Mshitakiwa Kesi Ya EPA Ajiua kwa Risasi

Mshitakiwa Kesi Ya EPA Ajiua kwa Risasi

Duuh tusipoangalia tutakumbuka shuka angali kumeshakucha, lazima mmoja afe, afe sababu ya wengi simama inuka kwa ajili ya Taifa.

sijakuelewa mmoja afe ili kuokoa taifa au ni Kafara?
 
Hapo ndo watu wanakosea(kujiua)! Ukiwa na tatizo acha mpaka likuue lenyewe! Kidini tunaamini kuna mbinguni na motoni lakini hakuna mwenye uhakika! Si ajabu ukifa ndo basi, you go nowhere! Komaa mpaka mwisho ufe naturally!
 
wahindi ndo wenye hii nchi hii kuanzia kina rostam....wao wanaishi kwenye nyumba zetu sie tumebanana uswahilini..
 
Nenda baba nenda, umaskini uliotusababishia na ukutangulie mbele ya kiti cha hukumu, na Mungu ailaze roho yako panapostahili.
 
Bouncer; Hakianani haya mawazo yako ninaiunga mkono!

wao serikali ndo wametufikisha hapa! ofcoz sio vizuri ku-doubt kifo cha mtu esp. kama taarifa imetolewa na ndugu wa damu kabisa, but ktk sarakasi hizi hizi za epa kuna mazingaombwe mengi, hivyo ni lazima tuhoji authenticity ya taarifa kama hizi!
 
Mahakama zetu nazo haziko fair mtu anaiba bilioni 2.2 unamfunga miaka 2 na faini ya milioni 400 zingine ni sadaka au sielewi hapo
 
Wakati anajiua nani alikuwepo. Tutajuaje kama alijiua??!!

We elewa tu amekufa huruhusiwi kuhoji hili jambo limeshafika polisi. Kuhusu mzishi atachomwa nyumbani kwake hakuna kupiga picha.
 
Hapa pesa tu na ikiwezekana kaburi lake watupie pingu mpaka hukumu isomwe
 
atakuwa kavushwa mipaka huyo akina sobhai walisindikizwa mpaka mpakani kukimbia kesi
 
MSHITAKIWA Katika kesi ya wizi wa zaidi ya Sh bilioni tano za Benki Kuu ya Tanzania kutoka katika Akaunti ya Madeni ya Nje ya Benki Kuu ya Tanzania (EPA), Jai Somani amejiua kwa kujipiga risasi.

Mshitakiwa huyo anadaiwa kujiua jana asubuhi nyumbani kwake katika mtaa wa Mindu,Upanga katika Manispaa yaIlala.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Parang Somani ambaye ni kaka yake, hajui kwanini mdogo wake amejiua lakini hapo awali Jai alikuwa akisumbuliwa na tatizo la msongo wa mawazo.

Jai alikuwa anakabiliwa na kesi hiyo pamoja na kaka yake Ajay Somani ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela pamoja na kulipa faini ya Sh.milioni 400 baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya wizi wa Sh bilioni 2.2 kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupitia akaunti ya EPA.

Jai, Ajay na washitakiwa wengine wanne wanakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kesi hiyo bado inaendelea.

Parang alisema maandalizi ya maziko yanaendelea nyumbani kwa marehemu katika mtaa wa Mindu.

Akizungumza na gazeti hili Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alithibitisha Jai kujiua na kuwa polisi wanaendelea na
upelelezi wa chanzo cha kifo chake kwa kuwa hajacha ujumbe wowote.

Washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka matano ya kula njama, kughushi, kuwasilisha hati ya kuhamisha deni iliyoghushiwa, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kujipatia ingizo la kiasi hicho cha fedha kutoka BoT.

Source. Habari leo
Babalao, isije kuwa ni KIINI MACHO kumbe mtu katoweka NCHINI, ukizingatia hakuna last respect!!!!!!!!!mh! Lolote lawezekana!!!!!

Si unakumbuka hadithi ya yule mzee mwingine wa EPA, mpaka leo hakuna aliyeona kaburi, wala kushuhudia mazishi!

Anyway God knows, maombi ya kuikomboa TZ yanaendelea mwaka 2013 kwa kasi ya ajabu, mpaka kieleweke.

Queen Esther
 
Jamaa shujaa kwa kukataa kwenda kuwa mke wa mtu
 
Babalao, isije kuwa ni KIINI MACHO kumbe mtu katoweka NCHINI, ukizingatia hakuna last respect!!!!!!!!!mh! Lolote lawezekana!!!!!

Si unakumbuka hadithi ya yule mzee mwingine wa EPA, mpaka leo hakuna aliyeona kaburi, wala kushuhudia mazishi!

Anyway God knows, maombi ya kuikomboa TZ yanaendelea mwaka 2013 kwa kasi ya ajabu, mpaka kieleweke.

Queen Esther

queen hata wale wa KAGODA wako kwenye mchakato wa kujiua.
KUJIUA = KUTOROKEA NJE.
 
Ayaa tumesha kula hasara

Most likely!
Tujue wana bodi maana ya limited liability!
Fedha hiyo si ajabu ilikwisha tangulizwa India , UK au Canada ambako mkono wa Kova au TRA haufiki kirahisi.
 
Back
Top Bottom