Msiba wa Regia waibua mazito | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msiba wa Regia waibua mazito

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Jan 18, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Tuesday, 17 January 2012 21:27 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  [​IMG]

  Askari wa Bunge wakiwa wamebeba jeneza la aliyekuwa mbunge wa viti maalum (Chadema), Regia Mtema, wakati wa salamu na rambirambi za kumuaga rasmi kiserikali zilizofanyika viwanja vya karimjee jijini Dar es Salaam jana.Mbunge huyo anatarajiwa kuzikwa leo alasiri nyumbani kwao Ifakara mkoani Morogoro.Picha na Silvan Kiwale

  CHADEMA NUSURA WAZICHAPE MSIBANI IFAKARA, MBOWE AIPIGA SERIKALI KIJEMBE, MAKANI AANGUKA AKIAGA MWILI, KAFULILA AWA KIVUTIO

  Na Waandishi Wetu

  MAKUNDI mawili yanayopinga ya wanachama wa Chadema jana nusura yazichape kavukavu yalipokuwa katika msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kwa tiketi ya chama hicho, Regia Mtema huko Ifakara, kutokana na chuki na makovu ya uchaguzi wa wa ndani wa chama hicho wa mwaka 2010.

  Wakati hayo yakitokea huko Ifakara, jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitumia fursa aliyopewa wakati wa kuaga mwili wa mbunge huyo kuipiga vijembe Serikali huku Mwenyekiti Mstaafu wa chama hicho, Bob Makani akianguka ghafla.

  Marehemu Regia ambaye alifariki dunia Jumamosi iliyopita kwa ajali ya gari iliyotokea Ruvu, Pwani, unatarajiwa kuzikwa leo Ifakara.

  Katika tukio la Ifakara, mgogoro baina ya kambi mbili zilizotokana na makovu ya uchaguzi huo wa ndani kati ya wafuasi wa marehemu na ya Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Kiwanga ulisababisha kutimuliwa msibani hapo kwa Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kilombero, Salum Ngozi.

  Ilielezwa kwamba baada ya Ngozi kufika msibani hapo juzi majira ya saa moja usiku na kusalimiana na viongozi wa Serikali, alifuatwa na baadhi ya makada wa chama hicho wakimtaka aondoke eneo hilo jambo ambalo aliligomea. Wafuasi hao wa Chadema waliamua kutumia nguvu kumwondoa hali iliyowalazimu polisi waliokuwa eneo hilo kuingilia kati. Askari walimtoa mwenyekiti huyo na kumpeleka katika Kituo cha Polisi Wilaya.

  Hiyo ilikuwa mara ya pili kwa Ngozi kutimuliwa katika msiba huo. Mara ya kwanza ilikuwa juzi na kumlazimu Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Francis Miti kuingilia kati.

  Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, Ngozi alikiri kutokea vurugu hizo msibani na kudai kwamba, alifanyiwa fujo na kikundi cha watu aliowaita wahuni na kwamba amefungua kesi ya kufanyiwa vurugu katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Kilombero na kwamba baada ya kumalizika kwa mazishi atasimamia suala hilo ili haki itendeke.
  

  Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe mbali na kukiri kuufahamu mgogoro huo, alisema asingependa kuzungumzia suala hilo sasa wakati watu bado wanaendelea na msiba.

  Mbowe aipiga vijembe Serikali

  Jijini Dar es Salaam, tukio la kuaga mwili wa marehemu Regia liligeuka jukwaa la siasa baada ya Mbowe na Makinda kupiga siasa.Mbowe alitumia msiba huo kutoa dukuduku lake juu ya shughuli za chama chake kisiasa na kiutendaji wakati akitoa salaam za rambirambi kwa marehemu.Mbowe aliirushia kombora Serikali na vyama vingine vya upinzani kuhusu mwenendo wa Chadema kuendesha siasa katika vyuo vya elimu ya juu akisema ni mpango maalumu kuwanoa wanasiasa mahiri.

  Aliishauri Serikali na vyama vingine vya siasa kuiga utaratibu huo wa Chadema akisema unasaidia kukuza vipaji na kuwaandaa viongozi makini kwa kuwapa nafasi vijana kushiriki katika uongozi.

  "Kuna jambo moja ambalo ningependa Serikali, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyama vingine walitafakari na wasilibeze hili. Viongozi huandaliwa na viongozi makini hawazuki tu," alisema na kuongeza;

  "Naeleza hivyo maana mara nyingi tumekuwa hatueleweki na tumekuwa tukibezwa. Sisi tunatambua viongozi wa baadaye kisha tunakuza vipaji na kutoa fursa za nafasi za uongozi kwa vijana."

