniair JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu mama namfahamu vizuri sana. Ana majibu machafu mno. Huyu binti ni binti pekee aliyeishi naye kama H/girl kwa mda mrefu sana. Kwa mama huyu wasichana walikuwa hawakai. sisi tuliokuwa tukienda kula maeneo yale tunajua. Tukivyoulizia wenyeji mbona Binti huyu kadumu sana kwa mama huyu tuliambiwa kuwa alikuwa ni ndugu wa karibu mno, na kuwa wenye mtoto walimpa mwanao kwa masharti ya kuto mnyanyasa.

  Na binti huyu alikuwa ni mpenda watoto wa mama huyu sana sana, "Kwa mujibu wa majirani". Kwa suala hili yule binti wa Grace anaweza akatoa ukweli tupu juu ya Anneth kwani walishibana mno. Kuna wakati Anneth alitaka kuondoka, Lakini binti wa mama huyu alipinga vikali tena kwa kukataa kula.

  baada ya kwenda America, habari zilizorudi zilikuwa eti, Aneth aliolewa miezi 3 baada ya kufika huko!! Wengi walimpa hongera kwani Aneth ni binti mzuri mno na mpole sana. hata tembea yake inadhihilisha hayo. Na hivyo ni vigezo vya sisi kuwa tunamfuatilia kujua anatokea wapi na kwa nini ameweza kuvumilia kuishi na mama huyu.
   
 14. D

  Danniair JF-Expert Member

  #14
  Sep 16, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa kuwa nchi yetu inao uongozi, basi tunaomba rais ateuwe watu wa kufuatilia ni wapi raia wetu Anneth alipo.
   
 15. Chum Chang

  Chum Chang JF-Expert Member

  #15
  Sep 16, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,001
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Msichana ni mkubwa na swala lina ulakini haswa ukiangalia familia anayotoka

  Kwanza awezi kukaa sehemu asio kuwa na amani nayo (MDOMO WA MUAJILI WAKE HATA KIPIGO)

  Pili jamani jamani hii dunia ina mambo mengi sana sio kila mtu unaemuona ni binadamu wengine wanyama hawafai

  Tatu kama yuko hai basi mungu amlinde na siku moja ajikwamue na kuisaidia familia INSHALLAH
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kafika merekani kaingia mitini. Nini cha ajabu?
   
 17. Davie S.M

  Davie S.M JF-Expert Member

  #17
  Sep 16, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 720
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Binti 'Amejilipua' at least ata akatafuta ndugu zake...(Kama yupo Hai ama eneo salama )

  Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
   
 18. D

  Danniair JF-Expert Member

  #18
  Sep 16, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Usiseme hivyo hata kidogo. kwa mimi ninayemfahamu, yule binti hawezi kufanya hivyo. Huyu mama aseme Aneth yuko wapi? Hadhi ya kibalozi mtu huvishwa vile vile huvuliwa. Ebu rais wetu lipe jambo hili uzito mwingi. Mama huyu avuliwe u-diplomasia, tujue kwanza raia wa Tanzania (ANNETH) yupo wapi. Tukisha jua mvisheni tena.
   
 19. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #19
  Sep 16, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,531
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  Tumeegemea upande mmoja tu
   
 20. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #20
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Umeona ee, tangu awali nimetahadharisha jambo hili kuwa makini kwa sababu ni la kimataifa. Ingekuwa kitaifa ingekuwa vyema kumwandama mama, lakini kwa hali ilivyo kuna umuhimu wa kulifuatilia kidiplomasia ili wazazi na ndugu zake wajue yuko wapi. Suala lilipofikishwa vyombo vya usalama Marekani walijibiwa ni mtu mzima huenda yuko na bf wake, ukisikia hivyo hawa jamaa wanajua yuko wapi na anaishi na nani, ila huwa hawapendi kuingilia private ya mtu aliyekwisha vuka 18. Muhimu kutumia njia za kawaida kumtafuta aliko ili wazazi na ndugu wake wajue alipo ili kupata amani mioyoni mwao.
   
Loading...