Mshitakiwa Kesi Ya EPA Ajiua kwa Risasi

Mshitakiwa Kesi Ya EPA Ajiua kwa Risasi

babalao 2

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
5,426
Reaction score
3,308
attachment.php

Marehem Jai Somani mwenye tshirt ya kijani

MSHITAKIWA Katika kesi ya wizi wa zaidi ya Sh bilioni tano za Benki Kuu ya Tanzania kutoka katika Akaunti ya Madeni ya Nje ya Benki Kuu ya Tanzania (EPA), Jai Somani amejiua kwa kujipiga risasi.

Mshitakiwa huyo anadaiwa kujiua jana asubuhi nyumbani kwake katika mtaa wa Mindu,Upanga katika Manispaa yaIlala.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Parang Somani ambaye ni kaka yake, hajui kwanini mdogo wake amejiua lakini hapo awali Jai alikuwa akisumbuliwa na tatizo la msongo wa mawazo.

Jai alikuwa anakabiliwa na kesi hiyo pamoja na kaka yake Ajay Somani ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela pamoja na kulipa faini ya Sh.milioni 400 baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya wizi wa Sh bilioni 2.2 kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupitia akaunti ya EPA.

Jai, Ajay na washitakiwa wengine wanne wanakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kesi hiyo bado inaendelea.

Parang alisema maandalizi ya maziko yanaendelea nyumbani kwa marehemu katika mtaa wa Mindu.

Akizungumza na gazeti hili Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alithibitisha Jai kujiua na kuwa polisi wanaendelea na
upelelezi wa chanzo cha kifo chake kwa kuwa hajacha ujumbe wowote.

Washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka matano ya kula njama, kughushi, kuwasilisha hati ya kuhamisha deni iliyoghushiwa, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kujipatia ingizo la kiasi hicho cha fedha kutoka BoT.

Source. Habari leo
 

Attachments

  • jai-chotalal-somani-mtuhumiwa-epa-ajiua-kwa-risasi.jpg
    jai-chotalal-somani-mtuhumiwa-epa-ajiua-kwa-risasi.jpg
    13.9 KB · Views: 1,185
Hizo pesa kama kweli alichukua kesi bado ipo hai ina maana family yake ndo itakua inatumia hizo pesa kesi ya madai inaendelea hapo.
 
Ndio yeye keshakufa, laki je, hela zetu kesha lipa?
 
Hizo pesa kama kweli alichukua kesi bado ipo hai ina maana family yake ndo itakua inatumia hizo pesa kesi ya madai inaendelea hapo.

Huyo atakuwa amejitoa mhanga ili familia yake iishi vizuri bila usumbufu.
 
Hata kama kajiondoa ama wamemuondoa ili waimalize kesi, bado haijasaidia. TUNATAKA mtandao mzima ukamatwe, uhukumiwe na utaifishwe. Kama nchi hatuwezi kuzama kwenye matatizo makubwa sababu ya uchu wa watu wachache.
 
Wasiishie kuchunguza sababu ya yeye kujiua,ila waende mbali kidogo kwa kuchunguza hatma ya fedha za walalahoi.
 
R.I.P. Somani
Kesi iendelee mpaka mwisho, deni litalipwa na alioshirikiana nao
 
Kwa kesi ya madai itaendelea na family yake itarudisha pesa zetu ingekua kesi ya jinai ingefutwa.

Kwa hyo kesi iko palepale?
Ila usishangae ikiundwaTUME YA KUCHUNGUZA KIFO CHAKE.
 
ooo..bhabhaa hii baya sana! dugu yetu jiua kisa pesa ya EPA...Tanjania imekuwa chungu, huko ahera dugu tasema nini mbele ya Mungu...oooh
 
Serikali ya JK ni ya kihuni sana, tunahitaji udhibitisho wa picha na video..hawakawi kutufanyia kama walvyofanya kwa Balali, pili sisi hatumtak mtu tnataka chetu, mama zetu wengi bado wanajfungulia sakafuni huku wadogozetu wakiendelea kukatia 'gogo' vichakani.....
Jamani hii nchi inahitaji shujaa haraka sana kusafisha huu ukoko wa uozo wa a.k.a Dhaifu!
 
Kutikana na tukio hili, tunaomba kesi zote za UFISADI apewe yule aliyumuhukumu kijana wa Mererani aliyepiga picha na G. Lema huku akiwa amevaa nguo za kijeshi. Namna hii tutakuja ambiwa watuhumiwa wote wamekufa na kesi zimeishia.
 
Hizo pesa kama kweli alichukua kesi bado ipo hai ina maana family yake ndo itakua inatumia hizo pesa kesi ya madai inaendelea hapo.

Wahindi ni Watu wenye kuweza fanya lolote juu ya fedha UK...wapo wanauchukua life insurance then wana commit suicide ili watoto wao wapate fedha....sio ajabu huyu kujiuwa ili familia ibaki na fedha
 
Ushughulikiaji wa wizi wa kupitia EPA na utoroshaji wa pesa kupeleka Uswizi ni USHAHIDI WA UDHAIFU WA KIWANGO CHA JUU KUPAT KUTOKEA.
 
Duuh tusipoangalia tutakumbuka shuka angali kumeshakucha, lazima mmoja afe, afe sababu ya wengi simama inuka kwa ajili ya Taifa.
 
Back
Top Bottom