Msiba wa Mama yake Askofu Mwamakula wapandisha Joto la Kisiasa Kyela

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,741
218,332
Bado sijafahamu sababu hasa za Wanasiasa kujazana kwenye Msiba wa Bibi yule, ambaye yeye mwenyewe hakuwa Mwanasiasa.

Bali nadhani uwepo wa Mtoto wake, mpigania haki Emmaus Bandekile Mwamakula yaweza kuwa chanzo cha kujazana kwa wanasiasa kwenye msiba huo wa mkulima mdogo wa Kijiji cha Itunge.

Sijui kama walialikwa ama la , Lakini ccm ndio waliokuwa wa kwanza kutoa salamu zao kwenye msiba huo, wakiongozwa na Diwani wa eneo hilo pamoja na Mwakilishi wa Mbunge, kama kawaida ya ccm wakaleta porojo zao za ujenzi wa barabara kutoka Community center hadi Itunge, jambo ambalo lilizua zogo msibani hapo, hii ni baada ya Waombolezaji kutokuwa na imani na CCM, wanadai porojo hizo ni za kila mwaka.

Kazi ikaanza baada ya Wawakilishi wa Chadema, ambao ni Mwenyekiti wa Mkoa wa Mbeya, China wa China na Twaha Mwaipaya kutoka Bavicha Taifa, baada ya hawa kupewa kipaza sauti Msiba ukageuka kuwa Shangwe, walipangua uongo wote wa CCM, hakika Chadema Kyela ina watu.
 
China wa China: Mimi na kaka yangu Kinanasi tunashirikiana sana Hata Ule mkataba wa DP World aliniahidi atakuja Kutoa ufafanuzi Jimboni 😄🔥
 
Bado sijafahamu sababu hasa za Wanasiasa kujazana kwenye Msiba wa Bibi yule , ambaye yeye mwenyewe hakuwa Mwanasiasa.

Bali nadhani uwepo wa Mtoto wake , mpigania haki Emmaus Bandekile Mwamakula yaweza kuwa chanzo cha kujazana kwa wanasiasa kwenye msiba huo wa mkulima mdogo wa Kijiji cha Itunge.

Sijui kama walialikwa ama la , Lakini ccm ndio waliokuwa wa kwanza kutoa salamu zao kwenye msiba huo , wakiongozwa na Diwani wa eneo hilo pamoja na Mwakilishi wa Mbunge , kama kawaida ya ccm wakaleta porojo zao za ujenzi wa barabara kutoka Community center hadi Itunge , jambo ambalo lilizua zogo msibani hapo , hii ni baada ya Waombolezaji kutokuwa na imani na ccm, wanadai porojo hizo ni za kila mwaka.

Kazi ikaanza baada ya Wawakilishi wa Chadema, ambao ni Mwenyekiti wa Mkoa wa Mbeya, China wa China na Twaha Mwaipaya kutoka Bavicha Taifa , baada ya hawa kupewa kipaza sauti Msiba ukageuka kuwa Shangwe, walipangua uongo wote wa ccm, hakika Chadema Kyela ina watu.
Askofu Mwamakula pekee ndiye aliyefurukuta kuandamana kipindi Cha jiwe.

BAVICHA walikuwa wapi sijui.
 
Mnatia huruma sana Rafiki yangu kwa sasa katika siasa za nyanda za juu kusini. Mmebaki mnavizia misiba ndio mkatoe hotuba? Hivi kweli CHADEMA ni ya kusubiri misiba ili ikaeleze sera zake? Badala ya kuhuzunika na kutoa faraja kwa mfiwa na kumtia nguvu na moyo nyie mnaleta porojo zenu za uongo uongo tu. Subirini uchaguzi uwadie hapo mwakani ili mpigwe kipigo kizito katika sanduku la kura.
 
Mnatia huruma sana Rafiki yangu kwa sasa katika siasa za nyanda za juu kusini. mmebaki mnavizia misiba ndio mkatoe hotuba? Hivi kweli CHADEMA ni ya kusubiri misiba ili ikaeleze sera zake? Badala ya kuhuzunika na kutoa faraja kwa mgiwa na kumtia nguvu na moyo nyie mnaleta porojo zenu za uongo uongo tu. Subirini uchaguzi uwadie hapo mwakani ili mpigwe kipigo kizito katika sanduku la kura.
Umeelewa uzi kweli ?
 
Back
Top Bottom