Huyu ni baba yake Susan Mzee aliyepo UK.Pole Susan,mdogo wako Charles pamoja na wanafamilia wote.He was a great person.We will definetly miss him.Wanajamvi,
KWa huzuni kubwa napenda kuwaarifu msiba wa Prof Samuel Stephen Mushi, mwalimu wa muda mrefu wa Idara ya Sayansi na Elimu ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam. Itakumbukwa kuwa Prof Mushi amewahi kutoa mchango sana katika masuala ya Siasa akifundisha, pia akitoa ushauri wa mambo mbalimbali yahusuyo siasa ya Tanzania. Mara ya mwisho kumuona alikuwa akitoa maoni katika kituo cha Television juu ya Rostam Azizi na CCM kujivua gamba.
Msiba upo kwake Regent Estate njia ya kwenda Mikocheni Hospital nyumba ya 3 kulia baada ya kuingia lami ya kwenda hospital ukitokea Victoria.
Mimi binafsi nimegwaya, nimeguswa na kuhuzunishwa sana na msiba huu.
Nawasilisha!