mtafuta-maisha
JF-Expert Member
- Nov 5, 2016
- 1,982
- 2,934
Mwaka 2010 Skinner alikuwa amekaa gerezan kwa miaka 15, akiwa amejaribu kukata rufaa mara kadhaa na kukataliwa. Tarehe 24, mwezi wa 2 mwaka 2010, Skinner alihamishiwa kwenye kitengo cha unyongaji kilijulikanacho kama HuntsVille Unit kilichopo katika jimbo la Texas. Hapa ndipo watuhumiwa wengi wa mauaji USA huletwa kwa ajili ya kunyongwa. Muda wake wa kunyongwa ulipangwa kuwa ni saa 6 kamili mchana.
Owen na wenzake walitoa pingamizi la kujaribu kuzuia zoezi la kunyongwa kwa Skinner lakini hawakufanikiwa. Muda ulikuwa unakimbia. Owen alimwambia Skinner kuwa, “Sikia Skinner ninataka niwe mkweli juu ya hili, ni kwamba naona huu ndiyo mwisho wake hivyo jiandae maana tumejaribu njia zote imeshindika hivyo jiandae kwa kunyongwa”.
Emily ambaye mwaka 2010 alikuwa ni mtayarishaji wa vipindi vya CNN (nadhani mnamkumbuka huyu ndiye alikuwa mkufunzi awali), alikuwa akifuatilai hiyo kesi kutoka kwenye chumba cha habari huko Atlanta. Akiwa ana ujauzito wa miezi mitano wakati huo, alisimama na kupiga kelele kuwa kuna mtu amepangiwa kunyongwa huko Texas siku hiyo, na amekuwa akiomba ushaidi ufanyiwe vipimo vya DNA, tafadhali waandishi wa habari nawaomba hili tukio lisipite hivi hivi bila kuangaziwa macho.
Kwa upande wa Sandrina ambaye alikuwa akifuatilia kesi hii kwa zaidi ya miaka 10, hii kesi kwa sasa alikuwa anaichukulia kama yake. Sandrina aliwambia rafiki zake na wafanyakazi wenzake kuwa kunajambo hamjui kuhusu maisha yangu. Aliwambia kuwa kaolewa na mumewe atanyongwa siku hiyo huko Texas. Sandrina na Skinner walikwua wakiandikaina barua kwa miaka 12, na mara kadhaa alikuwa akimtembelea gerezani, walijikuta wakianzisha mahusiano ya kimapenzi na wakaoana mwaka 2008.
Sandrina na familia ya Skinner waliruhusiwa kumuona kwa mara ya mwisho. Mtoto wa Skinner aliyemuacha akiwa na umri wa miaka mine alikuwa hamkumbuki baba yake wakati mtoto wake mwingine aliyemuacha akiwa mdogo kabisa alikuwa hamjui kabisa baba yake. Siku hiyo ndiyo walikuwa wanamuona baba yao na kufanyika utambulisho upya ambao huenda ulikuwa ni utambulisho na mara ya mwisho ya kumuona baba yao.
Akiwa gerezani anaambiwa kuwa familia yake inakuja kumuona anaambiwa kuwa ajaribu kuwa jasiri, naye anajibu kuwa atakuwa ajsiri kwa ajili ya wanaye na mkewe na wanafamilia wengine kwa kutoonyesha masikitiko. Na kweli anapozungumza na familia yake anawashauri kwamba wakitoka hapo wapande ndege warudi makwao kama hakuna kilichotokea ila tu wamkumbuke kwa mazuri aliyofanya akiwa pamoja nao. Akiwa anazungumza nao askari anakuja anamtaarifu muda wa kuzungumza umekwisha anamuondoa kwenye simu bila hata kumpa nafasi ya kuwambia kwaheri.
Kachero Stubblefield aliendesha gari mwendo wa maili 500, kushuhudia Skinner akinyongwa, ambapo yeye andai kuwa alimuahidi mama yake Twila kuwa ataenda kushuhudia muaji wa manaye na wajukuu zake akinyongwa hivyo alitaka kutimiza hiyo ahadi. Pia anadai yeye ni kati ya watu wanaounga mkono adhabu ya kifo kwa watu amabo hasa wametenda mauaji. Anaongeza kuwa asamehewe kwa mtazamo wake kama utakuwa unamkera mtu lakini Biblia inasema Jicho kwa jicho na yeye ndicho anachounga mkono.
Saa nne kamili, Skinner alipewa mlo wake wa mwisho na kuombewa mara ya mwisho kutoka kwa mchungaji. Baada ya hapo alianza kuandaliwa kwa ajili ya kupelekwa kwenye chumba cha kunyongea ambacho kimezungushiwa nondo huku upande wa pili ni sehemu kwa ajili ya watazamaji ambapo familia ya anayenyongwa na askari pamoja na viongozi wa serikali ndiyo wanaoruhusiwa kushuhudia.
