Msiba wa Daudi Mwamgosi: Kinachojili Itete, Tukuyu katika mazishi yake

inauma, na mungu hawalaani waliofanya kitendo hiki, ni wajibu sasa kwa serikali kuchukua jukumu zima la kulea familia hii, hasa kwa kuwasomesha watoto wa marehemu, wasikae kimya kama hawajui walilofanya, rip daudi mwangosi, mpiganaji wa haki za wanyonge.
 
Nimepata taarifa kuwa Mhe. Mwandosya amejtolea kuwasomesha watoto wa marehemu.

That is secondary, his and his party's primary responsibility was to make sure that all citizens are safe and that the kids remained with both their parents, there is no reason for the murder of their father by Police for such flimsy excuses. Hii huruma yao/yake "is cosmetic". Ni sawa na yule marehemu Ali wa Morogoro waliyetorosha mwili wake na kwenda kuzika kwa haraka haraka huko Tanga. Kwao siasa za chama ni muhimu kuliko maisha ya wananchi. Ndio maana tumefika hapa tulipo.
 
Oh Poleni sana: mjane, ndugu, marafiki, wapenzi wa mageuzi nchini, waandishi wa habari, na wananchi wote. Ni simanzi kubwa, na aibu kuu kwa taifa letu.
 
RIP Kamanda.

Vipi mipolisi na mapolisi hayakuzuia mkusanyiko maana ni wakati wa sensa?

Mwandosya hapo anawakilisha kijani?
Marehemu nasikia alikuwa ni Mfuasi Mzuri wa CCM... Polisi hawakulijua hili ila Watu wa Mbeya Wanalifahamu Sana Hata Mwandosya Ukimuuliza analijua na Mimi kuna Mchizi wangu ni wa Huko Mbeya anaujamaa naye Marehemu anasema Marehemu alikuwa Mfuasi Wa CCM ...

Mara zote CCM Wakicheza Miziki yao Dua baya linawarejea Wenyewe nashauri Waache kwani Siku walizotawala mbona Zinatosha hawawezi kulazimisha Kutawala watu wasiowataka Alaaa!
 
inauma sana, amwandsya awaache tu,

wakasome shule zipi? atawapa kazi

ipi baada ya kuhitimu? ukoloni mambo

leo huo,,
 
Jamani Tanzania inakimbilia kuzimu. Raisi anazika Ethiopia kweli? Akimaliza ataenda kushangaa ndizi, kahawa, au hata maembe yao kwani Tanzania hakuna kitu.
Jamani tuamke toka kwenye huu usingizi na tuache kabisa kubezana kwenye hi mitandao. Hawa polisi hawataacha kutuua kwani halipo linalofanyika. Hii serikali yetu imefilisika kiasi cha kutisha.
Daudi alikuwa mzima salimini na mara baada tu mawasiliano na huyu mkuu wa mapolisi amelipuliwa kama ndege. Je RPC alipata wapi kibali cha kuagiza mauwaji ya raia? Hivi tutalala na kulia hadi lini? Hawa polisi si tunawaona kwenye picha? Huyo aliyewapa wao mamlaka ya kufanya hiki walichokifanya ametunyima sisi mamlaka hayo? Na jeshi mshahara wa polisi unatoka wapi? Kama ni kwa walipa kodi je hao walipa kodi watatoka wapi kama wanatunguliwa na kulipuliwa kama wanyama wa msituni? Je tunatozwa kodi kulipia silaha za ulinzi wa taifa au za kutulia?
Je hawa polisi watamtunza mjane huyu masikini na watoto wake? Je huyu RPC ameshawajibishwa kwa namna yeyote ile? Je hawa polisi wamefikishwa kwenye vyombo vya sheria?
Watanzania tunaadhirika vibaya sana na matukio haya. Yanatuafeckt kisaikologia, kiroho, kiakili na kimwili. Kuendelea kuwaacha hawa polisi waende katika mwendo huu si sawa. Ni vyema serikali hii iliyojidhihirisha kwa kila jambo kuwa DHAIFU ichukue hatua. Poleple mto unatiririka, na hatimae utafurika damu hii inayomwaga kila siku na Kikwete hataweza kuuzuia hata akiomba na polisi toka nchi za ulaya.
Wapendwa tuamke. Tena tuamke mapema kukiwa asubuhi tuzuie rushwa, kubambikiwa makesi yaliyofanywa na polisi, mauwaji na mengine. Tufanye haya kwa vitendo hata kama ni kuiondoa hii serikali madarani basi tufanye vile.
 
