Mshitakiwa Kesi Ya EPA Ajiua kwa Risasi

Mshitakiwa Kesi Ya EPA Ajiua kwa Risasi

Tanzania ukiwa na skendo ya wizi tu basi "unakufa!"
 
Heri mjambazi wote wanaoliibia taifa letu wangepata laana ya kujitoa roho ingependeza sana.

jai-chotalal-somani-mtuhumiwa-epa-ajiua-kwa-risasi.jpg



Marehemu Jai Somani (kushoto, mwenye shati la kijani) alipokua akiingia mahakamani na watuhumiwa wenzake, enzi za uhai wake
MSHITAKIWA katika kesi ya wizi wa zaidi ya Shilingi bilioni 5 za Benki Kuu ya Tanzania kutoka katika Akaunti
ya Madeni ya Nje ya Benki Kuu ya Tanzania (EPA), Jai Chotalal Somani amejiua kwa kujipiga risasi.
Mshitakiwa huyo anadaiwa kujiua jana
asubuhi nyumbani kwake, mtaa wa Mindu, Upanga katika Manispaa ya Ilala. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Parang Somani ambayeni kaka yake hajui kwa nini mdogo wake amejiua.


Source - habarileo
 
kwa hiyo kafa bila kurudisha pesa zetu.?
 
Wanabodi nimekutana na hii kitu kwenye gazeti la mwananchi;


MSHTAKIWA wa kesi ya wizi wa Fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), katika Benki Kuu ya Tanzania, Ajay Somani

amefariki dunia baada ya kujipiga risasi.

Habari zilizolifikia Mwananchi Jumamosi wakati tunakwenda mitamboni na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, zinasema kuwa Jay alijipiga risasi jana asubuhi, maeneo ya Upanga karibu na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

“Alijipiga risasi saa 2 asubuhi nyumbani kwake Upanga, karibu na Hospitali ya Muhimbili.”, alisema Kamanda Minangi na kuongeza kuwa haijajulikana tukio hilo kwa kwa hakuacha ujumbe wowote.

Jay alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya wizi wa pesa hizo kiasi cha Sh5.9, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, yeye pamoja na ndugu yake Ajay Soman, ambaye anatumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatika na hatia katika kesi nyingine ya EPA.

Mbali na ndugu hao wawili, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Kanda wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Rajabu Maranda na binamu yake Frijala Hussein, ambao tayari wanatumikia kifungo gerezani baada ya kupatikana na hatia katika kesi nyingine tatu za EPA.

Katika kesi hiyo, washtakiwa wengine ni waliokuwa wafanyakazi wa BoT, Ester Komu, aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Madeni na Bosco Kimela aliyekuwa Kaimu Katibu wa BoTna Imani Mwakosya, ambapo walisomewa maelezo ya awali Julai 26, 2012 na kesi hiyo iko katika hatua ya usikilizwaji wa mashahidi wa upande wa mashtaka.

Mwisho
 
Huyu ni binadamu, tunastahili kusikitika kwa kifo chake japo amejiua. Je ingekuwa mmoja wa jamaa yako ungejisikiaje?
 
Hii habari ilishajadiliwa kwa kina humu JF tangu jana.
 
Huyu ni binadamu, tunastahili kusikitika kwa kifo chake japo amejiua. Je ingekuwa mmoja wa jamaa yako ungejisikiaje?
Wewe umeiona maiti yake? ukiambiwa mwili wake umeshachomwa moto wanataka kuzika majivu itakuingia akilini? kichwa kazi yake si kufugia nywele.
 
Hii itakuwa ni movie ya kihindi starling kafa mwanzo wa picha.Habari leo ufisadi ccm.Je kama kafa kweli watauza mali zake kurudisha hela zetu au ndio kafa na kesi.
 
Huyu ni binadamu, tunastahili kusikitika kwa kifo chake japo amejiua. Je ingekuwa mmoja wa jamaa yako ungejisikiaje?

siyo kila mtu lazima umsikitikie akifa..yaani mtu kamuua mama na baba yako bado una muonea huruma au ni unafiki tu au kwa wewe mtu unaepaswa kuwa na chuki nae ni yule atakae kufa akiku fi..
 
Kama ajarudisha pesa zetu basi tuchukue petrol station zake,
1 ya kwa Nyerere mikocheni
2 Karibu hotel maisha club
3Nyingine mtaa wa jamhuri
 
kwa hiyo kafa bila kurudisha pesa zetu.?

nijuavyo; asilimia 90 ya watuhumia wa EPA walitumiwa na chama chenu na familia zao hazikufaidi pesa hizo, hatupaswi kuwatuhumu na kuwalaani. wabaya wetu bado tunao majukwaani.
 
kwa serikali yetu mtu akiwa hai kesi inachukua 4ever sasa huyu amekufa sijui itakuwaje.
 
Hii Kesi ya wizi wa pesa za EPA kulikua na ushirikiano BOT
Jee wangapi kati ya walohusika BOT wameunganishwa na kesi hizi?
Kurejesha itakuwa ngumu kwani hapo tunazungumzia mgao
Waligawana na wahusika wengine lakini zigo wamepachikwa wao

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Kafa wapi?
Kuna,alieiona maiti yake?
Hawa jamaa hua wanachomaga watu, so wanaenda wanachoma mabua then tunazugwa ndie wakati mtu anakula kuku Canada

mi nawasi wasi kakimbilia India kwao
 
attachment.php

Marehem Jai Somani mwenye tshirt ya kijani

MSHITAKIWA Katika kesi ya wizi wa zaidi ya Sh bilioni tano za Benki Kuu ya Tanzania kutoka katika Akaunti ya Madeni ya Nje ya Benki Kuu ya Tanzania (EPA), Jai Somani amejiua kwa kujipiga risasi.

Mshitakiwa huyo anadaiwa kujiua jana asubuhi nyumbani kwake katika mtaa wa Mindu,Upanga katika Manispaa yaIlala.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Parang Somani ambaye ni kaka yake, hajui kwanini mdogo wake amejiua lakini hapo awali Jai alikuwa akisumbuliwa na tatizo la msongo wa mawazo.

Jai alikuwa anakabiliwa na kesi hiyo pamoja na kaka yake Ajay Somani ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela pamoja na kulipa faini ya Sh.milioni 400 baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya wizi wa Sh bilioni 2.2 kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupitia akaunti ya EPA.

Jai, Ajay na washitakiwa wengine wanne wanakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kesi hiyo bado inaendelea.

Parang alisema maandalizi ya maziko yanaendelea nyumbani kwa marehemu katika mtaa wa Mindu.

Akizungumza na gazeti hili Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alithibitisha Jai kujiua na kuwa polisi wanaendelea na
upelelezi wa chanzo cha kifo chake kwa kuwa hajacha ujumbe wowote.

Washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka matano ya kula njama, kughushi, kuwasilisha hati ya kuhamisha deni iliyoghushiwa, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kujipatia ingizo la kiasi hicho cha fedha kutoka BoT.

Source. Habari leo

Unadaiwa BILIONI 5 Faini MILIONI 400 Nadhani sijaelewa faini ya nini???
 
Back
Top Bottom