Msiba wa Daudi Mwamgosi: Kinachojili Itete, Tukuyu katika mazishi yake

Utakumbukwa daima kwa msimamo wako dhidi ya udhalimu umekufa umesimama hujawahi kumpigia goti dhalimu yeyote.
RIP mpiganaji David
 
RIP Mwangosi!Mungu akupe pumziko la milele...ila hakika damu yako itawalilia milele!
 
Tangulia kamanda, damu yako haijamwagika bure, itachipua ukombozi na uhuru wa kweli, itaondoa udhalimu, tangulia, nenda!!!
 
Ukombozi wa mwanadamu siku zote haujawahi kuwa rahisi na mara zote umehusisha umwagikaji wa damu.
In other words,ukombozi ni mchakato na katika huo mchakato matukio kama haya hutokea,Mungu ailinde familia yako Mwangosi na akuinulie ukumbusho wa kazi yako uliyoifanya katika nia njema ya kuwapatia watz habari zisizoghushiwa.
Umechangia sana ukombozi wa nchi yetu ndidi ya wadhalimu,wabinafsi,wauaji,wapenda madaraka na utukufu wa binadamu na ambao wako tayari kuutafuta kwa gharama yeyote hata kwa damu ya watz kama wewe Mwandosi...

Hata hivyo myaonayo haya yanatukia,jueni kuwa ukombozi wenu unakaribia...
Hii ni ishara ya uchungu mithili ya uchungu wa mwanamke anayekaribia kujifungua,maana ni dhahiri kabla mtoto hajazaliwa utungu huja,ndivyo hivyo hivyo kuwa kwa tanzania huru na ya haki,lazima matukio kama haya yatokee.
Eee Mwenyezi Mungu tusaidie.....
 
Tunaanza kuzalisha kizazi chenye chuki na visasi ndani ya nchi yetu na hii ni hatari sana!!!Hakuna mtu anayeweza kuvumilia baba yake kuuawa kinyama namna ile bila kosa lolote.

Hii ni Kweli kabisa....cjui hakuna watu wanaoweza kuliona hili?
 
R.I.P Mwangosi kwa damu yako iliyomwaka cdm haitaonewa tena .tutakukumbuka jina lako siku ya Uhuru wa pili.kama moja wa mashuja wa nchi hi .amen
yap kamananda,jina lake litatajwa miongoni mwa mashujaa katika siku hiyo ya kushukuru Mungu na kuwaenzi mashujaa( Thanks giving and heroes day).siku hiyo itakuwa public holiday na siku kubwa mno kwa wazalendo wa nchi hii.wajane,wagane,watoto na wajukuu wa mashujaawatoka mbele kupokea nishani za ushujaa(PRIZE OF VALOUR) kwa niaba ya wapendwa wao!nami hata kutoka kaburini,nitaungana na watakaokuwepo wakati huo kushukuru, na kuwaenzi mashujaa
 
yap kamananda,jina lake litatajwa miongoni mwa mashujaa katika siku hiyo ya kushukuru Mungu na kuwaenzi mashujaa( Thanks giving and heroes day).siku hiyo itakuwa public holiday na siku kubwa mno kwa wazalendo wa nchi hii.wajane,wagane,watoto na wajukuu wa mashujaawatoka mbele kupokea nishani za ushujaa(PRIZE OF VALOUR) kwa niaba ya wapendwa wao!nami hata kutoka kaburini,nitaungana na watakaokuwepo wakati huo kushukuru, na kuwaenzi mashujaa

maneno mazito mkuu wangu.
 
serikali ya ccm na polisi ni JANGA LA KITAIFA haiwezekani ikawa inaua raia kwa lengo la kuwatisha wasikubali mabadiliko yanayoendelea nchini kwa sasa na kwa lengo la kuichafua CHADEMA mbele ya jamii
 
Mke wa marehemu akikumbatia kaburi la mpendwa mumewe. Asubuhi juzi mumewe alimwaga anakwenda kazini.
Mjane na watoto wanataraji atarudi na mkate wa siku kupitia kalamu na kamera.
Jioni wanakumbuna na kisichoelezeka. Leo wapo wenyewe hawajui watasimama wapi.
Maisha katika saa 72 yamebadilika ghafla. Inauma, initia uchungu sana!

Nchimbi anaunda tume marehemu akiwa ameshazikwa. Mtaalamu wa mabomu anaenda kuchunguza kisichokuwepo.
Polisi waliofanya uhalifu wapo mbele ya TV wakishuhudia mke na watoto wa marehemu wanavyokwisha kwa kusononeka.

Leo tumeona haya, hatujui kesho ni kwa nani yarabi!
Tukibaki kutuma rambi rambi wataendelea kutufanya vibwengo, vicheche wa kutunguliwa na risasi, wanyama wa kulipuliwa na mabomu. Wakati umefika, wakati tunasema RIP Mwangos sisi hatuna nafasi ya ku-rest.

Tupeleke ujumbe kwa Mwema, Nchimbi na JK kuwa sisi ndio wenye nchi.
 
kuondokewa na mume pia baba ni pigo sana kwa familia ya Daudi. Kweli ni majonzi sana kufikiria jinsi alivyokutwa na mauti, sasa familia yake imebakia wapweke milele bila yeye. Haki hamna kabisa Tz. RIP Daudi!!
 
R.I.P MWANGOSI Njia yetu ni 1 tutakutana Paradiso na wauaji nao hawatakwepa mauti
 
Back
Top Bottom