BOB LUSE
JF-Expert Member
- Jan 25, 2014
- 3,738
- 3,198
Binadamu kiumbe cha mwenyezi Mungu kuishi nao ni kazi.wanapenda sana kushirikishwa kwenye taarifa za misiba,harusi lakini sio kuuguza mgonjwa au kusaidiwa kulipa karo za wanafunzi.
Kuna ndugu yangu nilimuuguza miaka michache iliyopita.sikupata ushirikiano wa ndugu wa karibu.kila mtu alikuwa busy na jiji la DAR.Mgonjwa alilazwa zaidi ya wiki mbili hospitali tofauti za hapa DAR,Ndugu wachache walikuja kumuona au kupiga simu.lakini wengi walipoteza mawasiliano.Bahata mbaya mgonjwa alifariki.Nikawapa taarifa wachache tu wale waliokuwa wanahangaika namimi huko mahospitali au kuuliza kwa simu.wengine nikawapotezea.
Nikaanza kupigiwa simu na watu waliokuwa hawana msaada wala mawasiliano na mimi nikiwa nauguza.niliwapuuza.wakaja msibani hazuiliwi mtu.nilikuwa na uwezo wa kukodi gari na kupeleka msiba mkoani nikawashirikisha walewale wachache walionijari na majirani.tukasafiri salama na kufika mkoa na kuzika.wale ndugu lawama waliokuwa hawana msaada huku DAR wakaitisha kikao kunilaumu kutowapa taarifa za msiba!! 'wabongo mnataka mpewe taarifa za msiba au msaidie kuuguza mgonjwa?'
Jana nimekumbuka hilo tukio baada ya ndugu yangu wa mbali kufariki.alivyokuwa anaumwa hakuna alikuwa anamjali wala kupokea simu yake.wakiogopa kuombwa hela.jana kafariki.saa moja millioni mbili za kusafirisha msiba na kuzika mkoa zilipatikana fasta! tunaenda wapi jamani.kama siyo jehanamu kuchomwa moto! upendo umepoa ndani ya jiji la DSM!
Karibu tuonyane kwa upole.