Poleni sana,
Msiba huu umenigusa sana,maana huyu Prof.S.S.Mushi alikuwa mwalimu wangu nilipokuwa ninasoma pale UDSM kwenye miaka ya 1999,na pia ninamshukuru Mungu leo tarehe 27.07.2011,Mungu alinipa neema ya kuhudhuria na kutoa heshima zetu kwa mwanazuoni huyu mahiri,wageni mashuhuri waliokuwepo ni Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Rais Mstaafu Mkapa na waziri Mkuu mstaafu Fedrick Sumaye,pamoja na wahadhiri waandamizi mbalimbali,kweli ilikuwa ni huzuni kubwa,na nilipata nafasi ya kutoa mkono wangu wa pole,kwa mjane wa Prof.Samuel S.Mushi na watoto wake.Mazishi yatafanyika Bunju mahali iliko shule yake inayoitwa Dar es salaam Prime Secondary school,
Bwana alitoa na bwana ametwaa jina la Bwana lihidimiwe.R.I.P Prof. S.S .MUSHI .Amen