Msiba mkubwa mtaani Kwetu

Mamndenyi

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
31,259
2,000
Salaam sana wana MMU na wengineo wote;

Ilikuwa ni juzi ijumaa jirani yetu amepata balaa la kuunguliwa na nyumba;

Kwa kifupi;
Baba mwenye nyumba alimwacha mkewe wa ndoa akaamua kuvuta ndani house gel;

Mke wa ndoa kwa kihoro haikuchukua muda Mungu akampumzisha;

Maisha yakaendelea, mjakazi ambaye sasa ndo mama mwenye nyumba akajaliwa mtoto wa kiume tuseme mtoto alikuwa na miaka mitatu hadi minne;

Hiyo Ijumaa sasa;
Mama ameenda kwenye shughuli zake mtoto amebaki home na house gel,
haikujulikana kana ni shoti ya umeme au ni mtoto aliwasha kiberiti ndani
moto ukaanza kidogo kidogo, house gel badala akimbilie kumwokoa mtoto akaanza kutoa vyombo vya ndani
akamsahau mtoto, ile majirani wameona moto wakimbilie kwanza kuhangaika kufungua geti ili wafike ndani moto
ndo umezidi;

Wakamkuta house gel anajaribu kutoa vyombo vya ndani nje, kuuliza mtoto yuko wapi, kumbe alimsahau ndani;
ni majonzi na huzuni kubwa, kweli yule mtoto kaungulia ndani hadi kaisha kabisa;

Mbaya zaidi baba mwenye nyumba yuko kifungoni kutokana na kosa la kukutwa na pesa za bandia;


.................... Mtanisamehe pale ambapo sikueleweka vizuri, ni kiswahili kinanishinda.............
 

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,808
2,000
Hii Mamndenyi umekosea sana, ungeiuza kwenye magazeti ya udaku ungeshamalizia kile kibanda chako kule Kibaha.
Naanza kupata wasiwasi kama wewe ni Mchaga kweli.

Aisee umeshaharibu dili, maana wadaku wameshakuwahi na sasa timu yao iko eneo la tukio wanakusanya habari. Yaani kwa kupitia chanzo chako hiki watu wanajitengenezea mkwanja kiulainiiii...... LOL
 
Last edited by a moderator:

miss chagga

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
57,917
2,000
yeleuwiii jamani mtoto... house gilr aliogopa kukatwa mshahara vyombo vikiungua.. kwa sababu akipasua sahani au kikombe imekula kwake
 

Mamndenyi

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
31,259
2,000
Heee,
Mie ni mshamba sana sijui kutafuta hata hizo pesa;
Ipo ingine nayo moto hata hii ni cha mtoto pale pale mtaani kwetu
waambie tu niwape halafu mkwanja tunagawana nusu kwa nusu.

Hii Mamndenyi umekosea sana, ungeiuza kwenye magazeti ya udaku ungeshamalizia kile kibanda chako kule Kibaha.
Naanza kupata wasiwasi kama wewe ni Mchaga kweli.

Aisee umeshaharibu dili, maana wadaku wameshakuwahi na sasa timu yao iko eneo la tukio wanakusanya habari. Yaani kwa kupitia chanzo chako hiki watu wanajitengenezea mkwanja kiulainiiii...... LOL
 

miss chagga

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
57,917
2,000
Una akili sana wewe anti yangu
hata jana pale chachi kwetu wameyasema haya
yakuwakata hawa watu mishahara.

ila hiyo tabia ni mbaya sana... ile ni ajali kazini saa nyingine unamfokea sauti mbaya hadi anatetemeka ndo maana alikumbuka vitu akasahau utu,,.. na kwa kuwa yeye mwenyewe afanyiwi vizuri
 

HARUFU

Platinum Member
Jan 21, 2014
28,317
2,000
yeleuwiii jamani mtoto... house gilr aliogopa kukatwa mshahara vyombo vikiungua.. kwa sababu akipasua sahani au kikombe imekula kwake
Bora angekubali kukatwa kuliko msiba ambao umeleta hasara mara tatu, (i)uhai wa mtu hauwezi rudishwa
(ii)nyumba nayo imeteketea
(iii)baba mwenye nyumba ameenda lupango
 

miss chagga

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
57,917
2,000
so SAD...yani huyo hg sijui ningemfanyaje sijui

sasa huna cha kufanya ... kama akisema sahani imepasuka mtoto alirusha mguu wakati nampa uji ukamakata mshahara yeye alifanya kilichokkua sahihi kwa wakati ule huku akili ikiwa imesongwa na wasi wasi bosi atanielewaje
 

miss chagga

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
57,917
2,000
Bora angekubali kukatwa kuliko msiba ambao umeleta hasara mara tatu, (i)uhai wa mtu hauwezi rudishwa
(ii)nyumba nayo imeteketea
(iii)baba mwenye nyumba ameenda lupango
lazima ujue mkuu ukifanya kosa moja jua unamakosa mia mbele yako usipokuwa makini...... yeye alikuwa anaokoa mali za bosi wake asikatwe mshahara kwa sababu angeweza afanye kazi mwaka mzima bila kulipwa,... mmi naona house girl kafanya kilichokuwa sahihi kabisa... huyo mama angemtengenezea mazingira ya kumjali mtoto kuliko mali zake sidhani kama angeweza fanya hiyo mistake kabisa... aliwekewa mazingira ya kujali mali kuliko utu na ndo amefanya implementation sasa hapa mabosi wa nyumbani tujifunze kwa kweli msitengenezee watumwa wenu mazingira ya woga.... wafundishwe zaidi utu
 

Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
13,195
2,000
Mamndenyi Malipo ni hapa hapa duniani, housegirl ali mkick mama mwenye nyumba hadi umauti ukampata. Yule aliyezaa amekufa, ile nyumba kwishney, the so called mume lupango!!! Unataka Mungu akuhukumu vipi tena!!! Ole wenu manungayembe mnamendea waume za watu, hata kama ni Hgilrl anatakiwa amwambie mama mwenyenyumba kam mume anamtongoza. Siku zote tenda wema nenda zako na kuwa mwaminifu hata kwa jambo dogo ili Mungu awe mwaminifu kwa mambo yako. Sifurahii mtoto amekufa ila tu nataka uone jinsi Mungua anavyofanya kazi yake. Iogope ndoa ya mtu kama ukoma.
 

everlenk

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
11,604
2,000
Duh! Kweli Mungu yupo, Malipo hapahapa dunian, mwisho wa ubaya aibu.,vyote kapoteza.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom