Katibu wa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo CCM Paul Makonda ameahirisha ziara yake ya Mikoa 20 Back to Back ili kushiriki msiba wa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa aliyefariki jana katika Hospital ya moyo ya JKCI Jijini Dar es salaam.
Akizungumza mjini Songea Mkoani Ruvuma Makonda amesema kama chama kimeona kisitishe ziara hiyo iliyoifikia mikoa 18 ili kumpa heshima kiongozi huyo ambaye ametoa mchango mkubwa katika kuliletea taifa maendeleo.
"Dhamira ya CCM na Rais Dk Samia Suluhu Hassan ni kuona wananchi wanatumaini jipya, watendaji wa umma wanawajibika, heshima ya chama inarudi, ila kazi alizofanya, michango mbalimbali aliyotoa kwa taifa hana budi kupewa heshima zake za dhati", amesema Makonda.
Ziara katika mikoa ya Mtwara na Lindi itapangwa wakati mwingine hivyo wananchi wamikoa hiyo wameombwa kuwa na subira kutokana na msiba huu ambao taifa umeupata.