Kila mtu ataionja mauti,lakini this was realy unneccessary!Nimetizama picha hizi,sikumfahamu huyu mtu,lakini nimejikaza nisitoke machozi!This was unneccessary,ni kile kitendo tulichokiona kwenye picha,kitendo cha kinyama!Hizi yule mnyama ana familia?ana mke?ana watoto?ni lazima haki ipatikane,ni lazima!
 
Duh kamanda unastahili pongezi na shukrani kubwa sana kwa jinsi ulivopangilia picha kwa mtiririko wa matukio, ubarikiwe sana na pia R.I.P MPENDWA WETU DAUD MWANGOSI, UPUMZIKE KWA AMANI!!!
 
mwenye contacts za ndugu wa marehemu naomba wanijuze nami nimsomeshe mtoto mmoja mpaka upeo wa uwezo wake tafADHALI.
 
RIP mpiganaji. Naona Polisi wamegoma kuhudhuria msibani. Hili ni jibu la maswali mengi.
 
Thanx for the update.
======================

Tokana na wingi wa picha Update zote zimewekwa mwanzo wa habari ili kuhakikisha ujumbe unasomeka kwa wote
wenye niya ya kutambua nini kinaendelea katika msiba wa Marehemu D. Mwambosi

========================




IMG-20120904-WA009.jpg


Wawakilishi Mbalimbali wakitoa salam za Pole kwa ndugu wa Marehemu


Mwakilishi wa Chanel Ten Hamis akitoa pole katika msiba huu muda huu






Mwenyekiti wa Mbeya Press Club akitoa pole zake kwa wafiwa


Mwanaharakati Francis Godwin akielezea Jinsi Mauti yalivyo mkuta Mwandishi wa Habari Daudi Mwangosi






Rais wa UTPC Kenny Simbaya ambaye pia ni kiongozi wa msafala wa kuleta Mwili wa Marehemu Daudi Mwangosi akiwa anatoa salam za Pole kwa wafiwa.


Dr Slaa akitoa pole kwa wafiwa wote Muda huu










Wakina mama wakiwa wenye majonzi makubwa sana na huzuni muda huu

Mke wa Marehemu Daudi Mwangosi akilia kwa Uchungu Muda huu

Maelfu ya watu wakiongezeka kuja katika Mazishi ya mwandishi wa habari wa Chanel 10 Daudi Mwangosi Muda huu

Mheshimiwa Mark Mwandosya ambaye ni Waziri ofisi ya Rais na pia Mbunge wa Rungwe Mashariki akitoa salam kwa Niaba ya Serikali

Watu wakiwa wengi na wenye utulivu wakisikiliaza watu mbalimbali wakitoa salam zao kwa ndugu wa Marehemu

Mjane Mke wa Marehemu Daudi Mwangosi aliye jishika, akiwa na uchungu muda huu




Ibada ikiwa inakaribia kuanza

Ibada ya mazishi ndio imeanza muda huu

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa wenye majonzi Makubwa

Waandishi wa Habari wakiwa katika msiba wa kwanza kutoka kulia ni Ndugu Joseph Mwaisango ambaye ni mwandishi mkuu wa Mbeya yetu Blog, Rais wa UTPC Keny Simabaya, pamoja na Felix Mwakyembe .


Endelea kufuatilia Moja kwa moja hapa


PICHA ZOTE NA MBEYA YETU BLOG

Updates; Forever Bold, RIP D. M, Tuonane Mtoni Mkuu!!



