Msiba wa Daudi Mwamgosi: Kinachojili Itete, Tukuyu katika mazishi yake

What do you mean?? Amiri Jeshi Mkuu or??

That what i mean mkuu,huyu amiri jeshi mkuu yupo kimya wakati raia wake wanauwawa bila hatia tena wanaowaua ni moja ya chombo chake kinachopaswa kutulinda!
 
CDM wajue matukio haya yanatokea chini ya harakati za ukombozi zinazoongozwa na wao.
Wakitusaliti,tutawaua! Inauma kuwapoteza wapendwa wetu wanaounga mkono vuguvugu la mabadiliko. CDM wakitusaliti tutawaua!

R.I.P Daudi.
 
isiishie kusomesha watoto tu, na kuwa fariji iwe ni jambo lingine, watoto wanahitaji mtu atakaye onyesha mapendo kwao
 
RIP kamanda. May ur shed blood be the need ammunition to bring the end of a tyrant ccm rule. May u children live in a better Tanzania with an open democracy resulting from your shed blood. May ur blood not have been shed in vain.
 
Kiukweli inasikitisha sana kuona na kuamini Kama kweli ndugu yetu hatunae tena,tumshukuruni Mungu kwa kila jambo na tukumbuke mwanadamu aliezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi hapa duniani ni chache.Ee mwenye enzi Mungu wetu wa mbinguni mpokee mtumishi wako Daudi Mwangosi na raha ya milele umpe ee bwana apumzike kwa amani amen.
 
poleni wana familia na waandishi wa habari wote, ila waandishi wa habari
 
RIP Kamanda, damu yako ivuruge CCM, na wauane wenyewe kwa wenyewe,
polisi kamwe hatapanda gari langu kwa unyama huu!!!!!!!!!!!! akiomba lift namwambia uliye muua ndo angekupa lift
 
Anayesema hii serikali ni sikivu na ajitokeze mbele,
anayesema polisi hawana double standards na anyooshe mkono,
anayesema Tanzania kuna uhuru wa habari na aseme sasa,
anayedhani polisi hawajatumwa na atupe maelezo ya kutosha.

Hii kitu inauma,.
ANAYESEMA TANZANIA NI NCHI YA AMANI NA AONGEE SASA!
 
saidi mwema kazi imeshamshinda, HE MUST GO, hakuna haja ya serikali kuunda tume ni kupoteza muda.
 
Pole sana kamanda DM kapumzike kwa AMANI.Jamani mimi nilidhani hapo ndio Kamanda Kamhanda angekuja kuwatawanya waombolezaji kwani hao niwengi kushinda waliokuwa Kule Nyololo wasije haribu Sensa.
 
Wakiongea kwenye mazishi ya mwandishi wa habari aliyeuwawa na polisi.kwa nyakati tofauti Mbunge wa Rungwe Profesa MARK MWANDOSYA na Katibu mkuu wa Chadema Dk W.P.SLAA wameahidi kuwasomesha watoto wa marehemu Daud Mwangosi.
Akianza Prof Mark Mwandosya amesema anajitolea kumsomesha mtoto wa kwanza alie kidato cha nne mpaka chuo kikuu.
Naye katibu mkuu wa Chadema amesema kwa kuanzia wameshatoa kiasi cha fedha na vile vile wameahidi kumsomesha mtoto wa pili ambaye sasa yuko darasa la saba.
Source; Eborn Fm

Mke wa Marehemu Daudi Mwangosi akilia kwa Uchungu Muda huu

Maelfu ya watu wakiongezeka kuja katika Mazishi ya mwandishi wa habari wa Chanel 10 Daudi Mwangosi Muda huu

Mheshimiwa Mark Mwandosya ambaye ni Waziri ofisi ya Rais na pia Mbunge wa Rungwe Mashariki akitoa salam kwa Niaba ya Serikali