Stubblefield na baadhi ya wanafamiila wa Skinner ndiyo walikuwa eneo la kushuhudia. Akiwa analetwa kutoka kwenye vyumba vya ndani kuelekea kwenye chumba cha kunyongea kwa ajili ya kufungwa kwenye kitanda cha kunyongea, mara simu inaita na habari inayoletwa ni kwamba Mahakama ya Juu kabisa (supreme court) imesitisha zoezi la kunyongwa kwako. Skinner anakosa la kusema, anshindwa zungumza, anashindwa kuhema vizuri, mate yanamkauka anahisi furaha na majonzi kwa pamoja.
Familia wanapopata hii habari wanalipuka kwa furaha na vilio pia maana ulikuwa kama muujiza. Simu ile ilikuwa imepigwa na Owen ambaye kumbe muda wote alikuwa bado hajakata tama alikuwa akihangaika kuangalia namna ambavyo anaweza kuzuia zoezi hilo.
Stubblefield na wanafamilia wanatoka kwenye kile chumba cha kushuhudia na wanakutana na watu wakiwa na mabango wakiwa wanaandamana kupinga kunyongwa kwa Skinner na mabango yakiwa yanataka vipimo vya DNA vifanyike. Stubblefield anaingia kwenye gari lake na kuondoka huku hajaridhishwa na maamuzi hayo.
Owen anadai hii ilikuwa ni kesi ya aina yake ambayo ilikuwa ni rahisi kukukatisha tamaa. Anadai kwamba japo mahakama ya juu ilisitisha kunyongwa kwake kwa muda huo, ilikuwa inaabidi warudishe shauri lao mahakama ya wilaya na kuanza upya.
Mwaka mmoja baada ya maamuzi ya mahakama ya juu, kusitisha kwa muda kunyongwa kwa Skinner, jimbo la Texas linabadiri sheria zinazohusiana na kupima DNA, na hii ilimpa nafasi Owen kuweza kupima ushahidi wote uliopatikana kwenye eneo la tukio.
Koti lile lilikutwa pembeni ya mwili wa Twila ndio ushahidi wa msingi ambao owen alitegemea, kutokana na sheria mpya ofisi ya mwendesha mashitaka ilimtaarifu Owen kuwa wamekubari kufanya vipimo lakini kuna tatizo moja, hawana lile koti eti limepotea. Skinner alipopata hii taarifa alishangaa kwamba wamepanda kwa muda mrefu wakijaribu kuiomba ofisi ya mwanasehria ikubari kupima DNA lile koti na sasa wanapokubari wanadai limepotea katika mazingira ya kutatanisha.
Ofisi ya mwanasheria inadai kwamba uwa inatokea kwa bahati mbaya mara nyingine ushahidi unachanganywa au unapotea wakati wa kusafirishwa kutoka chumba cha kuhifadhia ushahidi kupelekwa mahakamani lakini anadai kwamba ni makosa ya kibinadamu na hainabudi kukubari kwamba makosa hufanyika na kutarajia makosa mara nyingine.
Owen yeye anadai hakuna sababu inayoweza kueleza na kueleweka ushahidi mkubwa kama lile koti lilivyokuwa kubwa, inawezekanaje ukapotea hivi hivi tu, anaendela kudai kwamba inashangaza zaidi hasa kwenye kesi hiyo ambapo wameweza kuhifadhi hata ushahidi wa vitu vidogo kama kucha zilizookotwa eneo la tukio na nywele lakini koti lipotee. Owen anadai kwamba mwaka 2005 wakati wakipagania rufaa ya Skinner, aliwapata anfasi ya kumuuliza John aliposimama mahakamani kama shahidi na alimuuliza anafikiri kwamba kitengo cha polisi cha Pampa kilikuwa na uwezo wa kuchunguza na kukusanya ushahidi kwenye eneo la uharifu kama huo ambao uko kwenye kesi hiyo. Jibu la John lilikuwa Hapana kabisa. Sidhani kama hiki kitengo cha polisi kina uwezo unaohitajika kufanya hivyo.
Kutokana na kutokuwepo kwa koti hilo basi lisingeweza kutumika kama ushahidi hivyo walifanya vipimo vya vitu vingine, ofisi ya mwanasheria mkuu ilidai kwamba matokeo ya vipimo hivyo yalishindilia msumari juu ya uhusika wa Skinner kwenye mauaji hayo. Msaidizi wa mwanasheria mkuu anadai kwamba vipimo vilionyesha kwamba damu aliyokuwa nayo Skinner ilikuwa imesambaa kila mahali, kuanzia suruali alilokuwa amevaa maeneo ya miguu, sehemu za kola la shati lake, mikononi, ndani ya meneo ya miguu ya suruali lake, sehemu ya nyuma na oembeni ya nguo zake na hii hali wanadai isingeweza kutokea isipokuwa kama alikuwa anatembea tembea wakati damu ikiwa inaruka.