Waandishi wa Habari wakiwa wamebeba Mwili wa Marehemu kuelekea Makabirini

Wakiwa wanafanya ibada ya Mwisho kabla ya kuanza maziko

Hapa wakiwa wanashusha mwili wa marehemu katika Nyumba yake ya milele

Mwili wa Marehemu Daudi Mwangosi ukiwa Tayari katika Kaburi

Shughuri za kuzika zimeanza

Mazishi yanaendelea

Mke wa Marehemu Daudi Mwangosi akiweka Shada la Mauwa kwa machungu

Mke wa Daudi Mwangosi akiwa analia kwa uchungu katika Kaburi la Marehemu Mumewe

Watoto wa Marehemu wakiwawanaweka mashada ya maua sasa

Ni ngumu sana Kuamini kwa mke wa Marehemu lakini hali ndivyo ilivyo kuwa akiwa na huzuni kubwa

Dr Slaa akiweka Shada la Mauwa

Dr Slaa Baada ya kumaliza kutoa heshima za mwisho

Mh. Mark Mwandosya akiweka Taji la maua pamoja na mke wake

Rais wa UTPC akiweka shada la Maua
Ndugu wa Marehemu akiweka shada la Maua

Mwenyekiti wa Mbeya Press Club akiweka shada la maua


Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu, Ndugu Joseph Mwaisango akiwa anatoa heshima zake za Mwisho katiaka Kaburi

Wananchi wakiwa wanarejea baada ya mazishi

Waandishi wa Habari wakichukua Tukio Live `

Na huu Ndio Mwisho wa tukio zima la Mazishi ya Ndugu yetu, Mwanaharakati, Mpiganaji Daudi Mwangosi aliyekuwa Mwandishi wa Chanel 10.


 
Dah, insikitisha sana, familia imebaki ya kipweke sana, tuliofiwa na wazazi angali tupo wadogo, tunajua adha ya kutokuwa na wazazi/mzazi, ni shida kubwa. RIP mpiganaji, tunakuombea kwa Mungu na pia familia iweze kupata misaada ya kujiendeleza sana sana ki-elimu japo pengo halitazibika kamwe!
 
Kamanda Kiganyi,

Nimeshuka na picha moja baada ya nyingine kwa utulivu wa hali ya juu - japokuwa kimwili sikuwa Itete lakini kifikra ni kama nilikuwa pale - Ahsante kwa kutuwakilisha - Damu na udhalimu aliofanyiwa ndugu yetu, mtanganyika mwezetu, mpiganaji mwenzetu, mlipa kodi na mjenga nchi mwenzetu, na wale wote waliotangulia mbele ya haki kwa staili hii ya uuaji wa kinyama - KAMWE HAITAPOTEA!!!
 
Labda waliogopa kutolewa kafara, si unajua migombani?

Kamanda Mestod,

Si rahisi katika tukio kama hili WAUAJI na serikali yao kuhudhuria - hata Mwandosya hakuhudhuria kama mwakilishi toka serikalini - bali kama mnyakyusa, mwakilishi wa wananchi wa Rungwe ambako Marehemu Mwangosi ni eneo lake, na pia kama mwathirika wa kuuawa kisayansi na serikali yake mwenyewe, - kwa kweli anaoneka na mzima kwa kumuangalia lakini ndugu zanguni tumuombe Mungu ndugu yetu Mwandosya BADO MGONJWA!!
 
Kamanda Mestod,

Si rahisi katika tukio kama hili WAUAJI na serikali yao kuhudhuria - hata Mwandosya hakuhudhuria kama mwakilishi toka serikalini - bali kama mnyakyusa, mwakilishi wa wananchi wa Rungwe ambako Marehemu Mwangosi ni eneo lake, na pia kama mwathirika wa kuuawa kisayansi na serikali yake mwenyewe, - kwa kweli anaoneka na mzima kwa kumuangalia lakini ndugu zanguni tumuombe Mungu ndugu yetu Mwandosya BADO MGONJWA!!

Nimeshaanza kuonesha chuki binafsi kwao, kuanzia leo hata wale niliokuwa nawapa lift nawachunia tu. Unaweza wapa msaada wa usafiri, wanaposhuka wanakutupia bomu, hawa si salama tena.

'Be careful, police ahead of you'.
 
Nilikuwa nikufuatilia ITV habari jana usiku - kauli ya kiongozi wa kidini akikemea dhidi ya udhalimu wa mauaji ya watanganyika wenzetu ilinitoa machozi tena kwa mara ya pili - mchungaji alipanda juu na kukemea ".. HII HALI MPAKA LINI?" - hapa alinifungua macho kuwa "SAA YA UKOMOZI NI SASA" na sio kusubiri mapaka 2015. Mtikila uliyekuja na mbiu hii ya "SAA YA UKOMBOZI NI SASA" upo wapi. Tunafikiri mbio yako imefika mahala sitahili
 
Back
Top Bottom