Watu wakiwa wengi na wenye utulivu wakisikiliaza watu mbalimbali wakitoa salam zao kwa ndugu wa Marehemu

Mjane Mke wa Marehemu Daudi Mwangosi aliye jishika, akiwa na uchungu muda huu


Ibada ikiwa inakaribia kuanza

Ibada ya mazishi ndio imeanza muda huu

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa wenye majonzi Makubwa

Waandishi wa Habari wakiwa katika msiba wa kwanza kutoka kulia ni Ndugu Joseph Mwaisango ambaye ni mwandishi mkuu wa Mbeya yetu Blog, Rais wa UTPC Keny Simabaya, pamoja na Felix Mwakyembe .

IMG-20120904-WA039.jpg


Waandishi wa Habari wakiwa wamebeba Mwili wa Marehemu kuelekea Makabirini

Wakiwa wanafanya ibada ya Mwisho kabla ya kuanza maziko

Hapa wakiwa wanashusha mwili wa marehemu katika Nyumba yake ya milele

Mwili wa Marehemu Daudi Mwangosi ukiwa Tayari katika Kaburi

Shughuri za kuzika zimeanza

Mazishi yanaendelea

Mke wa Marehemu Daudi Mwangosi akiweka Shada la Mauwa kwa machungu

Mke wa Daudi Mwangosi akiwa analia kwa uchungu katika Kaburi la Marehemu Mumewe



Watoto wa Marehemu wakiwawanaweka mashada ya maua sasa

Ni ngumu sana Kuamini kwa mke wa Marehemu lakini hali ndivyo ilivyo kuwa akiwa na huzuni kubwa

Dr Slaa akiweka Shada la Mauwa

Dr Slaa Baada ya kumaliza kutoa heshima za mwisho

Mh. Mark Mwandosya akiweka Taji la maua pamoja na mke wake

Rais wa UTPC akiweka shada la Maua
Ndugu wa Marehemu akiweka shada la Maua

Mwenyekiti wa Mbeya Press Club akiweka shada la maua


Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu, Ndugu Joseph Mwaisango akiwa anatoa heshima zake za Mwisho katiaka Kaburi

Wananchi wakiwa wanarejea baada ya mazishi


Waandishi wa Habari wakichukua Tukio Live `

Na huu Ndio Mwisho wa tukio zima la Mazishi ya Ndugu yetu, Mwanaharakati, Mpiganaji Daudi Mwangosi aliyekuwa Mwandishi wa Chanel 10.




 
Mbona naona mavazi ya CHADEMA hapo msibani yametawala sana ilihali ni msiba wa mwandishi wa habari?
 
R. I. P kamanda naamini damu yako haitapotea bure na ni ishara ya ukombozi kwa wa Tz upate pumziko la amani la milele
 
Naungana na dunia kulaani kitendo hiki cha kinyama. Tunaomba mkuu wa kaya utoe tamko. Naamini tofauti za kiitikadi haziwezi kuwa sababu za upotevu wa maisha ya watanganyika. Naamini chama changu makini hakiwezi kuhusika na utovu wa nidhamu wa watendaji ndani ya serikali yetu tukufu. waliousika na unyama huu, wabebe mzigo wenyewe, na msiba huu usitujengee chuki watanganyika.
 
Tunashukuru kwa picha.Poleni ndugu na jamaa wa marehemu,poleni watanzania wenzangu tunaopenda haki na kujali uhai wa wenzentu.Hongeleni mapolisi kwa mission yenu hii ya kuua rai wasio na hatia,hongereni wakuu wa polisi ambao haiwaumi hata kidogo,hongereni viongozi wa nchi ambao mnakumbatia uovu na hamchukui hatua yeyote kwa sababu mmeweka maslahi yenu mbele kuliko ya nchi na raia wake.
"You can choose your actions but you can not choose the consequences of your actions" and "never underestimate the power of your enemy."Ni hayo tu.
R.I.P Mwangosi
 
32 Reactions
Reply
Back
Top Bottom