Huyo aliyeyakagua na kutoa wito wa kutokutumika ni nani? Sisi tumefika pale miaka ya 98 tukaambiwa mara yamekaa upande sijui yameegama, mara sijui yametitia upande, lakini hatukuwahi kuona tatizo hata siku moja zaidi ya kukatika kwa zile kingo za kwenye viambaza vya nje. Mimi sidhani kama uongozi wa UDSM ni mzembe kiasi hicho kwamba usijui hali halisi ya majengo hayo. Hakuna kiongozi yeyote wa chuo ambaye anapenda wanafunzi wengi kiasi kile wanaoishi kwenye vyumba hivyo wafe. Bila shaka wamejiridhisha na usalama wake ndiyo maana wamewaacha wanafunzi humo. Hao walioumia walianguka kutoka vyumbani au ilikuwaje? Na kwanini waanguke, au pressure? Huko unakosema kuyumba, ni mechanism ya majengo yote ya Ghofofa kufanya hivyo kwa ajili ya shock absorption.kaka ungekuwa umelala mle siku ya tukio ungejua namaanisha nini hata wale makauzu walikimbia kma wewe ulimaliza na akina samwel sitta enzi hizo pita kesho uyachungulie ujionee nyufa