Owen yeye anadai kwamba inajulikana kwamba Skinner alikuwa na jeraha mkononi alilopata baada ya kuchanwa na kisu alichokuwa nacho huyo mtu anayedai alipozinduka alikuta kasimama mbele yake, na huenda ndio chanzo cha damu ile kuruka nyuma ya nguo zake.
Pia vipimo vilionyesha kwamba alama za kiganja chenye damu iliyoachwa kwenye Mlango wa chumba cha Gray ilikuwa sawa na kiganja cha Skinner. Kile kisu kilichoachwa mlango hakikuwa na damu ya Skinner jambo ambalo Owen anadai kwamba kama kweli Skinner ndiye muaji kile kisu ilibidi kiwe na damu yake pia maana atakuwa alikuwa kakishikiria wakati ana jeraha kwenye kidole basi kungekuwa na mchanganyiko wad emu za marehemu na damu yake lakini vipimo vilionyesha hakikuwa na damu ya Skinner.
Taulo iliyokutwa kwenye mfuko ule mweusi pamoja na kisu, ilikutwa ina DNA ya mtu asiyefahamika. Hiyo taulo ilikutwa na damu ya Twila na DNA ya mtu mwingine asiye Skinner wala watoto wa Twila. Pia kluna DNA ilikutwa upande wa pili wa taulo hiyo ambayo inafahamika ni ya nani, hiyo DNA ni ya mtaalamu wa masual ya DNA ambaye pia alikuwa shahidi upande wa serikali. Dna yake ilikutwa kwenye vitu viwili kisu pamoja na taulo.
Hii inadhihirisha kuwa hawa atu hawakuwa makini na kuhifadhi ushahidi kama waliweza kuhifadhi na kuushika ovyo ovyo mpaka huyo anayeitwa matalaamu anaacha DNA yake kwenye ushahidi ni jambo la ajabu sana.
Jaji alifikia hitimisho kuwa ushahidi mpya ulikuwa haujitoshelezi kubadiri uamuzi wa majaji waliotoa hukumu ya kwanza. Aliendelea kusema kuwa hata huu ushahidi ungekuwepo toka mwenzo huenda majaji wa mwanzo wangempa adhabu ile ile.
Baada ya zaidi ya miaka 20, ya mapigano ya kujaribu kumuokoa Skinner na mamiliona ya dola kutumika katika kulipia msaada wa kisheria, Skinner bado anasubiri kutekelezwa adhabu yake ya kunyongwa huku bado akishikiria msimamo wake kuwa hakuhusika. Leo skinner tumaini lake limebakia kwenye kurudia tena upimaji wa DNA, na kama hakuna jambo jipya litakalopatikana kwenye zoezi hilo tarehe yake mpya ya kunyongwa itapangwa.
John yeye anadai kwamba anaona pesa nyingi na muda uliotumiaka na wanaomtetea Skinner umetosha, hakuna njia nyingine zaidi yahiyo adhabu kutekelezwa. Msaidizi wake John yeye anasema haingii akilini kuwa ulikuwa umelala unashituka unakuta mpenzi wako na watoto wameuawa na mbele yako kuna mtu mwenye kisu unatoka ndani umekimbia, unaelekea kwa mpenzi wako wa zamani akushine jeraha lako hata hujishughulishi kutoa taarifa polisi halafu baadae unakuja kudai kuwa hukuhusika.
John anadai yeye hana shaka kuwa Skinner alihusika na siku ya kunyongwa ikapangwa ataenda kushuhudia akinyongwa bila shaka.
Hitimisho: kuna mambo mengi sikoyaandika kwenye kisa hiki ila nina amini Skinner alihusika kwenye mauaji hayo. Kwa mfano akiwa gerezani aliweza kuipenyezewa simu mabyo aliitumia kumtishia mwendesha mashitaka wa Texas, polisi vamia anapolala kujaribu kutafuta hiyo simu hawakuipata ila walikuta line za simu mbili kwenye Biblia aliyokuwa nayo. Baadaye walimpiga X-ray iliyoonyesha kuwa alikuwa na simu kwenye utumbo wake.
Hii inadhihirisha kuwa Skinner alikuwa ni muarifu mzuri tu.
Mpaka leo Skimmer bado anasubiri kunyongwa.
**********************mwisho****************************
pia una weza soma makala zangu zifuatazo kwa kufuata link hapo chini
Wakala wa kifo alivyowatesa polisi katika kesi ya aina yake
Ndoa na malaika wa kifo (Hadithi ya kweli kuhusu mauaji
Kilio marehemu kudai haki toka kaburini baada ya miaka 30...