  "Vijana lazima waandaliwe kimaadili na ndiyo maana tuliingia vyuo vikuu lakini tukatafsiriwa kuwa ni wakorofi na wachochezi wa vurugu. Lakini leo tumepata viongozi wazuri vijana kwa njia hiyo kutoka vyuoni kama vile Mheshimiwa Zitto (Zuberi Kabwe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini), Mnyika (John Mbunge wa Ubungo, Mdee (Halima-Mbunge wa Kawe), Silinde (David Mbunge wa Mbozi) na Mtema (Regia Marehemu).

  "Hawa tuliwaandaa, hawakuzuka. Rai yangu kwa Serikali na kwa wazazi ni kwamba vijana hawa wakifanya siasa tusiwakwaze na kuwafukuza, bali tuwalee."

  Spika Makinda katika kile kilichoonekana kama ni kumjibu Mbowe, alitumia fursa hiyo kufafanua uendeshaji wa shughuli za Bunge akisisitiza kwamba linaendeshwa kwa kanuni na wala si kufurahisha watu.
  Alimsifia marehemu Mtema kwamba alikuwa akizijua vyema kanuni za Bunge: "Bunge huendeshwa kwa kanuni na si kwa matakwa tu ya kufurahisha watu. Yeye marehemu alizijua kanuni ndiyo maana hata wakati alipokuwa akikosea alikuwa tayari kuomba radhi."

  Mzee Makani aanguka
  Hata hivyo hafla hiyo iliingia dosari baada ya Makani kuanguka muda mfupi baada ya kuuaga mwili wa marehemu. Baada ya tukio hilo, alibebwa na kupelekwa pembeni ambako alipepewa kwa takriban dakika tano kisha kurejea katika hali yake ya kawaida na kurudi kwenye kiti chake.

  Baadaye Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia ambaye alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wakimpatia Mzee Makani huduma ya kwanza aliwaambia waandishi wa habari kuwa alianguka baada ya kuishiwa nguvu ghafla.

  "Sasa anaendelea vizuri na amerudi kushiriki kumuaga mpendwa wetu katika safari yake hii ya mwisho," alisema Mbatia.

  Kafulila ashangiliwa

  Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila jana alishangiliwa kwa makofi baada ya kutangazwa kuwa mmoja wa wabunge walioteuliwa na Ofisi ya Bunge kuwamo katika msafara kusindikiza msiba huo akiwakilisha chama chake.
  Baada ya kiongozi wa shughuli hiyo, Ofisa Mwandamizi wa Ofisi ya Bunge, Saidi Yakub kumtaja Kafulila baadhi ya waombolezaji walishangilia kwa makofi, vicheko vya chini kwa chini na minong'ono ya hapa na pale.

  Hatua hiyo ya waombolezaji inatokana na hali ya kisiasa ilivyo kati ya Kafulila na chama chake hicho ambacho mwishoni mwa mwaka jana kilitangaza kumvua uanachama hatua ambayo ameipinga mahakamani. Kama ikitekelezwa, itamvua ubunge.

  Imeandikwa na Venance George, Morogoro, Aziza Masoud na James Magai, Dar
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Jan 18, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  That is so beyond the pale. Shameful!
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  All crass, no class.
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hichi nacho ni nini?

  Mambo mengine aibu kabisa
   
 5. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2012
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Waandishi wengine wanakuza mno mambo... like in last para; anasema walipiga makofi, which is not true! Walioenda kuomboleza 'walinong'ona tu huku kukiwa na kicheko kile cha chini kwa chini, makofi kama alivyoandika hayakupigwa!!
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Jan 18, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,572
  Likes Received: 18,349
  Trophy Points: 280
  Lets hope siasa hizi za msiba huu zitaishia Dar, leo huku mazikoni kazi iwe ni moja tuu, kumpunzisha Regia katika pumziko la amani kwenye makao yake ya milele ya muda tuu wakati akisubiria ufufuko wa miili na kuelekea kwenye uzima wa milele yote ijayo!.
  Rip Regia.
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Jan 18, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  What is this now!
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,572
  Likes Received: 18,349
  Trophy Points: 280
  Steve, kwa vile watu walikuwa wengi makofi yalipigwa!. Hata wakati Kafulila inaingia kwenye gari yake akiwa amekaa siti ya mbele ya abiria, alipunga mkono na umati wa washangiliaji walimshangilia tena huku wengine wakinyanyua mikono na wengine wakipiga makofi!.

  Hali niliyoiona jana pale Karimjee ni as if kulikuwa na kikundi kisicho rasmi cha washangiliaji wa ile dizain ya mikutano ya CUF!. Na kwa jinsi nilivyowaona washangiliaji hao, nadhani wako njia moja mpaka mazikoni!.
  Note: mikusanyiko yoyote yenye vijana wenye mwamko ni rahisi kuhamanika na kuonekana kama washangiliaji!.
   
 9. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #9
  Jan 18, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Wanajaribu kunogesha habari.

  Ila hiyo habari ya kufukuzana msibani inashangaza.
   
 10. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #10
  Jan 18, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Pasco,

  Mkuu na wewe umeanza siasa msibani kama alivyofanya mwenyekiti wangu na madam spika? lol

  Kusema kwamba chadema ilipeleka kikundi cha washangiliaji karimjee utakuwa unatukosea adabu mkuu. Otherwise itabidi ututhibitishie pasi na shaka kwamba chadema ilipeleka hicho kikundi. Jina la Kafulila lilipotajwa kwamba anakwenda ifakara kama mbunge wa nccr mageuzi watu walinong'ona tu na miguno ya hapa na pale, wala hakukuwa na kushangilia ama kupiga makofi. Makofi yalipigwa katika matukio mengine, sio kwa kumshangilia Kafulila!!


  Nakumbuka wakati msafara unaondoka na yeye kuwapungia watu waliokuwa wamesimama pembeni ndipo nao wakampungia huku wengine wakimbeza kwamba ni mbunge wa mahakama!! Nadhani ni vizuri tukawa wakweli wakati huu tunapomsindikiza mpendwa wetu katika makazi yake ya kudumu hapa duniani.
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #11
  Jan 18, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,572
  Likes Received: 18,349
  Trophy Points: 280
  Mwita, naomba msamaha in a sense kuwa sio Chadema ilioleta kikundi cha washangiliaji as an organized group bali kulikuwepo genge la vijana wenye sare na scuf za chama fulani, ambao hata wakati wa kuondoka wakiwa kwenye mini bus iliyoshehenezwa bendera za chama fulani walikuwa wanashangilia huku wakishangiliwa!.

  Makofi au no makofi depends umesimama wapi!. Kwenye kundi la waombolezaji 1000 plus, no one can see everyone everything, the cameras ambazo zimerecodi everything can see more than eyes can see, ukiona vipi tunaweza kwenda next stage!. Nikirudi naweza kureview footage hili la makofi tukalimaliza!.
   
 12. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #12
  Jan 18, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  mmesomeka; mbarikiwe.
   
 13. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #13
  Jan 18, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Haya mkuu Pasco,

  Naona umeamua kusimama pale pale kwa style nyengine. Tuendelee na mambo mengine kwakuwa uwanja wa karimjee ni mkubwa na si rahisi kuona ama kushuhudia kila kitu ingawa ni vigumu vitendo vya kushangilia ama kupiga makofi kufanyika kimya kimya.

  Wengine tulikuwa tuna move around kwahiyo tulifanikiwa kushuhudia matukio mengi mkuu, au nikwambie nilikuwa pembeni yako wakati unaongea na yule mama nanihino mkuu wa mkoa!! lol
   
 14. The Stig

  The Stig JF-Expert Member

  #14
  Jan 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 882
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80
  Gazeti gani hili lisilo na staha?
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Jan 18, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,572
  Likes Received: 18,349
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mwita, nimekubali yaishe. Kumbe ulikuwepo pale nilipokuwa nasalimiana na yule mama kasuku?!.
   
 16. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #16
  Jan 18, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mh magazeti njaa yanayotafuta kula. Habari gani hii? Kwani ni ajabu kwa mtu kuanguka ktk mcba wa mtu ampendae?! Mbona wanaitaka kuisiasalize hii issue ya Mzee Makani?

  Hao waliomfukuza huyo mpinzani wa marehemu nao hawajakomaa kisiasa.Unless kuwe na ya ziada kati yake na marehemu!

  Rest In Peace Shujaa wetu.
   
 17. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #17
  Jan 18, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huyo mwandishi ni mfuasi wa kafulila, usishangae
   
 18. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #18
  Jan 18, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  chama fulani ndiyo chama gani tena ??
  wengine htupo msibani tunategemea JF mtuteletee habari " and here we dare to talk openly " otherwise CDM wanaleta aibu kwa kugombana msibani
   
 19. Blandes

  Blandes JF-Expert Member

  #19
  Jan 18, 2012
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  ubishi sio nzuri,makofi yaligwa mi nilikuwepo bhana
   
 20. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #20
  Jan 18, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Tabia ni kama ngozi, haivuki. Si ajabu marehemu hakuwa na tatizo na huyo shosti, wapambe tu wanajitutumua kuonyesha majonzi ya ziada.
   
Loading...