Mshitakiwa Kesi Ya EPA Ajiua kwa Risasi

Mshitakiwa Kesi Ya EPA Ajiua kwa Risasi

Sasa amekufa deni le2 vp?hivi hakuna sheria ya kuidai maiti?2nataka che2
 
R.I.P. Somani
Kesi iendelee mpaka mwisho, deni litalipwa na alioshirikiana nao

Sikujua kama kuna kesi ya EPA sasa slaa huwa anaongea vitu gani kumbe kuna watuhumiwa wana kesi; mkuu Mungi hebu nijuze.

Chama
Gongo la mboto DSM
cc Ritz
 
Last edited by a moderator:
attachment.php

Marehem Jai Somani mwenye tshirt ya kijani

MSHITAKIWA Katika kesi ya wizi wa zaidi ya Sh bilioni tano za Benki Kuu ya Tanzania kutoka katika Akaunti ya Madeni ya Nje ya Benki Kuu ya Tanzania (EPA), Jai Somani amejiua kwa kujipiga risasi.

Mshitakiwa huyo anadaiwa kujiua jana asubuhi nyumbani kwake katika mtaa wa Mindu,Upanga katika Manispaa yaIlala.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Parang Somani ambaye ni kaka yake, hajui kwanini mdogo wake amejiua lakini hapo awali Jai alikuwa akisumbuliwa na tatizo la msongo wa mawazo.

Jai alikuwa anakabiliwa na kesi hiyo pamoja na kaka yake Ajay Somani ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela pamoja na kulipa faini ya Sh.milioni 400 baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya wizi wa Sh bilioni 2.2 kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupitia akaunti ya EPA.

Jai, Ajay na washitakiwa wengine wanne wanakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kesi hiyo bado inaendelea.

Parang alisema maandalizi ya maziko yanaendelea nyumbani kwa marehemu katika mtaa wa Mindu.

Akizungumza na gazeti hili Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alithibitisha Jai kujiua na kuwa polisi wanaendelea na
upelelezi wa chanzo cha kifo chake kwa kuwa hajacha ujumbe wowote.

Washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka matano ya kula njama, kughushi, kuwasilisha hati ya kuhamisha deni iliyoghushiwa, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kujipatia ingizo la kiasi hicho cha fedha kutoka BoT.

Source. Habari leo

Mimi wasiwasi wangu ni kuwa ALIYEKUFA NI YEYE KWELI?? Hawa ndugu zetu wenye asili ya Asia mambo ya usanii wanayamudu.....TUSIJEKUWA NA MWILI WA MDOSI MWINGINE KABISA WAKATI MSHTAKIWA KAENDA KUANZA MAISHA MAPYA nchi nyingine....
 
Huyu atakuwa ametwangwa risasi ili kuizima case taratibu..! Yaani nidaiwe bilioni 5 nijiue? Never on earth
 
Hata kama alikuwa na hiyo kesi, basi nianze mimi kuandika RIP Jai maana kila mmoja anauliza na kuzidai hizo pesa. RIP Om shanti om shanti
 
usikute hata hajafa,wanatupiga changa la macho,huenda kasepesha zake kwenda India,Uingereza,USA,Canada na kwingeneko
 
Hatakuwa kajiua ila kauawa ili kupoteza ushahidi. Jk atakuwa analijua hilo.
 
Kama kweli kajiua kafanya uamuzi sahihi, kwa sababu yeye alipoiba hizo hela alisababisha watanzania wengi kufa kwa kukosa huduma muhimu
 
Mwili umeonekana? mazishi yamefanyika? au kafa kama Balali tu....
 
Back
Top Bottom