Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,438
Mh, umenikumbusha moja ya ndugu zangu Wachaga, Walipata msiba wa ghafla wa bibi wa bi harusi mwenye jina la bi harusi wakaficha hadi walipomaliza kula ndafu ndiyo asubuhi wakatangaza msiba...
ODM Asprin asiome hapa
Mkuu sina uhusiano wowote ila nilizisikia hizo habari toka chanzo cha karibu na bi harusi huyo!! Nikaona nilete hapa ili wajuzi wa mambo watufungue majicho...
Ok pole sana....
Mimi nimezisikia juu juu tu mahali fulani.
Acheni ushirkina, watu wanakufa kama kawaida.
Mkuu je hii kwa mila zenu huwa mnaiwekaje?? Maana humu kuna watu wamezaliwa Ocean Road na kukulia Upanga wala hawafahamu mila na desturi zao....
Ngoja leo nipime umri wa watu humu Mmu, kuhusu hii mada nitawapa majibu stahiki kesho.......
Nina rafiki yangu ni mzaramo moderate alitualika marafiki zake tumsindikize kwao Msanga kulikuwa na ngoma zao za kimila za kutoa wali (siyo ubwabwa ni mabinti)
Hizi ngoma za Wazaramo kwa kawaida huandamana na ngono zembe hasa yule mpiga goma huwa anasusa kupiga mpaka apewe mwanamke achachuwe kwanza.....
Lakini yule mzee Alwatan kwenye mkesha ule aliifunga kitaalam ile shughuri hakuna ngono iliyofanyika na hakuna mtu yeyote aliyejisaidia haja kubwa na pia alikamata anga na kuizuia mvua.
Kuwa uyaone, siyo magorofa.
Basi shusha neno la unabii kuhusu hii mada........
Ya kweli hayo?
Hata wewe!?
Ndugu yangu Matola,
Siyo watu wote wanaamini mambo ya ushirikina. Mimi ni mmoja wao na wakati mwingine huwa natamani kukutana ana kwa ana na hao wachawi!!
Hata hivyo, nakubali kuwa kuna watu wanaendekeza ushirikina hadi wamekuwa watumwa wa hayo mambo. Nadhani wanasiasa ndiyo wanaongoza!!
Bahati nzuri nimeona hata wachungaji wakiwatumia waganga wa kienyeji......
Kabla ya kifo chake Sheikh Yayha alikuwa rafiki mkubwa wa Mzee wa Upako.
Tembelea maeneo ya Gamboshi halafu ongea hii kauli kwamba huamini uchawi.
Gamboshi iko wapi kaka?
Kweli naweza kwenda nikaone mwenyewe....
Haijawahi kukaa kichwani kabisa hii biashara ya uchawi, wachawi wenyewe na wafuasi wao!
Naamini sitakaa niwe mmoja wa watumishi wao!