Msiba

Duh pole sana kwa msiba huu wa ghafla hivi. Mnahitaji faraja toka kwa Mungu mwenyewe.
 
Poleni sana mkuu kwa msiba huo mzito. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi- Aaamin!
 
Mungu ailaze mahari pema peponi
roho ya marehemu, Yupo Yeye mfariji wa wanyonge,
naye atakutieni nguvu wakati huu wa majonzi,
 
Pole sana kwa msiba, mwenyezi mungu akupe wewe na familia yako nguvu na amani katika wakati huu mgumu wa msiba.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe - AMINA
 
Pole sana Meku! Roho ya marehemu ipumzike kwa amani, mwanga wa milele umuangazie, Amen!!
 
Ni tabibu wa karibu, tabibu wa ajabu.
Na neema ya daima, ni dawa yake njema.
Hatufai kuwa hai, wala hatutumai
Ila yeye kweli ndiye atupumzishaye.


Imbeni malaika siafa za Yesu Bwana
Peke limetukuka Jina lake Yesu x2


2) Dhambi pia na hatia ametuchukulia,
twenendeni na amani hata kwake mbinguni.

3) Uliona tamu Jina la Yesu Kristu Bwana
Yuna sifa mwenye kufa asishindwe na kufa.

4) Kila mume asimame sifa zake zivume
Wanawake na washike kusifu jina lake.
 
Pole sana ndugu yangu Mungu (Ruva) akupe nguvu kipindi hiki cha majonzi.
Na zaidi sana aipokee roho ya Marehemu peponi apumzike kwa amani-Amina.
 
Wapendwa Ndugu zangu. Mdogo wangu Amedeus atasafirishwa kesho jioni kuja Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi. Tutamchukua pale Mwananyamala saa nne asubuhi na kwenda pale nyumbani Kimara Temboni. Kutakuwa na ibada pale na kuaga pale nyumbani Kimara. Baada ya hapo msafara utaanza saa nane hivi. Mazishi yatafanyika nyumbani Kibosho siku ya Jumanne.
Tuombeane uzima.
 
poleni sana kwa msiba huu. mola awape faraja na nguvu katika kipindi hiki kigumu.
roho ya marehemu ipate pumziko la amani
 
Pole sana, Mungu akupe nguvu wewe pamoja na familia kwa ujumla katika kipindi hichi cha majonzi,

Inasikitisha sana kwa kweli..
 
Back
Top Bottom